Bomoabomoa ya kufa mtu Dodoma inaendelea

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,837
2,000
DODOMA: Kampuni Hodhi ya Usimamizi wa Reli (RAHCO) wameanza kubomoa nyumba zilizo karibu na hifadhi ya reli kupisha ujenzi wa reli ya kisasa

Wananchi walioathirika na zoezi hilo wamesema wamepewa muda mchache wa kuhama na mali zao zimeharibika na kuwasababishia hasara kubwa

Ofisa uhusiano wa RAHCO, Catherine Mushi amesema walitoa notisi ya kuwabomolea tangia mwezi Novemba mwaka jana

Bomoa bomoa hiyo linategemewa kuchukua siku 3 hadi 5 na watu walio katika hifadhi ya reli hawatalipwa===============================

Hivi sasa hapa Dodoma ineandelea bomoabomoa ya kufa mtu.Vibanda vya biashara vingi vimenjwa ikiwa ni pamoja na ofisi za Shabiby na kituo cha mafuta cha ORYX kilichokuwa nyuma ya jengo la Shabiby.

Jengo la kampuni ya mabasi ya Shabiby lilikuwa bado jipya kabisa baada ya kulijenga upya hivi karibuni.

Kituo cha mafuta cha TOTAL kilichokaribu na stand ya Jamatani wao angalau wamefanikiwa kuokoa pump zao na wananyonya mafuta yaliyoko chini kwenye matenki.

Benki ya NMB nao ndio wanajaribu kuokoa mashine zao 3 za ATM zilizokuwakuwa zimefungwa katika kituo hiki cha mafuta cha TOTAL.

Kwa ujmla watu wengi sasa wanahangaika kuokoa mali zao.Zoezi limeanza saa 10 jioni hii na kuna taarifa wananchi walitangaziwa ingawa wengine wanasema hawakutarajia kuwa itakuwa ni leo.

Ukweli ni kuwa ajira nyingi sana zisizo rasimi zimeathirika maana vibanda vya biashara vilivyovunjwa ni vingi mno na eneo lililoathirika ni kubwa sana.

Eneo hili tunaambiwa ni mali ya Shirika la Reli nchini.

Ulinzi ni mkali.
 

MAUBIG

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
997
1,000
Hivi sasa hapa Dodoma ineandelea bomoabomoa ya kufa mtu.Vibanda vya biashara vingi vimenjwa ikiwa ni pamoja na ofisi za Shabiby.

Kwa sasa watu wanahangaika kuokoa mali zao.Hili zoezi limeanza jioni hii.
Walitangaziwa tangu jana wavunje ni vibanda vinavyozunguka stendi kuu kama sikosei,
 

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,992
2,000
Hivi sasa hapa Dodoma ineandelea bomoabomoa ya kufa mtu.Vibanda vya biashara vingi vimenjwa ikiwa ni pamoja na ofisi za Shabiby.

Kwa sasa watu wanahangaika kuokoa mali zao.Hili zoezi limeanza jioni hii.
Ka picha tafadhali mkuu
 
  • Thanks
Reactions: BAK

shululu

JF-Expert Member
Jan 26, 2015
28,111
2,000
IMG-20171202-WA0024.jpg
IMG-20171202-WA0023.jpg
IMG-20171202-WA0022.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom