Bomoabomoa ya kufa mtu Dodoma inaendelea

Bomoabomoa ya kufa mtu Dodoma inaendelea

Hawa TRL waende Nairobi wakaone serikali imewezaje kujenga reli kutoka Mombasa mpaka Nairobi bila kubomoa makazi ya watu. Kwanini kituo cha kushushia ama kubebea abiria kisijengwe nje ya Dodoma badala ya kulazimisha kijengwe kwenye kituo cha zamani.[/QU
Mkuu hakuna cha kujifunza kutoka Kenya kwa sababu zifuatazo
1-Kenya ardhi ni mali ya mtu binafsi sio ya serikali
2-Hakuna aliyevamia sehemu ambayo siyo yake akawekeza
3-Reli ya kisasa ilipopita ni sehemu halali ya shirika la reli Kenya
Hapa kweli
1-Ardhi si mali ya mtu,bali ni mali ya serikali
2-Serikali inakodisha ardhi yake kwa wawekezaji kwa miaka ama 33 ama 66 ama 99
3-Sehemu walipowekeza wawekezaji,kwa maana wamachinga pale DODOMA halikuwa eneo lao.
4-Sisi Watanzania tumezoea kuvamia maeneo,na kuwekeza bila kufuata utaratibu,matokeo yake tunafanya shughuli zetu kisiasa zaidi,badala ya kiserikali,matokeo yake ni kubomolewa kila kukicha.
 
SAWA. JE JAMTIN NA LILE KANISA PALE KAMA UNAELEKEA SARAFINA BAR, VIPI NA ZENYEWE. JE ZIMEVUNJWA?
inasemekana ukuta ulio upande wa SARAFINA ndio utakaobomolewa km mita7 kurudi ndani ambapo utavifikia vyoo na shule ya chekechea, Kanisa lenyewe la KKKT litabaki ingawa ukiangalia uhalisia lipo ndani ya eneo la Railway kulingana na bar ya Arctic Open Bar
 
Hawa wananchi cha kufanya ni kuweka record zao za gharama au ikipidi wafungue kesi mahakamani ili kusaidia kuweka record zao sawa .alafu wasubiri awamu itakayo fuata maana hakuna namna itakuwa ya kulipa fidia hasara iliyopatikana tuu.
Ufanye trespassing halafu ulipwe fidia !?
Labda awamu ya chadema
 
HUMAN FACE

AKIJA RAIS ANAYETOKA KANDA NYINGNE, ATAANZA NA MWANZA, KIROHO SAFI.
 
Nchi yetu inashida ya uongozi tangu zamani. Nyerere hakuweka utawala wa sheria na ndiyo maana tunajifanyia mambo kiolelea. Ninashindwa kuamini kwamba kituo cha mafuta kinajengwaje kwenye sehemu ya reli. Hiyo michoro hakuna afisa aridhi wa wilaya aliyeipitisha kwa kujiridhisha mwenyewe kwamba hiyo sehemu siyo ya mtu. Is a shame.
Rushwa huwa haifuti sheria, sheria na hadhi na eneo hubaki katika hali yake halisi ! Taratibu za kubalidilisha atumizi ni ndefu ikiwemo kufikishwa kwa waziri husika. Ukipewa eneo/kiwanja kujenga shule, ukaamua kujenga kiwanda basi unahitaji kibali, na kina process ndefu sana ikiwemo kuwaomba ridhaa wakazi na serikali ya mtaa iliyo kuzunguka. Ndio maana watu wanao jenga viwanda kwenye makazi hupata wakati mgumu wakati wote. Mwenye petro station kalazimisha apewe hapo kwa pesa yake. Hivyo hivyo open space ndivyo hugaiwa.
 
Wagogo ndio no.1 kuipa ccm kura.
kwa hiyo?
je kuhamia CCM ni ugogo
huyo Slaa na Mtulia ni wagogo?
hapa tunazungumzia eneo halali la Railways miaka yote na si Dodoma tu wanakobomoa hata km ni Mwanza wamevamia eneo hilo na kujenga watabomolewa
Tafuta kiwanja halali na lipia hutabomolewa na wakija unalipwa kwanza stahiki zako
 
c3e7c5b5b46ca2338096715f7d00e323.jpg
e07fa819e67150d985fad99da4917555.jpg

Ofisi za mabasi ya ABC
7d6794c4728251937e8ae0c0afff9d67.jpg

(Kwa Mwansasu) ilipokuwa Railways Club kulikokuwa kukifanyika vikao vya sherehe kila mwishoni mwa juma pia ofidi za mabasi ya Safari Njema
00daf0f8569f666d40760d64b98a3f7f.jpg

Sun Set (Mpepo au kwa Kimei)
df3fe65e24a98ea40aab5a0db7aa1259.jpg

nyuma ya stand ya Daladala za Mjini (Artic open Bar) inapopakana na ukuta wa Kanisa la Kilutheri
b46743d7caf3d272483639cb4c7382a4.jpg
Hawa wote walikuwa wanajua hiyo sehemu siyo yao ndo maana majengo si ya kudumu !
 
Hii ni awamu ya kuvunja tu hadi muishi kama mashetani
 
Tutaisoma namba mpaka miaka mitano iishee dodoma si makao makuu ya chama
 
Allah awapesubira kwa msiba huo unaendelea dodoma ,serikali ndio yenyemaamuzi ya mwisho kwa mambo yetu ya kidunia hivyo watu wamuombe Allah awape zaidi ya hivyo vilivyo haribiwa
 
Sheria inafuata mkondo! Uzuri hakuna anayeonewa, wako watu walijua wana makosa ila wakawa wanademadema wakati wa awamu zile. Sasa awamu ya utekelezaji iko kazin
Isipokuwa Mwanza tu, kwakuwa walitupigia kura.
 
Back
Top Bottom