Bomba la Mnazi Bay mpaka Dar

Bomba la Mnazi Bay mpaka Dar

Matumizi ya GAs sio umeme tu. So si dhani kama kitu unacho kisema kiko sawa. Halafu ujue kuwa Dar ni mji wa kibiashara Tanzania kwa sasa.
 
kama gas hiyo ni kwa ajili ya kuzalisha umeme tu ingefaa mitambo hiyo ikawekwa hukohuko inapozalishiwa ila kama ni kwa ajili ya matumizi ya viwanda na majumbani acha mradi uendelee kwani una manufaa zaidi.

mi swali langu watu wa kusini tutafaidika vipi na huu mradi?
Maana hiyo songosongo hatuoni faida yake zaidi ya kusifiwa tu
 
mi swali langu watu wa kusini tutafaidika vipi na huu mradi?
Maana hiyo songosongo hatuoni faida yake zaidi ya kusifiwa tu
Nadhani ni wakati wa serikali sasa kuhimiza viwanda vipya kujengwa kusini sehemu ambapo gas inapatikana na si kulazimisha kujengwa ndani ya jiji hili tena.na ingefaa sasa tuone kuna mchakato wa kujenga miundo mbinu muhimu ili iwe rahisi kwa wawekazejaji kuja kuwekeza huko!
 
Si lazima kuchangia kitu usichokijua mkuu , acha kabisa kupotosha
Mkuu Makupa, with due respect, kwenye mchango wangu huu

"Ni kweli wazungu hawawapendi Wachina mpaka basi!, ila pia hizi kampuni za China na hii benki ya Exim, sii bure iko namna!. Nakumbuka kisa cha Nundu na Mfutakamba!, wote walikwenda na maji!.
Mambo huwa kama hivi ifuatavyo

  • Kampuni ya Kichina hufanya visibility study ya mradi!
  • Kampuni hiyo huandaa proposal na gharama za mradi usually very high inflated rates!,
  • Kampuni hiyo hutafuta mkopo wa riba nafuu toka kutoka Exim Bank ya China!, Ili riba iwe nafuu, repayment period huwekwa ndefu from 50 years on!.
  • Serikali hutakiwa kutoa "government guarantee"!.
  • Kampuni hiyo ya Kichina itafanya management ya mradi kwa kipindi chote cha hiyo miaka 50 mpaka deni likishalipwa lote ndipo Tanzania tutakabidhiwa mradi, by then life span ya mabomba na mitambo itakuwa almost end of its life span!.
  • Tukishakabidhiwa mradi, then there will be a need to replace mabomba na old worn out machinery, hivyo China will bail us out kwa mkopo mwingine nafuu wa 50 years nyingine!.
  • Kwa vile wachimbaji wote wa gesi ni makampuni ya wazungu, ili watuibie gesi yetu, kama msafirishaji wa gesi yote ni Mchina, na endapo serikali yetu itagoma kabisa kuruhusu mitambo ya baharini, then kuna uwezekano baadhi ya makapuni wezi wa kizungu, wakasusa kuendelea kutafuta gesi!."
Nilianza hoja yangu kwa mfano hai wa waliokwenda na maji kwa deals hizi hizi za kampuni za kichina na benki ni hii hii ya Exim Bank!. Nikatoa mchakato na mlolongo wa games people play kwenye hiki kiini macho cha mikopo inayoitwa ya riba nafuu!. Hoja zangu niliziweka in points format, hivyo kama kuna kitu nisichokijua na ime happen wewe unakijua, basi unakisema ili watu wakijue!.

Kwa kukusaidia tuu, naomba tembelea ule uzi huu NYARAKA: Omar Nundu ni msafi. wa kilichoimkuta kwanza Omar Nundu na Naibu wake Mfutakamba!, then Ephraim Mgawe na mwisho Bodi Nzima ya Bandari!. The Chinese are the same people, the same company, the same bank, the same tricks and the same games they play on us!.

Mkuu Mkandara, asante kwa kulisemea hili!.
1. Gharama za kwanza za CCCC zilikuwa dola milioni 600 plus wajenge hizo gati mbili na kukarabati gati zingine zote kwa mchanganuo wa dola milioni 400 gati mpya na dola milioni 200 ukarabati!.

2. TPA wakawaambia waachane na ukarabati hivyo CCCC wakaleta makadirio mengine ya dola milioni 400 kujenga hizo gati 2.

3. Baada ya TPA kupata hayo makadirio wao TPA wakaandika barua wizarani kuwa wanataka udhamini wa serikali kuomba mkopo wa dola milioni 500!. Ina maana wao wameshaweka cha juu cha dola milioni 100!. Tena kimekuwa inserted kwa peni!.

4. Waziri Mkulo nae baada ya kupokea barua ya TPA serikali sasa ndio ikaiandikia barua Exim Bank ya China kuomba mkopo wa Dola milioni 527 ikiwa na cha juu zaidi cha dola milioni 27 za "wakubwa"!.

5. Ukisoma dokezo lenye dola milioni 600, 527 na 400 maneno mengine yote ni yale neno kwa neno!. Haiwezekani kuwepo kwa flactuations kubwa hivyo ya figures in terms of millions of dollars bila any explanations!.

6.Ukisikia high level corruption ndio hii!. Mijitu mijizi inataka kuwaibia Watanzania, Nundu ameishtukia dili sasa ndio anapigwa vita kuzuia ulaji!.

7. Wajameni hapo kuna MOU tuu, bado hakuna mkataba wowote!. Hakuna mkopo wowote! na hakuna ujenzi wowote!. Hizi zote ni harakati za kundi la mijizi ndidi ya harakati za wazalendo kuinusuru nchi!.

Pasco.
 
Hii ni sawa

Songo Songo mpaka Dar ni zaidi ya kilomita 200 – tuliruhusu wachimbie bomba la gasi badala ya kufua umeme Songo Songo na kuvuta waya mpaka dar (na kwingine). Anayetabasamu mpaka benki ni mkanada mwenye kandarasi ya kumaintain bomba na mitambo yake.

Sasa naambiwa Mnazi Bay mpaka Kinyerezi ni kilomita 550. Safari hii ni sisi wenyewe tunachimbia bomba. Gharama za bomba, uchimbaji, fidia ya linamopita, compressors za kusukuma gasi na maintanance zake na mengineyo.
Hivi vyote kweli inakuwa rahisi kuliko kuprocess gasi na kufua umeme hapo Mnazi Bay na kusambaza umeme kutokea hapo?
Je ingekuwa vibaya kusambaza viwanda na ajira mpaka huko kusini?
Nani anafaidika na hii shughuli ya kufikisha gasi Dar?
Pole sana kwa ujuha wako kuhusu gesi. Matumizi ya gesi si kuzalisha Umeme tu. ingia google utaelimika sana kuhusu matumizi Mengi ya gesi badala ya mtu mzima kufuata, kutafuta na kupata aibu hapa JF. kukusaidia, na leo ndo mwisho kukusaidia uwe unafanya uchunguzi wa kina Kabla hujatoa mada Ni kuwa hapa Dar baadhi ya Viwanda vinatumia gesi asili. Fuatilia pia Hansard za Bunge Kwenye tovuti ya Bunge maana nakumbuka siku moja kusikia idadi ya Viwanda hivyo ink itakuwa.
 
Ungeuliza kwanza gharama za kuleta gas hadi DAR ni kiasi gani, na gharama za kuzalisha umeme Mnazi Bay na kujenga miundo mbinu ya kuuleta huo umeme ni kiasi gani. Baada ya kupata hizo gharama, ndio ungeanza kuhoji ni kwa nini uamuzi umefanywa. Tusiwe na mazoea ya kuanza tu kuponda vitu au maamuzi bila kufanya utafiti. Huna haja ya kuwa mtaalamu ufanye hizo hesabu mwenyewe. Uliza kwa watu wenye kujua hizi hesabu ndio wakueleze. Watu wengi tunayo mazoea ya kukurupuka na kuzungumza kwa jazba kwenye maswala ambayo tuko mbumbumbu

ni zipi sasa? Si tunalaumu kila kitu kuwa Dar? Why?
 
Yale yale ya kiwanda cha sigara kuwa Dar! Cha nguo Dar! Raw materials Tabora and Lake zone? Why not Lake zone?
 
Just imagine, mipuuzi inawaza kuweka flyovers na BRT kwa mabilioni ya pesa bila kujali sehemu zingine nchi hii maji km 20
 
Ungeuliza kwanza gharama za kuleta gas hadi DAR ni kiasi gani, na gharama za kuzalisha umeme Mnazi Bay na kujenga miundo mbinu ya kuuleta huo umeme ni kiasi gani. Baada ya kupata hizo gharama, ndio ungeanza kuhoji ni kwa nini uamuzi umefanywa. Tusiwe na mazoea ya kuanza tu kuponda vitu au maamuzi bila kufanya utafiti. Huna haja ya kuwa mtaalamu ufanye hizo hesabu mwenyewe. Uliza kwa watu wenye kujua hizi hesabu ndio wakueleze. Watu wengi tunayo mazoea ya kukurupuka na kuzungumza kwa jazba kwenye maswala ambayo tuko mbumbumbu
Kisamo nakuunga mkono ,hapa jamii forum imevamiwa na kundi la watu wanaojifanya kuwa wao ni mabingwa wa kila ,ili uonekane wa maana hapa jf ni lazima uwe bigwa wa uongo
 
Wakuu heshima mbele

Naona kuna kitu mnamiss hapo, gesi inayoletwa Dar es Salaam sio kwa ajili ya umeme pekee! Umeme ni primary ila itatumika pia kwenye viwanda! Kuna mashine za viwandani za kisasa nyingi zinatumia gas!(LNG). Na nnadhani hata wale waCanada wa Songas wanfanya biashara hito tayari kuna viwanda vimeshaunganishwa kwahito tatitzo sio usafirishaji wa gesitatizo ni strategy zetu zilizojaza viwanda Dar es Salaam

.....Pamoja na hayo lakini nadhani katika mikoa itakayokuja kuwa na maendeleo makubwa ya kiviwanda ni hapo Lindi na Mtwara na hata investors wameshaliona hilo SIO kwasababu ya umeme ila kwasababu ya GESI inayotumika mojakwamoja bila kuhitaji kuibadilisha kwenda kwenye umeme!

.....Yule tajiri wa kiNigeria guru wa Cement anajenga kiwanda huko tayari

kiwanda gan!?
 
mkuu kwani hii gas ni LNG??sio NG tu??

sio anesco,bomba la awali lilikuwa kwa ajili ya twiga cement na songas ndugu
adilli

Kama ni mdau unayefuatilia haya maswala ya gesi nadhani utakua ushasikia kauli moja ya meneja mmoja kwenye vitalu pale rasi ya Songosongo, mpaka sasa hivi kuna visima vimeshachimbwa viko tayari ila watumiaji hakuna na naomba ukumbuke kuwa plan ya lile bomba la Songas haikua kuuza kwa private industries ilikua ni ya tanesco peke yake ila waliuza surplus tu na ile pipe imeshafikia maximum yake sasa hivi lakini viwanda vipo vingi vinapeleka maombi waonganishiwe kwasababu its much cheaper kuliko umeme

.....kwahiyo ilikua i lazima ifanyike namna hiyo gesi ivifwate viwanda lakini in long term plan viwanda watafuata gesi wenyewe kule kusini! Gesi ni nafuu mno huwezi amini
 
hatujaanza kuzalisha LNG tanzania
Mkuu Gobore,

Viwanda vichache vinavyotumia LNG vingeendelea kumtegemea Songo Songo. Viwanda vipya vyenye mahitaji ya LNG vielekezwe huko kusini. Hii ingekuwa ni usambaaji wa viwanda kuelekea maeneo ya Tanzania ambayo kwa kweli ni kama yalisaauliwa. Tanzania siyo Dar au pwani peke yake.
 
mi swali langu watu wa kusini tutafaidika vipi na huu mradi?
Maana hiyo songosongo hatuoni faida yake zaidi ya kusifiwa tu
kama mna vingozi wapumbavu na bado mnawachagua tu, basi faida yenu ni sifa tu inatosha, kwani kama mtambo ungekuwa mtwara gesi na umeme ukifika dar na sehemu zote ulikopita mradi ni stahili yao, na sasa inanyesha watu walio na sifa ya kutumia umeme na gesi ni wa dar baada ya hapo kusini itafikiriwa, kama unabisha nenda shinyanga wana sifa kweli ya kutoa almasi lakini wenyewe wanapata madhara yatokanayo na kemikali
 
Pole sana kwa ujuha wako kuhusu gesi. Matumizi ya gesi si kuzalisha Umeme tu. ingia google utaelimika sana kuhusu matumizi Mengi ya gesi badala ya mtu mzima kufuata, kutafuta na kupata aibu hapa JF. kukusaidia, na leo ndo mwisho kukusaidia uwe unafanya uchunguzi wa kina Kabla hujatoa mada Ni kuwa hapa Dar baadhi ya Viwanda vinatumia gesi asili. Fuatilia pia Hansard za Bunge Kwenye tovuti ya Bunge maana nakumbuka siku moja kusikia idadi ya Viwanda hivyo ink itakuwa.

Nadhani ni busara zaidi kumuelimisha kuliko kumkashifu JF hatuendi hivyo hii ni sehemu ya kuelimishana,kubadilishana mawazo na kupashana habari sio vizuri kupeana kashfa
 
kiwanda gan!?

Sijui ulikua unamanisha kiwanda gani kipi?

Kama unaulizia kiwanda Mtwara ni Dangote Cement

Kama unaulizia kiwanda kinachotumia gesi Dar basi ni viwanda zaidi ya 30 so far na sio kiwanda, kwa uchache tu ni

Twiga Cement,ALAF,TBL,Serengeti Breweries......
 
mkuu kwani hii gas ni LNG??sio NG tu??

Natural gas(Hiyo unayoiita NG) kuna process inapitia inabadilishwa kwenda either LNG or CNG

Samahani hapo nimechanganya kwa bongo wanasupply CNG(Compressed Natural Gas) sio LNG
 
sio anesco,bomba la awali lilikuwa kwa ajili ya twiga cement na songas ndugu

Acha kuchanganya madesa mkuu!! Tanesco alikua mdau mkuu kwenye Songas from verry begining!

Kwa kukusaidia tu ujue ni kwamba anayewauzia gesi Twiga cement sio songas ni Pan Africa ltd embu kajaribu kusoma tena huo uhusiano wa kibiashara kati ya TPDC, Songas, Tanesco, Pan Africa LTD, Globeleq na wale waholanzi kwenye kuanzia exploration ndo utaelewa nini ninakisema! Tanesco ni shareholder wa Songas ila Twiga cement anauziwa tu.
 
Back
Top Bottom