Bomoabomoa itakavyoyumbisha taasisi za kifedha

Bomoabomoa itakavyoyumbisha taasisi za kifedha

Kama wewe unapinga hilo na wengine wanapinga ubomoaji wa nyumba za raia wasio na hatia bila ya kufuata kanuni za kiutu ambazo ni kutathimini mali zilizopo, na kulipa fidia, kutumia ubinadamu kwenye ubomoaji!

Wapeleke kesi mahakamani kama wanaona wameonewa.
 
Sijawahi kuona Kiongozi ambaye lengo lake kuu la uongozi wake ni kukomesha wananchi .
 
Ndiyo maana Tanzania haiendelei kwa kuwa na watu wenye akili kama hizi. Kwenye hili bandiko umeona nimeandika CCM ama Magufuli?
Mimi nimetoa mapendekezo tu. Kwani ni pendekezo baya kwa Lowassa kuwalipia?
 
Kuna makosa makubwa yanafanyika ila watu wanatii tu kwa woga. Hiyo barabara kubwa hivyo inakwenda wapi? Kwa nini tusianzishe mji mpya kama kweli tunataka maendeleo? Huwezi pata maendeleo katika mji wa Dar uliobanana hivi. Mji mpya bagamoyo ama kibaha ingekuwa dawa tu.
Na kutipa mtu na kutompa ardhi ya mbadala ni dhambi kubwa kwa seriki.
 
Ukitaka kumuu mbwa mpe jina baya. wemeitwa "wavamizi wa hifadhi ya barabara" na wavamizi wakiondolewa hakuna fidia!
Mkuu sina hakika sana kwa sasa sheria ipi ilikiukwa na wahanga lakini nimefanikiwa kuiona kanuni ya 27 ya sheria ya hifadhi ya barabara ya mwaka 2007 ambayo imeainisha umbali tofauti wa hifadhi kutoka kwenye barabara kuanzia pale makutano ya bara2 ya umoja wa mataifa na morogoro eneo la fire, ukizingatia mabadiliko ya sheria hii kwa kipindi hicho na historia majengo yaliyovunjwa ni wazi wahanga wameonewa na serikali sababu wakati inafanyiwa mabadiliko wengi walikuwepo hapo. Tafute kwenye google mtaiona halafu tujadili hii issue
 
Maendeleo hayaji bila bomoa bomoa. Si nyumba tu, hata misingi ya utu inabidi ibomolewe. Hujaona watu wa jinsia moja wanaoana, tena cha ajabu wengine ni wachungaji wa kondoo wanaoana na kondoo zao.

Misingi ya utu inabomolewa na kanisa linabariki kwa kuwa wameendelea itakuwa serikali kubomoa nyumba kupisha highways? Fikiri.
wewe nae unazeeka vibaya, udini wa nini hapa?
 
Maendeleo hayaji bila bomoa bomoa. Si nyumba tu, hata misingi ya utu inabidi ibomolewe. Hujaona watu wa jinsia moja wanaoana, tena cha ajabu wengine ni wachungaji wa kondoo wanaoana na kondoo zao.

Misingi ya utu inabomolewa na kanisa linabariki kwa kuwa wameendelea itakuwa serikali kubomoa nyumba kupisha highways? Fikiri.
upo sawa but nani alaumiwe kati ya yule aliyejenga na kuishi miaka 20 na yule aliyekuwa anasimamia upande wa serikali na hakutimiza wajibu wake wa kuwaelekeza wanachi?. je kwa kushindwa kuwaelekeza wanachi kuwa hapa si mahala sahihi pa kujenga haitoshi kuwa kigezo cha kulipa fidia?
 
Wizara ya aridhi watoke maofisini, watu wengi wanauziana viwanja kienyeji enyeji kiasi kwamba ni ngumu sana, kupeleka maendeleo sehemu husika
 
Wapeleke kesi mahakamani kama wanaona wameonewa.

Kweli kabisa @ Madam for the matter of sincerity ! Sometimes tunapaswa kujaribu kuwa fair! Swala la Upanuzi wa barabara ni muhimu sana Kwa maendeleo ya Taifa letu! Binafsi nimekuelewa vizuri @ Madam!
 
Maendeleo hayaji bila bomoa bomoa. Si nyumba tu, hata misingi ya utu inabidi ibomolewe. Hujaona watu wa jinsia moja wanaoana, tena cha ajabu wengine ni wachungaji wa kondoo wanaoana na kondoo zao.

