Bomba la Mnazi Bay mpaka Dar

Bomba la Mnazi Bay mpaka Dar

Huu uzi umejaa maGt watupu hamna utumbo hapa,ila ndugu zangu kwa utawala huu wa ccm hata mvumbue cash aridhini bado tutaendelea kuwa masikini tu.mkopo miaka 50 menegment mchina!
 
Huwa najiuliza sana maswali haya? What has Magufuli, Mwakyembe, Tibaijuka done in other regions that worth recognition? The answer is NOTHING!! Wote ni mawaziri wa Dar!!

It takes more than 5 years to see real results. Also, how do you know nothing has or is being done outside Dar?
Na wewe ukute ni mkazi wa Dar tu 🙂
 
Huu ni upuuzi wa viongozi wetu, wao kila kitu lazima kiwe Dar. Upuuzi mtupu

tuombe tuendelee kuwa na hii amani, ikitokea vita tumeisha, Ukipiga ubungo tu nchi yote giza....., na system pamoja na uongozi wote upo centralizes Dar
 
Yale yale ya kiwanda cha sigara kuwa Dar! Cha nguo Dar! Raw materials Tabora and Lake zone? Why not Lake zone?[/Q

Na market kubwa ipo wapi?

kiwanda kingekuwa Tabora ni virahisi kupeleka bidhaa kila kona. Lake zone ina watu zaidi ya mil. 15
 
tuombe tuendelee kuwa na hii amani, ikitokea vita tumeisha, Ukipiga ubungo tu nchi yote giza....., na system pamoja na uongozi wote upo centralizes Dar

kweli mkuu! Mi linanikera saana hili jambo. Na walaaniwe wote wanaofikiri kila kitu lazima kiwe Dar!
 
Kwa nini hospitali ya taifa iliwekwa Dar? Kwa nini isiwe katikati ya nchi? Why? Why? Why? It pains me a lot
 
Mkuu nnacho kijua ni kwamba hio gesi itatumika kwa matumizi mengi kama majumbani, viwandani n.k pamoja na hilo la umeme ambalo ndio kipaumbele ndo mana gesi inaletwa Dar badala ya kufua umeme uko uko
 
Mkuu nnacho kijua ni kwamba hio gesi itatumika kwa matumizi mengi kama majumbani, viwandani n.k pamoja na hilo la umeme ambalo ndio kipaumbele ndo mana gesi inaletwa Dar badala ya kufua umeme uko uko

najua ndo kinachofuata kama kiini macho kwa wapiga kura!.....kusambaza gesi majumbani! Take my words "this will never be succesful in tanzania" na hii ni kutokana na miundo mbinu, hatuna plan ya over 50 years!....hizo bomba zitapita wapi mjini kila mwaka upanuzi wa barabara...... Andaeni zima moto za kutosha
 
Ni kweli wazungu hawawapendi Wachina mpaka basi!, ila pia hizi kampuni za China na hii benki ya Exim, sii bure iko namna!. Nakumbuka kisa cha Nundu na Mfutakamba!, wote walikwenda na maji!.
Mambo huwa kama hivi ifuatavyo
  1. Kampuni ya Kichina hufanya visibility study ya mradi!
  2. Kampuni hiyo huandaa proposal na gharama za mradi usually very high inflated rates!,
  3. Kampuni hiyo hutafuta mkopo wa riba nafuu toka kutoka Exim Bank ya China!, Ili riba iwe nafuu, repayment period huwekwa ndefu from 50 years on!.
  4. Serikali hutakiwa kutoa "government guarantee"!.
  5. Kampuni hiyo ya Kichina itafanya management ya mradi kwa kipindi chote cha hiyo miaka 50 mpaka deni likishalipwa lote ndipo Tanzania tutakabidhiwa mradi, by then life span ya mabomba na mitambo itakuwa almost end of its life span!.
  6. Tukishakabidhiwa mradi, then there will be a need to replace mabomba na old worn out machinery, hivyo China will bail us out kwa mkopo mwingine nafuu wa 50 years nyingine!.
  7. Kwa vile wachimbaji wote wa gesi ni makampuni ya wazungu, ili watuibie gesi yetu, kama msafirishaji wa gesi yote ni Mchina, na endapo serikali yetu itagoma kabisa kuruhusu mitambo ya baharini, then kuna uwezekano baadhi ya makapuni wezi wa kizungu, wakasusa kuendelea kutafuta gesi!.

Mkuu PASCO kama Wachina wangekuwa ni watu wanao zungumza with a forked tongue basi hilo lingeonekana kwenye project za Ujenzi wa TAZARA, Urafiki textile, UFI, Mzinga Corp, Mang'ula, Concrete plant Mbeya, Upanuzi wa Twiga Cement, Ujenzi wa Ukumbi wa Bunge, Ujenzi wa Ukumbi wa Jego la AU pale Adis, Mabarabara, Mchuchumaa/Liganga project etc.

Wenzetu Kenya siku hizi wako karibu sana na Wachina na wanawatumia kikamilifu kuendeleza TAIFA lao, muda si mrefu Kenya itapiga hatua kubwa sana ya maendeleo, Wakenya wanaona mbali SANA. Nenda Angola utashuhudia maajabu ya Wachina - just to mention a few!

Mkuu tuwe wakweli we're better off tukishilikiana na na Wachina kuliko Mataifa mengine specifically nchi za magharibi, Wachina hawa ingilii internal affairs za nchi zinazopewa misaada na wao - wanatoa misaada bila ya ku-attach strings zozote.
 
ninacho kishangaa ni kwamba iyo gass itakuja mpaka dar alafu nguzo zitawekwa kupeleka umeme mnazi bay huu ni ujinga
 
Huwa najiuliza sana maswali haya? What has Magufuli, Mwakyembe, Tibaijuka done in other regions that worth recognition? The answer is NOTHING!! Wote ni mawaziri wa Dar!!

Bora ungeandika Kiswahili tu What has Magufuli, Mwakyembe, Tibaijuka done
 
Mkuu PASCO kama Wachina wangekuwa ni watu wanao zungumza with a forked tongue basi hilo lingeonekana kwenye project za Ujenzi wa TAZARA, Urafiki textile, UFI, Mzinga Corp, Mang'ula, Concrete plant Mbeya, Upanuzi wa Twiga Cement, Ujenzi wa Ukumbi wa Bunge, Ujenzi wa Ukumbi wa Jego la AU pale Adis, Mabarabara, Mchuchumaa/Liganga project etc.

Wenzetu Kenya siku hizi wako karibu sana na Wachina na wanawatumia kikamilifu kuendeleza TAIFA lao, muda si mrefu Kenya itapiga hatua kubwa sana ya maendeleo, Wakenya wanaona mbali SANA. Nenda Angola utashuhudia maajabu ya Wachina - just to mention a few!

