Bomba la Mnazi Bay mpaka Dar

Adili

JF-Expert Member
Nov 3, 2007
3,138
1,117
Hii ni sawa

Songo Songo mpaka Dar ni zaidi ya kilomita 200 – tuliruhusu wachimbie bomba la gasi badala ya kufua umeme Songo Songo na kuvuta waya mpaka dar (na kwingine). Anayetabasamu mpaka benki ni mkanada mwenye kandarasi ya kumaintain bomba na mitambo yake.

Sasa naambiwa Mnazi Bay mpaka Kinyerezi ni kilomita 550. Safari hii ni sisi wenyewe tunachimbia bomba. Gharama za bomba, uchimbaji, fidia ya linamopita, compressors za kusukuma gasi na maintanance zake na mengineyo.
Hivi vyote kweli inakuwa rahisi kuliko kuprocess gasi na kufua umeme hapo Mnazi Bay na kusambaza umeme kutokea hapo?
Je ingekuwa vibaya kusambaza viwanda na ajira mpaka huko kusini?
Nani anafaidika na hii shughuli ya kufikisha gasi Dar?
 
mambo yanafanywa kisiasa tuu, ilikuwa rahisi sana kujenga mtambo huko huko na kusambaza umeme. Mchina katoa mkopo wa miaka 50 na riba ndogo mno. huo mkopo unawanyima usingizi wazungu vibaya sana
 
Huu ni upuuzi wa viongozi wetu, wao kila kitu lazima kiwe Dar. Upuuzi mtupu
 
Wakuu heshima mbele

Naona kuna kitu mnamiss hapo, gesi inayoletwa Dar es Salaam sio kwa ajili ya umeme pekee! Umeme ni primary ila itatumika pia kwenye viwanda! Kuna mashine za viwandani za kisasa nyingi zinatumia gas!(LNG). Na nnadhani hata wale waCanada wa Songas wanfanya biashara hito tayari kuna viwanda vimeshaunganishwa kwahito tatitzo sio usafirishaji wa gesitatizo ni strategy zetu zilizojaza viwanda Dar es Salaam

.....Pamoja na hayo lakini nadhani katika mikoa itakayokuja kuwa na maendeleo makubwa ya kiviwanda ni hapo Lindi na Mtwara na hata investors wameshaliona hilo SIO kwasababu ya umeme ila kwasababu ya GESI inayotumika mojakwamoja bila kuhitaji kuibadilisha kwenda kwenye umeme!

.....Yule tajiri wa kiNigeria guru wa Cement anajenga kiwanda huko tayari
 
Mkuu Gobore,

Viwanda vichache vinavyotumia LNG vingeendelea kumtegemea Songo Songo. Viwanda vipya vyenye mahitaji ya LNG vielekezwe huko kusini. Hii ingekuwa ni usambaaji wa viwanda kuelekea maeneo ya Tanzania ambayo kwa kweli ni kama yalisaauliwa. Tanzania siyo Dar au pwani peke yake.
 
adilli

Kama ni mdau unayefuatilia haya maswala ya gesi nadhani utakua ushasikia kauli moja ya meneja mmoja kwenye vitalu pale rasi ya Songosongo, mpaka sasa hivi kuna visima vimeshachimbwa viko tayari ila watumiaji hakuna na naomba ukumbuke kuwa plan ya lile bomba la Songas haikua kuuza kwa private industries ilikua ni ya tanesco peke yake ila waliuza surplus tu na ile pipe imeshafikia maximum yake sasa hivi lakini viwanda vipo vingi vinapeleka maombi waonganishiwe kwasababu its much cheaper kuliko umeme

.....kwahiyo ilikua i lazima ifanyike namna hiyo gesi ivifwate viwanda lakini in long term plan viwanda watafuata gesi wenyewe kule kusini! Gesi ni nafuu mno huwezi amini
 
Last edited by a moderator:
Jamani angalieni na soko pia ata uyo dangote anajenga kiwanda cement almost yote anataka kuiexport
dsm viwanda ni vingi na viko karibu na soko
 
mambo yanafanywa kisiasa tuu, ilikuwa rahisi sana kujenga mtambo huko huko na kusambaza umeme. Mchina katoa mkopo wa miaka 50 na riba ndogo mno. huo mkopo unawanyima usingizi wazungu vibaya sana
Ni kweli wazungu hawawapendi Wachina mpaka basi!, ila pia hizi kampuni za China na hii benki ya Exim, sii bure iko namna!. Nakumbuka kisa cha Nundu na Mfutakamba!, wote walikwenda na maji!.
Mambo huwa kama hivi ifuatavyo
  1. Kampuni ya Kichina hufanya visibility study ya mradi!
  2. Kampuni hiyo huandaa proposal na gharama za mradi usually very high inflated rates!,
  3. Kampuni hiyo hutafuta mkopo wa riba nafuu toka kutoka Exim Bank ya China!, Ili riba iwe nafuu, repayment period huwekwa ndefu from 50 years on!.
  4. Serikali hutakiwa kutoa "government guarantee"!.
  5. Kampuni hiyo ya Kichina itafanya management ya mradi kwa kipindi chote cha hiyo miaka 50 mpaka deni likishalipwa lote ndipo Tanzania tutakabidhiwa mradi, by then life span ya mabomba na mitambo itakuwa almost end of its life span!.
  6. Tukishakabidhiwa mradi, then there will be a need to replace mabomba na old worn out machinery, hivyo China will bail us out kwa mkopo mwingine nafuu wa 50 years nyingine!.
  7. Kwa vile wachimbaji wote wa gesi ni makampuni ya wazungu, ili watuibie gesi yetu, kama msafirishaji wa gesi yote ni Mchina, na endapo serikali yetu itagoma kabisa kuruhusu mitambo ya baharini, then kuna uwezekano baadhi ya makapuni wezi wa kizungu, wakasusa kuendelea kutafuta gesi!.
 
Awali ya yote nitoe pongezi za dhati kwa wote mliotoa michango kabla yangu it is very constructive, Jambo hili nami lilikuwa linanisumbua sana ila kwa ufupi tunahitaji mtandao mkubwa zaidi wa bomba la gesi nchi nzima it is much more cheaper na ni moja ya competitive advantage ambazo zinaweza kutusaidia katika kuwa ni nchi yenye uchumi wa kati kama kweli tutaweza kuwe mikakati mizuri katika eneo hilo.

Sanjari na hilo Gas hii tulionayo kwasasa siyo processed kwa mantiki huwezi kuibeba katika mtungi kwa matumizi ya nyumbani kwavyo tunahitaji uwekezaji katika kiwanda cha kutengeneza Compressed Natural Gas (CNG) kwasasa tunatumia Liquefied Petroleum Gas (LPG) ambayo tuna-import nadhani hapo tabata ndipo wataweka kiwanda cha kutengeneza CNG, katika hilo swali na msingi je ni kwanini kiwanda hicho kisingewekwa kwenye source ya Gas, majibu bila shaka yanaweza kuwa mengi sana ila kwa mtazamo wangu nadhani issue ya Industry allocation is more than availability of raw materials. Kwavyo nadhani kuna mambo mengi ya msingi yamezingatiwa katika kufanya maamuzi husika.

Suala lingine ni Nishati viwandani. Mahitaji ya nishati katika maendeleo ya viwanda ni makubwa sana kwa mfano takribani kila kiwanda cha kuanzia saizi ya kati amabacho kinafanya processing kinahitaji kuwa na boiler kwaajiri ya prouduction ya steam, kwa sasa tunatumia mafuta machafu ambayo yanatoka ughaibuni sasa kama tukiingiza mifumo ya gesi katika hivyo viwanda ambavyo vimetapakaa dar,arusha, mbeya, mwanza nk tutashusha kwa asilimia kubwa gharama za uzalishaji na kwakweli tutajiweka vizuri sana katika soko la EAC.

Maeneo kama kigoma kuna opportunity kubwa sana mathalani material yote ya kutengenezea cement yapo, kuanzia gypsum na chokaa ambazo ndio main material sana tatizo ni moja tu nishati na hata kama mpango wa kuunganisha mkoa na grid ya taifa utafanikiwa katika miezi labda kumi na nane ijayo bado kigoma haitakuwa katika nafasi nzuri ya kutumia material husika ila endapo mtandaoo huu wa gesi ukapanuliwa sambamba na uboreshaji wa reli ya kati kwakweli itakuwa ni maendeleo makubwa sana. Na ikumbukwe kigoma ipo very strategically positioned kuweza kuwa ni mzalishaji wa ukanda wa maziwa makuu.

Kwavyo nadhani nguvu zetu tuzipeleke kuiomba serikali kuangalia uwezekanao wa kuboresha reli ya kati ambapo katika uboreshaji huo uambatane na ufungaji wa bomba la gesi Dar -Tabora - Kigoma - Mwanza na mikoa yote ya kati itanufaika. Kama tukifika huko natabiri the Quantum jump of Tanzania to the middle earners country.
 
Huwa najiuliza sana maswali haya? What has Magufuli, Mwakyembe, Tibaijuka done in other regions that worth recognition? The answer is NOTHING!! Wote ni mawaziri wa Dar!!
 
Hii ni sawa

Songo Songo mpaka Dar ni zaidi ya kilomita 200 – tuliruhusu wachimbie bomba la gasi badala ya kufua umeme Songo Songo na kuvuta waya mpaka dar (na kwingine). Anayetabasamu mpaka benki ni mkanada mwenye kandarasi ya kumaintain bomba na mitambo yake.

Sasa naambiwa Mnazi Bay mpaka Kinyerezi ni kilomita 550. Safari hii ni sisi wenyewe tunachimbia bomba. Gharama za bomba, uchimbaji, fidia ya linamopita, compressors za kusukuma gasi na maintanance zake na mengineyo.
Hivi vyote kweli inakuwa rahisi kuliko kuprocess gasi na kufua umeme hapo Mnazi Bay na kusambaza umeme kutokea hapo?
Je ingekuwa vibaya kusambaza viwanda na ajira mpaka huko kusini?
Nani anafaidika na hii shughuli ya kufikisha gasi Dar?

Mkuu ur concern is understood, lakini somehow uko wrong kihandisi
1. Umeme huwa hausafirishwi kwa kuunganisha nyaya tu. For such along distance lazima kunakuwa na voltage drop as such utahitaji (transformers)substations in between kwa ajili ya kustep up hiyo voltage drop. Hizo substations zitahitaji maintenance na sometimes usimamizi wa moja kwa moja. Ni gharama kama hizo zikilinganishwa na kuweka bomba ambalo ni almost maintenance free, relatively involving less skilled labor zinapelekea kuukubali mfumo wa bomba kuliko kutandaza nyaya.

2. Gas huwa haisukumwi na compressors, the same pressure inayotoka nayo huko ardhi inatumika kuisafirishia, sana sana kunakuwa na regulators mfano valves of different designs.

3. Maintenance katika kusafirisha gesi kwa mabomba is considered a low level in terms of cost na. frequency.

Hivyo basi kwa matumizi ya umeme huko huko kusini yes umemeutazalishiwa huko huko lakini kupeleka distance kama hiyo it's cheaper and ecoomical kutumia mabomba. Nchi nyinine gesi husairishwa hadi 1000 km. Pia kama walivyosema wajumbe wengine matumizi ya hiyo gesi simkuzalisha umeme tu.
 
the issue here is, why Dar?
 
Ikifika Dar es salaam nini kinafuatia?Kama itasafirishwa mikoani kama umeme nafikiri changamoto ya kihandisi uliyoisema itabaki palepale.
 
Ni kweli wazungu hawawapendi Wachina mpaka basi!, ila pia hizi kampuni za China na hii benki ya Exim, sii bure iko namna!. Nakumbuka kisa cha Nundu na Mfutakamba!, wote walikwenda na maji!.
Mambo huwa kama hivi ifuatavyo
  1. Kampuni ya Kichina hufanya visibility study ya mradi!
  2. Kampuni hiyo huandaa proposal na gharama za mradi usually very high inflated rates!,
  3. Kampuni hiyo hutafuta mkopo wa riba nafuu toka kutoka Exim Bank ya China!, Ili riba iwe nafuu, repayment period huwekwa ndefu from 50 years on!.
  4. Serikali hutakiwa kutoa "government guarantee"!.
  5. Kampuni hiyo ya Kichina itafanya management ya mradi kwa kipindi chote cha hiyo miaka 50 mpaka deni likishalipwa lote ndipo Tanzania tutakabidhiwa mradi, by then life span ya mabomba na mitambo itakuwa almost end of its life span!.
  6. Tukishakabidhiwa mradi, then there will be a need to replace mabomba na old worn out machinery, hivyo China will bail us out kwa mkopo mwingine nafuu wa 50 years nyingine!.
  7. Kwa vile wachimbaji wote wa gesi ni makampuni ya wazungu, ili watuibie gesi yetu, kama msafirishaji wa gesi yote ni Mchina, na endapo serikali yetu itagoma kabisa kuruhusu mitambo ya baharini, then kuna uwezekano baadhi ya makapuni wezi wa kizungu, wakasusa kuendelea kutafuta gesi!.

Si lazima kuchangia kitu usichokijua mkuu , acha kabisa kupotosha
 
Ungeuliza kwanza gharama za kuleta gas hadi DAR ni kiasi gani, na gharama za kuzalisha umeme Mnazi Bay na kujenga miundo mbinu ya kuuleta huo umeme ni kiasi gani. Baada ya kupata hizo gharama, ndio ungeanza kuhoji ni kwa nini uamuzi umefanywa. Tusiwe na mazoea ya kuanza tu kuponda vitu au maamuzi bila kufanya utafiti. Huna haja ya kuwa mtaalamu ufanye hizo hesabu mwenyewe. Uliza kwa watu wenye kujua hizi hesabu ndio wakueleze. Watu wengi tunayo mazoea ya kukurupuka na kuzungumza kwa jazba kwenye maswala ambayo tuko mbumbumbu
 
Wakuu heshima mbele

Naona kuna kitu mnamiss hapo, gesi inayoletwa Dar es Salaam sio kwa ajili ya umeme pekee! Umeme ni primary ila itatumika pia kwenye viwanda! Kuna mashine za viwandani za kisasa nyingi zinatumia gas!(LNG). Na nnadhani hata wale waCanada wa Songas wanfanya biashara hito tayari kuna viwanda vimeshaunganishwa kwahito tatitzo sio usafirishaji wa gesitatizo ni strategy zetu zilizojaza viwanda Dar es Salaam

.....Pamoja na hayo lakini nadhani katika mikoa itakayokuja kuwa na maendeleo makubwa ya kiviwanda ni hapo Lindi na Mtwara na hata investors wameshaliona hilo SIO kwasababu ya umeme ila kwasababu ya GESI inayotumika mojakwamoja bila kuhitaji kuibadilisha kwenda kwenye umeme!

.....Yule tajiri wa kiNigeria guru wa Cement anajenga kiwanda huko tayari

kwa hadi mnaijeria na yeye kisha megewa pande lake kazi ipo bongo..

RIP my country tz..
 
Hii ni sawa

Songo Songo mpaka Dar ni zaidi ya kilomita 200 – tuliruhusu wachimbie bomba la gasi badala ya kufua umeme Songo Songo na kuvuta waya mpaka dar (na kwingine). Anayetabasamu mpaka benki ni mkanada mwenye kandarasi ya kumaintain bomba na mitambo yake.

Sasa naambiwa Mnazi Bay mpaka Kinyerezi ni kilomita 550. Safari hii ni sisi wenyewe tunachimbia bomba. Gharama za bomba, uchimbaji, fidia ya linamopita, compressors za kusukuma gasi na maintanance zake na mengineyo.
Hivi vyote kweli inakuwa rahisi kuliko kuprocess gasi na kufua umeme hapo Mnazi Bay na kusambaza umeme kutokea hapo?
Je ingekuwa vibaya kusambaza viwanda na ajira mpaka huko kusini?
Nani anafaidika na hii shughuli ya kufikisha gasi Dar?

Mkuu nadhani phase II, hilo bomba litafika Bagamoyo-Msata, na Kama Lowassa akichukua nchi basi litapinda kona na Phase III litaenda Monduli
 
Hii ni sawa

Songo Songo mpaka Dar ni zaidi ya kilomita 200 – tuliruhusu wachimbie bomba la gasi badala ya kufua umeme Songo Songo na kuvuta waya mpaka dar (na kwingine). Anayetabasamu mpaka benki ni mkanada mwenye kandarasi ya kumaintain bomba na mitambo yake.

Sasa naambiwa Mnazi Bay mpaka Kinyerezi ni kilomita 550. Safari hii ni sisi wenyewe tunachimbia bomba. Gharama za bomba, uchimbaji, fidia ya linamopita, compressors za kusukuma gasi na maintanance zake na mengineyo.
Hivi vyote kweli inakuwa rahisi kuliko kuprocess gasi na kufua umeme hapo Mnazi Bay na kusambaza umeme kutokea hapo?
Je ingekuwa vibaya kusambaza viwanda na ajira mpaka huko kusini?
Nani anafaidika na hii shughuli ya kufikisha gasi Dar?
Kama gas hiyo ni kwa ajili ya kuzalisha umeme tu ingefaa mitambo hiyo ikawekwa hukohuko inapozalishiwa ila kama ni kwa ajili ya matumizi ya viwanda na majumbani acha mradi uendelee kwani una manufaa zaidi.
 
Back
Top Bottom