Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,305
- 33,924
Jana tarehe 13/06/2023 Saa kumi jioni Mkuu wa MKoa wa Iringa anatoa Masaa 48 kwa wafanyabiashara wasio maeneo rasmi ya Biashara waondoke kwa hiyari yao ama wataondolewa kwa nguvu baada ya muda huo kupita.
Masaa 12 baadae (saa kumi usiku) vyombo vya dola vinaongoza bomoa bomoa eneo la Magari mabovu. Jee kauli ya Mkuu wa Mkoa kutoa masaa 48 ilibatilishwa na nani au nini kilitokea mpaka hayo masaa 48 kupungua mpaka kubaki 12?
Tarehe 02/06/2023 Meya wa Manispaa Iringa anamwagiza Kaimu Mkurugenzi kukaa na wafanyabiashara wa Magari Mabovu kuangalia jinsi watakavyoondoka eneo hilo. Siku nne baadae 06//06/2023 Manispaa inabomoa baadhi ya sehemu za kufanyia biashara. Kwa nini Meya aliagiza Mkurugenzi akae na wafanyabiashara wa Magari Mabovu halafu Ghafla Mkurugenzi anaamua eneo hilo libomolewe?
Tarehe 06/06/2023 Wafanyabiashara wanakwenda ofisi za CCM kulalamika kubomolewa eneo lao bila ya kufuatwa kwa utaratibu, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini anaigiza serikali yake isimamishe kwa muda zoezi la ubomoaji mpaka ijulikane wanaobomolewa wanakwenda wapi.
Siku tisa baadae serikali inavunja maeneo ya biashara ya wafanyabiashara walioahidiwa na CCM kwamba hayatavunjwa. CCM iliwatapeli wafanyabiashara wale huku ikijua kwamba serikali kumbe haiisikilizi CCM?
CCM inawezaje kujiita chama tawala kama haiwezi kuitawala serikali inayoongoza Iringa??