Misingi ya utu inabomolewa na kanisa linabariki kwa kuwa wameendelea itakuwa serikali kubomoa nyumba kupisha highways? Fikiri.
Bi shungi, dini yako ya sudusu nane ya kumi ya theluthi ya mali ya marehemu mumeo ndio dini nzuri wote tunajua, lakini hapa hatujadili mitala na talaka, tupo kimara. Kama huna cha kuchangia si uache wanaume watete, au kwa misingi wa dini yako siku hizi nawe ni mume kwa kuwa mjane?
 
Maendeleo hayaji bila bomoa bomoa. Si nyumba tu, hata misingi ya utu inabidi ibomolewe. Hujaona watu wa jinsia moja wanaoana, tena cha ajabu wengine ni wachungaji wa kondoo wanaoana na kondoo zao.

Misingi ya utu inabomolewa na kanisa linabariki kwa kuwa wameendelea itakuwa serikali kubomoa nyumba kupisha highways? Fikiri.
You're a very grown up person. Unaleta ushabiki utadhani umebwiya kungu manga. Siongezi neno, hebu jirekebishe. Huwa unanikwaza ingawa nakuheshimu mkuu. What you commented on is a crap! U - CCM usikuache ukawa zumbukuku!
 
Nashauri na naona ni vema tukijikita ktk kujadili hoja badala ya kumu attack Mtu personally! Mshinde Mtu kwa hoja na siyo vinginevyo! Strong people discuss issues, weak people discuss .....
 
Jana nilipokuwa naangalia kwenye mitandao ya kijamii niliona picha mbali mbali za bomoabomoa ya nyumba inayoendelea Dar es salaam. Pamoja na huzuni, hasira, navilio vilivyokuwa vimetawala zoezi hilo, mimi kwa mtizamo wangu nimeona kwamba zoezi lenyewe litaziathiri sana taasisi za kifedha na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Kati ya nyumba zilizobomolewa miongoni mwake kuna nyumba ambazo ziliwekwa dhamana kwa mikopo pia kuna nyumba ambazo zilitumika kama ni anwani za wakopaji. Na kwenye maeneo hayo pia kuna nyumba zilizokuwa zinatumika kama nyumba za biashara zilizotathiminiwa kupata kigezo cha kukopeshwa.

Nyumba za aina hiyo zinapobomolewa zinaleta sintofahamu kubwa sana kwa taasisi za kifedha. Kwa mfano nyumba iliyowekwa dhamana na mkopaji imebomolewa na nyumba iliyotumika kama anwani ya mkopaji nayo imebolewa, na eneo ilikokuwa inafanyika biashara iliyokopeshwa nayo imebomolewa. Hapa taasisi ya kifedha iliyokopesha inawezaje kulipwa?

Halafu eneo lote linalobomolewa, serikali imewahi kujua ni biashara ya thamani kiasi gani ilikuwa inafanyika kwenye eneo hilo? Leo wote waliokuwa wanawazuia bidhaa wafanyabiashra wa eneo hilo wamepoteza wateja na waliokuwa wateja nao wamepoteza mitaji. Ni kwa kiasi gani biashara iliyopootezwa kwenye eneo hilo italeta athari kwenye uchumi wa Dar es salaam na Taifa kwa ujumla?

Wafanyakazi wa serikali ambao watakuwa wanashughulika na matokeo ya ubomoaji huo,ni kwa kiasi gani watashusha ufanisi wao kazini na pia wanawezaje kuhimili makato ya mikopo yao waliyokopa ili kuendeshea shughuli za kujiongezea kipato kwenye maeneo nyumba zilikobomolewa?
Kukubali dhamana ya jengo ambalo liko sehemu ambayo haina hati. Huko ni kuchukua risk kichwani mwako. Eneo lililopimwa na kumilikishwa kisheria, serikali hulipa fidia kabla ya kulitwaa. Kukaa kwenye eneo kienyeji enyeji ujue tu mda wowote lolote laweza kutokea ukaondoka bila kulipwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali la msingi kabisa. mimi tangu mwaka 1998 nafuatilia kupimiwa na kupewa hati ya kiwanja changu na mpaka leo sijafanikiwa. Lakini serikali yenyewe inayatambua maeneo yaliyopimwa na yasiyopimwa kisheria.

Hapo kinachobomolewa si ardhi ambayo haijapimwa bali yanabomolewa majengo ambayo yako kisheria na ndiyo maana kwenye maeneo yaliyobomolewa nyumba kuna serikali za mitaa!
Wana vibali vya kujenga hapo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom