Bomoabomoa ya kufa mtu Dodoma inaendelea

Bomoabomoa ya kufa mtu Dodoma inaendelea

Mkuu read between the line,wanasema mkuu ni mbaguzi kwani hata Machinga wqlifurushwa kuanzia dar ya Kariakoo na Makonda na kukawa kweupe dar hadi Ubungo ila zoezi lilipofika Mwanza akasema waachwe wapiga kura wake na the same applied kwenye bomoa bomoa!!
Between the lines vp tena.punguzen ujuaji asee dom ni chama tawala damdam na lazima ilo eneo liandaliwe kna mradi mkubwa unapita huko
 
Sio kweli kuwa mradi utaanza baada ya mwaka miwili, mradi huu umeshaanza na kampuni ya Yapi Merkezi ambayo imeanza kujenga awamu ya kwanza ambayo inaishia Morogoro ndiyo hiyo ambayo imepewa awamu ya pili ya tayari wameshasaini mkataba na serikali kwa hiyo kwa sasa wanafanya mobilization ili waanze rasmi moja ya vitu wanavyohitaji ni Eneo la kufanya Kazi. Tayari uongozi wa Mkoa Una taarifa rasmi za ujio wa maofisa wa reli ambao wamevunja hizo nyumba ambazo ziliingia maeneo ya reli, Jamani waacheni watu wafanye kazi yao
 
Nchi yetu inashida ya uongozi tangu zamani. Nyerere hakuweka utawala wa sheria na ndiyo maana tunajifanyia mambo kiolelea. Ninashindwa kuamini kwamba kituo cha mafuta kinajengwaje kwenye sehemu ya reli. Hiyo michoro hakuna afisa aridhi wa wilaya aliyeipitisha kwa kujiridhisha mwenyewe kwamba hiyo sehemu siyo ya mtu. Is a shame.
 
Watu wa hivyo unawaacha wafurahishe jukwaa... Na viongozi wa wafanyabiashara walikuwa hawafikishi kila kitu kwa wafanyabiashara kwenye vikao mbalimbali walivyokuwa wanakaa,,hili jambo walishaambiwa sana sana.. Kibinadamu lazima uwaonee huruma maana vijana waliwekeza kwaajili ya kujipatia riziki,pa kwenda kwa sasa ndo mtihani,sabasaba kumejaa basi tabu tu.

Manisapaa walilijua hili,unajiuliza fensi waliojenga kuzunguka stand ya mkoa tena kwa kutumia kodi za wananchi walikuwa wanaweza nn,na wakajenga wakawekewa x
Bifu ya CDA na Manispaa hiyo. Fence iliwekewa X na CDA enzi hizo ndo mtawala wa Dodoma Mji. CDA kuondolewa Manispaa wakamalizia uzio huo. Mwenye kiwanja kaja anadai mali yake na hivyo kubomoa sehemu asizozihitaji na kuacha huo uzio kwa ajili ya kazi maalum. Naishauri Manispaa ikomae ibomoe huo uzio!
 
Hili ndo tatizo kubwa la Watanzania wengi,

Ukiwapa miezi mitatu wanapenda sana kujiongeza na kufanya miaka mitatu.

Sasa walishataadharishwa toka Novemba mwaka jana wakajiongeza na kufanya yao na sasa mda umefika wanasema mda ULIKUA MCHACHE SANA NA HAWAKUJIANDAA.

Huu ushahailifu si mzuri hata kidogo na unachelewesha sana shughuli za kimaendeleo.

Any way, pleni sana ila kwa wengine iwe fundisho.

Mkipewa notice muizingatie na si kujiongeza ongeza.

Over and out
 
Watanzania wengi tumelala sana na tunasumbuliwa na tatizo sugu la kujiongeza.

Tukiambawa tuhame na tukapewa na muda maalum wa kuhama hua tunapenda sana kujipa moyo na kudhani ni utani tu ama mzaha wa serikali na hatimaye mda ukifika tunakua mstari wa mbele kulalamika kua Serikali inatuonea ama muda mliotupa na mfupi sana na hautoshi kuhamisha mali zetu.

Huu ni uzembe na unahitaji kuachwa mara moja na wanaojielewa.

Poleni sana ila iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kujiongazaongeza.

Over and out
 
Mwenzako akinyolewa basi wewe tia maji.

Leo wanabomolewa wa Idodomia na kuna wengine weengi tu wamewekewa X sasa sijui nao wanasubiri nini!!!!! au wanasubiri Greda ndo waanze kulalamika Serikali inawaonea wakati muda ndo huu!!!!
 
DODOMA: Kampuni Hodhi ya Usimamizi wa Reli (RAHCO) wameanza kubomoa nyumba zilizo karibu na hifadhi ya reli kupisha ujenzi wa reli ya kisasa

Wananchi walioathirika na zoezi hilo wamesema wamepewa muda mchache wa kuhama na mali zao zimeharibika na kuwasababishia hasara kubwa

Ofisa uhusiano wa RAHCO, Catherine Mushi amesema walitoa notisi ya kuwabomolea tangia mwezi Novemba mwaka jana

Bomoa bomoa hiyo linategemewa kuchukua siku 3 hadi 5 na watu walio katika hifadhi ya reli hawatalipwa




===============================

Hivi sasa hapa Dodoma ineandelea bomoabomoa ya kufa mtu.Vibanda vya biashara vingi vimenjwa ikiwa ni pamoja na ofisi za Shabiby na kituo cha mafuta cha ORYX kilichokuwa nyuma ya jengo la Shabiby.

Jengo la kampuni ya mabasi ya Shabiby lilikuwa bado jipya kabisa baada ya kulijenga upya hivi karibuni.

Kituo cha mafuta cha TOTAL kilichokaribu na stand ya Jamatani wao angalau wamefanikiwa kuokoa pump zao na wananyonya mafuta yaliyoko chini kwenye matenki.

Benki ya NMB nao ndio wanajaribu kuokoa mashine zao 3 za ATM zilizokuwakuwa zimefungwa katika kituo hiki cha mafuta cha TOTAL.

Kwa ujmla watu wengi sasa wanahangaika kuokoa mali zao.Zoezi limeanza saa 10 jioni hii na kuna taarifa wananchi walitangaziwa ingawa wengine wanasema hawakutarajia kuwa itakuwa ni leo.

Ukweli ni kuwa ajira nyingi sana zisizo rasimi zimeathirika maana vibanda vya biashara vilivyovunjwa ni vingi mno na eneo lililoathirika ni kubwa sana.

Eneo hili tunaambiwa ni mali ya Shirika la Reli nchini.

Ulinzi ni mkali.

Hawa wananchi cha kufanya ni kuweka record zao za gharama au ikipidi wafungue kesi mahakamani ili kusaidia kuweka record zao sawa .alafu wasubiri awamu itakayo fuata maana hakuna namna itakuwa ya kulipa fidia hasara iliyopatikana tuu.
 
Duh aisee nilikuwa siamini hadi nimepitiliza kituo kumbe kweli shabiby terminal imelala down
 
Ikiwezekana hata bunge maana nahisi lipo kwenye hifadhi ya barabara.
Mkuu kama ni kweli watunga sheria ndio wavunja sheria hakuna haja ya kubomoa jengo la bunge taratibu ni kulilipua haraka na baruti
Ili angalau wapate likizo ya miaka 3 bila kufanya vikao na bila posho.Tokea hapo halipo live kwenye TV
 
Back
Top Bottom