Mkuu tuwe wakweli we're better off tukishilikiana na na Wachina kuliko Mataifa mengine specifically nchi za magharibi, Wachina hawa ingilii internal affairs za nchi zinazopewa misaada na wao - wanatoa misaada bila ya ku-attach strings zozote.
Mkuu Bukya, Wachina wa enzi za Chairman Mao sio hawa wa leo!. Fuatilia kisa cha deal ya upanuzi wa Bandari!.
  1. Aliyefanya upembuzi yakinifu ni kampuni ya CCCC na akaja na set tatu za gharama milioni 400, 500 na 600!, Waziri Nundu akaangalia upanuzi wa Bandari ya nchi nyine fulani ambao ni mkubwa kuliko huu wetu umegharimu dola milioni 200 tuu!, hii inamaanisha hawa Wachina wanajenga kwa highly imflated rates!.
  2. Ki kawaida anayefanya upembuzi yakinifu huwa mtu mwingine, na mshauri mwelekezi huwa mwingine na mjenzi huwa mwingine na mwendeshaji wa mradi huwa mwingine!. Kwenye deal ile Uchambuzi yakinifu ni CCCC, Mshauri mwelekezi ni CCCC, mjenzi ni CCCC na mwendeshaji ni yeye CCCC!.
  3. Zaidi ya yote, aliyekutafutiua mkopo kutoka Exim Bank ya Uchina ni CCCC, ili kupata mkopo ni lazima upate government guarantee!. Anayetakiwa kuiomba hiyo government guarantee ni Waziri husika. Kwenye issue hii baada ya waziri kushtukia deal akasita, CCCC wakamtumia naibu waziri, wa m by pass waziri, government guarantee ikapatikana "chap chap"!.
  4. Kupata government guarantee ili kupata mkopo wa kimataifa its not a joke!, Tido tangu ameingia TBC mpaka ametoka, amekuwa akiisubiri government guarantee ili kukamilishe lile jengo pale TBC mpaka ameondoka, haujatoka nadhani mpaka leo lile jengo pale bado limesimama kama gofu!, lakini mradi wa bandari guarantee imeommbwa leo, kesho imepatikana!.
  5. Hii bank ya Exim ina charge very low interest ya ajabu!,unaambiwa riba ni asilimia 02.0% kwa mwaka. Hii ni fixed interest na sio compound!. Wanakupa muda mtefu sana wa kuilipa lets say miaka 50!, tena watakupa na grace period fulani ya miaka miwili mitatu ya kutolipa mpaka mradi uanze operation. Hebu piga hiyo 2% interest kwa mwaka mara miaka 50!, utajikuta umelipa 100% interest!.

Kitu ambacho nakubali, wawekezaji wote ni waizi, ila afadhani waizi Wachina, wanatuibia kidogo tuu kwa sababu
gesi itakuwa yetu kuliko waizi wazungu, wangetuibia mpaka hiyo gesi yenyewe!.

P.
 
Hii ni sawa

Songo Songo mpaka Dar ni zaidi ya kilomita 200 – tuliruhusu wachimbie bomba la gasi badala ya kufua umeme Songo Songo na kuvuta waya mpaka dar (na kwingine). Anayetabasamu mpaka benki ni mkanada mwenye kandarasi ya kumaintain bomba na mitambo yake.
Sasa naambiwa Mnazi Bay mpaka Kinyerezi ni kilomita 550. Safari hii ni sisi wenyewe tunachimbia bomba. Gharama za bomba, uchimbaji, fidia ya linamopita, compressors za kusukuma gasi na maintanance zake na mengineyo.
Hivi vyote kweli inakuwa rahisi kuliko kuprocess gasi na kufua umeme hapo Mnazi Bay na kusambaza umeme kutokea hapo?
Je ingekuwa vibaya kusambaza viwanda na ajira mpaka huko kusini?
Nani anafaidika na hii shughuli ya kufikisha gasi Dar?

Adili
Kuna bidhaa zinatengenezwa pale pale malighafi inapopatikana na nyingine kwenye wanunuzi. Mfano gesi, ni rahisi kusafirisha gesi kwenda kwa watumiaji nikiwa na maana viwanda na kuzalisha umeme kuliko kuzalisha Mtwara. Ni sawa na kutengeneza fenicha inapopatikana miti badala ya kusafirisha magogo kwenda karibu walipo wanunuzi. Lakini huwezi kusafirisha muwa kutoka shambani kuleta mjini kuzalisha sukari! Ukifahamu kanuni hii ya uchumi utaelewa kwanini kuna bomba la gesi kutoka Siberia hadi Ulaya Magharibi.
 
kweli mkuu! Mi linanikera saana hili jambo. Na walaaniwe wote wanaofikiri kila kitu lazima kiwe Dar!
........

Unashangaa hayo tu mkuu,hata kuoa,watu wanaoa Dar,mtu kwao Namtumbo na kakulia huko,lakini mke anatafuta hapo hapo Dar.

H
arusi anafungia Dar na ndugu kama 6 au 7 anawasafirisha kutoka Namtumbo kuja Dar kwenye harusi,badala ya wao wawili tu kusafiri kwenda kufunga harusi huko Namtumbo.

M
wingine yuko mikoani huko anafanya kazi,anapata mchumba hukohuko countyside,ila kwa sababu alishawahi kuishi Dar kidogo na anandugundugu tena wengine ni wakuunga unga anataka au anakuja kufunga harusi Dar au kufanyia send of Dar.

H
uku akisafirisha ndugu zake kutoka mkoa mwingine tofauti na anakoishi kuja Dar , we acha tu,kuna watu wameikariri Dar hata uwape kazi ya maana mkoani hawaendi kisa Dar, duuuh,Dar kuna nini wajameni?
 
Hii ni sawa

Songo Songo mpaka Dar ni zaidi ya kilomita 200 – tuliruhusu wachimbie bomba la gasi badala ya kufua umeme Songo Songo na kuvuta waya mpaka dar (na kwingine). Anayetabasamu mpaka benki ni mkanada mwenye kandarasi ya kumaintain bomba na mitambo yake.

Sasa naambiwa Mnazi Bay mpaka Kinyerezi ni kilomita 550. Safari hii ni sisi wenyewe tunachimbia bomba. Gharama za bomba, uchimbaji, fidia ya linamopita, compressors za kusukuma gasi na maintanance zake na mengineyo.
Hivi vyote kweli inakuwa rahisi kuliko kuprocess gasi na kufua umeme hapo Mnazi Bay na kusambaza umeme kutokea hapo?
Je ingekuwa vibaya kusambaza viwanda na ajira mpaka huko kusini?
Nani anafaidika na hii shughuli ya kufikisha gasi Dar?

Uelewa mdogo sana unashamiri Tanzania especially sisi tuliopo huku Dar. Kuna yeyote kati yetu sis tuliopo dar amesikia wananchi wa miji na vitongoji vya Mtwara na Lindi wakilalamika hawana umeme? Kwanini hawalalamiki? Ni kwa vile tayari gesi ya Mnazi Bay inazalisha umeme pale Mtwara na unasambazwa humo. Artumas iliuzwa lakini mambo yake haya hapa: http://www.wentworthresources.com/p...27-The East African-Mtwara Energy Project.pdf na hapa: http://www.wentworthresources.com/pdf/reports/2006_Annual_Report.pdf

Vilevile, bomba la gesi kutoka visiwa vya Songosongo na lile kutoka Mnazi Bay zitaungana somwhere in Lindi, kijiji/mji mmoja unaitwa Somanga na kuendelea hadi Dar es Salaam. Litapita maeneo ya Mkuranga ambapo imegunduliwa gesi tele pia. Mmoja kauliza itwasaidia nini watu wa mikoa ile? Kwanza kabisa ni ajira - ujenzi wa miundombinu mara nyingi inajulikana kuhitaji nguvu kazi nyingi - gesi na mafuta pia. Ajira pia zitakuja kwa njia zingine - tumesikia viwanda vinajengwa huko. Inawezekana ni mwendo taratibu lakini kuna msemo wamarekani husema, "If you build it they will come"

Bomba linakuja Dar kwani tayari pameshajengwa mitambo ya kubadilisha gesi kuwa umeme. Isitoshe, kuna viwanda kadhaa tayari vinatumia gesi hiyo, kuna nyumba za majaribio zinazotumia gesi kwa ajil;i ya matumizi ya nyumbani kupikia na labda baadaye for HVAC (heating, Ventilation and air conditioning) MICHUZI: mradi utaomaliza kabisa kero ya mgao wa umeme nchini

Vilevile, ingekuwa vema sis wananchi tuwe makini kidogo kusoma mambo mengi tuu. Kwa muda wako mwenyewe hebu sikiliza hii: BBC Swahili - Medianuai - Gesi Tanzania inafaidi nani? na peruzi hizi zifuatazo: http://www.mem.go.tz/wp-content/upl...licy-Draft-Management-MEM-29-October-2012.pdf na http://www.mipango.go.tz/documents/MPANGO WA MAENDELEO final.pdf na http://www.ecfa.or.jp/japanese/act-pf_jka/H21/JDI_tanzania/english.pdf.
 
Back
Top Bottom