Hakuna hata mtu mmoja ambaye anazembea isipokuwa serikali ndiyo inazembea. Tanzania watu wanajenga nyumba kwa fedha zao binafsi na si kwa kutegemea fedha za serikali. kwa mantiki hiyo kunakobomolewa leo zama hizo yalikuwa ni mashamba tu ya watu binafsi ambao waliuza maeneo hayo kwa wengine. Serikali ina wajibu wa kupima Ardhi lakini ni kwa nini mpaka sasa Ardhi waliyopima haifiki hata asilimia 20?
Pili eneo linalobomolewa sasa halikuwa sehemu ya hifadhi ya barabara kwani hapo mwanzo hifadhi ya barabara haikuwa na sheria inayotumika hivi sasa. Kwa maana nyingine sheria ilitungwa wakati tayari watu wako pale na hapo wanasthaili kufikiriwa.
Nina miaka 19 nafuatilia kiwanja changu kipimwena hakipimwi halafu baaadaye anatokea mtu anasema nimejenga kiholela!
FaizaFoxy hiyo Kariakoo yenu ulipimwa enzi za Mkoloni. Hivi wale ndugu zako wa Vingunguti kiembe mbuzi na kule Tandale kwa mtogole maeneo yao yamepimwa na kupangwa?