Bomoabomoa ya kufa mtu Dodoma inaendelea

Tukumbuke kuwa awamu ya pili ya ujenzi wa standard gauge imeshasainiwa hadi Dodoma,contractors ni haohao Waturuki ni lazima sasa wanahitaji eneo ambalo reli hiyo itapita kwa ajili ya maandalizi ya awali kwa hiyo zoezi hilo ni sahihi maana wakicheleweshwa kupatiwa maeneo ya reli hiyo inapopita watadai waongezewe muda na wananchi wa maeneo hayo walishapewa taarifa na x ziliwekwa muda mrefu kuwa wahame
Taarifa iliwafikia wafanyabiashara wote tangu 6Novemba2016 walikaidi kama kawaida yao. Hakuna wa kulaumiwa
 
shabiby ana eneo kubwa pale petrol station yake anaweza hamishia pale ofisi na akapajenga upya sio mwenzao hao walalahoi wapambane na hali zao tu!..
 
Hivi sasa hapa Dodoma ineandelea bomoabomoa ya kufa mtu.Vibanda vya biashara vingi vimenjwa ikiwa ni pamoja na ofisi za Shabiby na kituo cha mafuta cha ORYX kilichokuwa nyuma ya jengo la Shabiby.

Jengo la kampuni ya mabasi ya Shabiby lilikuwa bado jipya kabisa baada ya kulijenga upya hivi karibuni.

Kituo cha mafuta cha TOTAL kilichokaribu na stand ya Jamatani wao angalau wamefanikiwa kuokoa pump zao na wananyonya mafuta yaliyoko chini kwenye matenki.

Benki ya NMB nao ndio wanajaribu kuokoa mashine zao 3 za ATM zilizokuwakuwa zimefungwa katika kituo hiki cha mafuta cha TOTAL.

Kwa ujmla watu wengi sasa wanahangaika kuokoa mali zao.Zoezi limeanza saa 10 jioni hii na kuna taarifa wananchi walitangaziwa ingawa wengine wanasema hawakutarajia kuwa itakuwa ni leo.

Ukweli ni kuwa ajira nyingi sana zisizo rasimi zimeathirika maana vibanda vya biashara vilivyovunjwa ni vingi mno na eneo lililoathirika ni kubwa sana.

Eneo hili tunaambiwa ni mali ya Shirika la Reli nchini.

Ulinzi ni mkali.

Weka na chachandu basi kunogesha habari
 
unajua ni bora ubomoe wakati mradi unakaribia kuanza kama vile tanesco ubungo lakini mradi wa tren ya umeme baada ya miaka miwili hi si sawa
 
Inasemekana eneo siyo la railway wala nini bali wamechukua serikali wanajenga maghorofa
Hapana ni hivi like eneo ni la railway ata kuangalia kuna baadhi ya miundombinu ya shirika la reli ila imeachwa .

Ishu ni ivi like eneo ilikuwaga Mali ya railway manispaa ndo wakawa wameomba shirika la reli waanze kulitumia wakawaruhusu kulitumia lakini kwa shughuli temporary sasa manispaa wao wakajenga masoko hadi stand wakawa wanakusanya ushuru pia wakawauzia na wafanya biashara kama akina shabby wakajenga halimashauri wakajenga na ukuta wa stand kutoza ushuru vizuri ndo railway wakawawekea bomoa ndo ishu imeenda mahakamani railway wameshinda miundombinu ya manispaa yote inaondoka yakiwemo masoko na stand .Kama utakuwa unapafahamu utaona kabisa kama Ile stand ya kisasa ipo katika makazi ya wafanyakazi wa reli.

Kingine usisahau wale wanajenga reli za kisasa wanaandaa mazingira kwa ajiri ya bandari kavu.Nachokisema nakijua kwa asilimia zote mkuu
 
Kule Mwanza zile nyumba elfu 3 kwenye eneo la reli ni reli ya Sudan ndio maana akakataza Bomoa bomoa?!@
Mambo ya mwanza sijui mi naongeleaga maswala ya dodoma niliko na ninayoyafahamu kwani mwanza nako ulikuwepo mgogoro kati ya shirika la reli na manispaaa?mwanza wanajenga standard gauge?mwanza wanajenga bandari kavu?
 
Hapana ni hivi like eneo ni la railway ata kuangalia kuna baadhi ya miundombinu ya shirika la reli ila imeachwa .

Ishu ni ivi like eneo ilikuwaga Mali ya railway manispaa ndo wakawa wameomba shirika la reli waanze kulitumia wakawaruhusu kulitumia lakini kwa shughuli temporary sasa manispaa wao wakajenga masoko hadi stand wakawa wanakusanya ushuru pia wakawauzia na wafanya biashara kama akina shabby wakajenga halimashauri wakajenga na ukuta wa stand kutoza ushuru vizuri ndo railway wakawawekea bomoa ndo ishu imeenda mahakamani railway wameshinda miundombinu ya manispaa yote inaondoka yakiwemo masoko na stand .Kama utakuwa unapafahamu utaona kabisa kama Ile stand ya kisasa ipo katika makazi ya wafanyakazi wa reli.

Kingine usisahau wale wanajenga reli za kisasa wanaandaa mazingira kwa ajiri ya bandari kavu.Nachokisema nakijua kwa asilimia zote mkuu
Ni kweli lile lilikuwa eneo la railway ma walishaambiwa waondoke mpaka kuwekewa X.. Railway imeshinda kesi na trh 1/12/2107 walipita kuwatangazia wahamishe Mali zao kwa usalama wa mali zao wanabomoa. So hakuna namna
 
Kweli mkuu watu wengine hawajui wanaleta siasa eti serikali inataka kujenga ghorofa sijui
 
Back
Top Bottom