Bomoabomoa itakavyoyumbisha taasisi za kifedha

Bomoabomoa itakavyoyumbisha taasisi za kifedha

Sijui ni kwa nini watu wanajitia upofu kwa kujifanya hata wao wanaishi kwenye maeneo yaliyopimwa. Tanzania nzima ni asilimia chini ya kumi ya ardhi ndiyo imepimwa. Na uhalali wa kuwa kwenye ardhi si kuwa na "Title deed" bali ni kuwa kihalali kwenye eneo husika.

Hivi vijijini ni wangapi wana hizo "title deeds" ambazo watu wanauliza kama watu wa Kimara walikuwa nazo, na jee kutokuwa na "title deeds" kunafanya nyumba yako kuwa "Condemned" na serikali? Jee kuaharamishwa kwa leo huko mbele ya safari kutakuwa halali?

Hawa watu waliobomolewa leo walikuwa hawalipi kodi za serikali, jee mipango miji walipoweka Namba kwenye nyumba hizo walikuwa wanawalaghai wamiliki wake? Watu wa mitaa hiyo walipowekewa serikali za mitaaa na mitaa yao ilitambulikaje na Serikali kuu na tume ya Uchaguzi kama walikuwa pale kiharamu? Miaka yote hiyo na shughuli zote hizo zilizokuwa zinatambuliwa na serikali ilikuwa ni danganya toto?
 
  • Thanks
Reactions: RMC
Yaani serikali ina wajibu wa kupanga miji lakini yenyewe haipangi, halafu wakija kubomoa nyumba zilizojengwa kiholela kutokana na uzembe wa serikali nyie mnaita "Planing"!?
Allen,tafadhali huo uzembe tumezembea wote yaani serikali na raia..unajenga kwenye road reserve bila kujua unadhani nini kitatokea?labda hata ushakufa unaachia watoto urithi hewa. Tupende tu kujifunza vinginevyo tutapata hasara kila siku,na kwa vile kukubali kosa ni ngumu tutamtupia lawama serikali tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haijakugusa hii ndo maana unaongea kama unajisaidia.... Ingekuwa wazazi wako au mwana familia yoyote imemgusa usingeongea upumbavu wako....

send via satellite-Vietnam
Yalitugusa kabla hujajuwa kuna jiji linaitwa Dar. Tulibomolewa majumba wakati wa upanuzi wa mtaa wa Msimbazi tukalipwa Shillingi 25. Thamani kamili ilikuwa zaidi ya Shillingi 750.

Ulikuwepo wakati thamani ya nyumba Shillingi 750?
 
Nyumba nyingi sana Dar zitabomolewa. Zimejengwa kiholela tu.

Halafu wakimaliza hizo waanze na nyumba ambazo zipo chini ya viwango.
 
Allen,tafadhali huo uzembe tumezembea wote yaani serikali na raia..unajenga kwenye road reserve bila kujua unadhani nini kitatokea?labda hata ushakufa unaachia watoto urithi hewa.
Hakuna hata mtu mmoja ambaye anazembea isipokuwa serikali ndiyo inazembea. Tanzania watu wanajenga nyumba kwa fedha zao binafsi na si kwa kutegemea fedha za serikali. kwa mantiki hiyo kunakobomolewa leo zama hizo yalikuwa ni mashamba tu ya watu binafsi ambao waliuza maeneo hayo kwa wengine. Serikali ina wajibu wa kupima Ardhi lakini ni kwa nini mpaka sasa Ardhi waliyopima haifiki hata asilimia 20?

Pili eneo linalobomolewa sasa halikuwa sehemu ya hifadhi ya barabara kwani hapo mwanzo hifadhi ya barabara haikuwa na sheria inayotumika hivi sasa. Kwa maana nyingine sheria ilitungwa wakati tayari watu wako pale na hapo wanasthaili kufikiriwa.

Nina miaka 19 nafuatilia kiwanja changu kipimwena hakipimwi halafu baaadaye anatokea mtu anasema nimejenga kiholela! FaizaFoxy hiyo Kariakoo yenu ulipimwa enzi za Mkoloni. Hivi wale ndugu zako wa Vingunguti kiembe mbuzi na kule Tandale kwa mtogole maeneo yao yamepimwa na kupangwa?
 
Maendeleo hayaji bila bomoa bomoa. Si nyumba tu, hata misingi ya utu inabidi ibomolewe. Hujaona watu wa jinsia moja wanaoana, tena cha ajabu wengine ni wachungaji wa kondoo wanaoana na kondoo zao.

Misingi ya utu inabomolewa na kanisa linabariki kwa kuwa wameendelea itakuwa serikali kubomoa nyumba kupisha highways? Fikiri.
Kwahiyo na wewe tukubali umebomoka akili maana umeendelea?
 
Mimi naendelea ku figure out eneo la hifadhi ya bara bara la mita 120 each side! Naamini ni railway hiyo!
 
Kwahiyo na wewe tukubali umebomoka akili maana umeendelea?

Usipoguswa ni rahisi kutapika upupu wa ana yeyote.Hata JKN alisema kwenye Kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo.

Huwezi kuwafanya watu wako masikini kosa unapanua Barabara ambazo kwa.miaka hata 20 haitafanyika
 
kweli mkuu ukumbi wa harusi kama kilato pale kimara ni uwekezaji mkubwa sana... kitendo cha kuubomoa kama ana loan bank anaweza asilipe na usimfanye chochote maana dhamana imevunjwa... au mama kapinga pale
Mikopo ina bima dhidi ya matukio km hayo kikiwemo kufariki kwa mkopaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom