Bomba la Mnazi Bay mpaka Dar

Bomba la Mnazi Bay mpaka Dar

Unashangaa hayo tu mkuu,hata kuoa,watu wanaoa Dar,mtu kwao Namtumbo na kakulia huko,lakini mke anatafuta hapo hapo Dar.

H
arusi anafungia Dar na ndugu kama 6 au 7 anawasafirisha kutoka Namtumbo kuja Dar kwenye harusi,badala ya wao wawili tu kusafiri kwenda kufunga harusi huko Namtumbo.

M
wingine yuko mikoani huko anafanya kazi,anapata mchumba hukohuko countyside,ila kwa sababu alishawahi kuishi Dar kidogo na anandugundugu tena wengine ni wakuunga unga anataka au anakuja kufunga harusi Dar au kufanyia send of Dar.

H
uku akisafirisha ndugu zake kutoka mkoa mwingine tofauti na anakoishi kuja Dar , we acha tu,kuna watu wameikariri Dar hata uwape kazi ya maana mkoani hawaendi kisa Dar, duuuh,Dar kuna nini wajameni?

Ni ujinga wa think tank ya taifa
 
Mimi nisie na shule nilishangaa kuona wanasafirisha mali ghafi badala ya kutengeneza umeme pale na kisha kusafirisha umeme na si gas hii kitu sijui itaisha lini?


Hii ni sawa

Songo Songo mpaka Dar ni zaidi ya kilomita 200 – tuliruhusu wachimbie bomba la gasi badala ya kufua umeme Songo Songo na kuvuta waya mpaka dar (na kwingine). Anayetabasamu mpaka benki ni mkanada mwenye kandarasi ya kumaintain bomba na mitambo yake.

Sasa naambiwa Mnazi Bay mpaka Kinyerezi ni kilomita 550. Safari hii ni sisi wenyewe tunachimbia bomba. Gharama za bomba, uchimbaji, fidia ya linamopita, compressors za kusukuma gasi na maintanance zake na mengineyo.
Hivi vyote kweli inakuwa rahisi kuliko kuprocess gasi na kufua umeme hapo Mnazi Bay na kusambaza umeme kutokea hapo?
Je ingekuwa vibaya kusambaza viwanda na ajira mpaka huko kusini?
Nani anafaidika na hii shughuli ya kufikisha gasi Dar?
 
Uelewa mdogo sana unashamiri Tanzania especially sisi tuliopo huku Dar. Kuna yeyote kati yetu sis tuliopo dar amesikia wananchi wa miji na vitongoji vya Mtwara na Lindi wakilalamika hawana umeme? Kwanini hawalalamiki? Ni kwa vile tayari gesi ya Mnazi Bay inazalisha umeme pale Mtwara na unasambazwa humo. Artumas iliuzwa lakini mambo yake haya hapa: http://www.wentworthresources.com/p...27-The East African-Mtwara Energy Project.pdf na hapa: http://www.wentworthresources.com/pdf/reports/2006_Annual_Report.pdf

Vilevile, bomba la gesi kutoka visiwa vya Songosongo na lile kutoka Mnazi Bay zitaungana somwhere in Lindi, kijiji/mji mmoja unaitwa Somanga na kuendelea hadi Dar es Salaam. Litapita maeneo ya Mkuranga ambapo imegunduliwa gesi tele pia. Mmoja kauliza itwasaidia nini watu wa mikoa ile? Kwanza kabisa ni ajira - ujenzi wa miundombinu mara nyingi inajulikana kuhitaji nguvu kazi nyingi - gesi na mafuta pia. Ajira pia zitakuja kwa njia zingine - tumesikia viwanda vinajengwa huko. Inawezekana ni mwendo taratibu lakini kuna msemo wamarekani husema, "If you build it they will come"

Bomba linakuja Dar kwani tayari pameshajengwa mitambo ya kubadilisha gesi kuwa umeme. Isitoshe, kuna viwanda kadhaa tayari vinatumia gesi hiyo, kuna nyumba za majaribio zinazotumia gesi kwa ajil;i ya matumizi ya nyumbani kupikia na labda baadaye for HVAC (heating, Ventilation and air conditioning) MICHUZI: mradi utaomaliza kabisa kero ya mgao wa umeme nchini

Vilevile, ingekuwa vema sis wananchi tuwe makini kidogo kusoma mambo mengi tuu. Kwa muda wako mwenyewe hebu sikiliza hii: BBC Swahili - Medianuai - Gesi Tanzania inafaidi nani? na peruzi hizi zifuatazo: http://www.mem.go.tz/wp-content/upl...licy-Draft-Management-MEM-29-October-2012.pdf na http://www.mipango.go.tz/documents/MPANGO WA MAENDELEO final.pdf na http://www.ecfa.or.jp/japanese/act-pf_jka/H21/JDI_tanzania/english.pdf.

Most informative and informative post of the thread

tatizo wenye vichwa kama vyenu mko wachache humu

Big up bro!
 
Back
Top Bottom