Bodi ya Pamba: Mfano wa kuigwa Duniani

Bodi ya Pamba: Mfano wa kuigwa Duniani

Bodi hizi zitazamwe upya ni mzigo kwa mlipa kodi wa Tanzania. Wafanyakazi kibao ufanisi SIFURI
Ni kweli kabisa na kuna bodi nyingine hazi sikiki kabisa mathalani Bodi ya pareto,Bodi ya kahawa,Bodi ya korosho na wakati wa Mwalimu zilikua na ufanisi zikawa kama nyimbo kwenye vyombo vya habari.
 
Bahati nzuri mtumbua majipu naye alishalima pamba anajua uozo wenu,mnauza mbegu hazioti,hamna mkakati wa kufufua zao,hata register ya wakulima hamna,jineri zimekufa mbele ya macho yenu,mmeishia kuwatoza wakulima tozo mbalimbali,jipu la bodi ya pamba linatoa usahaha,unadondoka wenyewe kabla dokta hajafika,na akifika helmet ni muhimu kutokana na wingi wa usaha,nafikiri pengine yale magari ya kufyonza kinyesi yangefaa,mpira uwekwe kwenye tundu la jipu gari lifyonze
Ginnery zilikuwa zinamilikiwa na vyama vya ushirika sio bodi ya Pamba. Christopher Chiza aliihujumu sana hii bodi na mwenzie Wassira. Ngoja tuone Mwigulu atafanya nini?
 
Bahati nzuri mtumbua majipu naye alishalima pamba anajua uozo wenu,mnauza mbegu hazioti,hamna mkakati wa kufufua zao,hata register ya wakulima hamna,jineri zimekufa mbele ya macho yenu,mmeishia kuwatoza wakulima tozo mbalimbali,jipu la bodi ya pamba linatoa usahaha,unadondoka wenyewe kabla dokta hajafika,na akifika helmet ni muhimu kutokana na wingi wa usaha,nafikiri pengine yale magari ya kufyonza kinyesi yangefaa,mpira uwekwe kwenye tundu la jipu gari lifyonze
Msamehe mtoa mada maana n mfanyakazi katika bodi ya pamba. Ko anajarbu kuona kama kweli bodi ya pamba inakubalika ....
 
Tafadhali Mhe.Waziri Nchemba usivunje bodi hii tuna watoto wadogo wanatutegemea. Kama ni mapungufu tutajirekebisha kidogo kidogo
 
Tafadhali Mhe.Waziri Nchemba usivunje bodi hii tuna watoto wadogo wanatutegemea. Kama ni mapungufu tutajirekebisha kidogo kidogo
Bwana kaka Bodi siyo kitalu cha kukuzia watoto, usifanye utani kwenye issue za msingi. Waziri atimize wajibu wake achunguze, kama hakuna tija kuwa na bodi na ifutiliwe mbali. Tafuta njia mbadala za kukuza wanao, ziwe standby kukusaidia likitokea lolote. Vinginevyo chapa kazi kwa weledi kwa sababu waliowapeni kazi watajua kama mnafanya ama mnafuja pesa za walipa kodi bila sababu. Angalizo, Watanzania hawa ukiwauliza watasema kila kitu kivunjwe, hata hawaeleweki. Kila kitu wao hakifai, akishindwa kesi mahakamani atasema mahakama hazifai, shule za tz zote hazifai, madaktari hawafai, polisi wa tz wote hawafai, jeshi nalo halifai, mabwana shamba nao hawafai, ma Rc na Dc na hawana kazi wafutwe. Ukiwasikiliza sana hawa watz utapoteza muda bure.
 
Wafanyakazi wengi tuna mikopo benki mnataka tulipe na nini? Acheni Bodi ya Pamba iendeleze pamba nchini
 
dogo acha mzaha kwenye maisha ya watu,unaipongeza bodi kwalipi?watu wanalima mpunga dabala ya pamba ww ndiyo unasifia bodi.
 
Sisi wakulima wa Pamba kanda ya Ziwa tunajivunia bodi ya Pamba Tanzania kwa kufanya kazi zake kwa WELEDI mkubwa katika kututafutia masoko ndani na nje ya nchi kwa uharaka sana. Wakulima wenzangu wa pamba ni mashahidi kwa hili kwani tunajivunia pamba na jasho letu wengi wetu tumeweza kuwekeza katika miraid mikubwa mikubwa ya maendeleo na kilio cha kisasa kabisa (Teknolojia za kisasa) Kama ingekuwa uwezo wangu ningepandisha hadhi bodi hii na iwe wizara kamili (WIZARA ya MAENDELEO ya PAMBA)
** WEBSITE: www.cotton.or.tz
NB: Wafanyakazi wa bodi hii wanastahili pongezi hasa tukiazimisha siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)

Tunataka substance ya kile unachokisema. Tuambie kwanza pamba inachangia kiasi gani katika pato la taifa ili tuchagie vizuri zaidi.
 
dogo acha mzaha kwenye maisha ya watu,unaipongeza bodi kwalipi?watu wanalima mpunga dabala ya pamba ww ndiyo unasifia bodi.

Kweli kabisa Mkuu. Asije akawa anapongeza kikundi kidogo cha watu wanaokaa vikao na kujilipa posho kubwa kwa kutumia fedha ya wakulima mskini bila ya kile wanachokisimamia kuwa na manufaa yoyote kwa uchumi wa nchi. Hizi Bodi ni ugonjwa mwingine mbaya sana katika nchi hii.
 
Kila kitu Bodi mara Kamati hii nchi yetu hii. Kitu kidogo tuu utasikia kimeundiwa kamati or Bodi. Wizara za kazi gani sasa
 
bodi hii isifutwe wandugu wacheni tumalizie nyumba zetu kwanza ndo muje na hizo maneno. UKAWA mpoje asee kila kitu kikifutwa tutajengaje nchi/Viwanda?
 
Mleta mada unasumbuliwa na brain conqution.Hivi unajua kuwa zao la Pamba huku kanda ya ziwa limekufa 75%????.Wakulima wengi wako busy na mazao ya chakula na ndiyo wanayoyatumia kama mazao ya biashara pia lkn hilo zao la pamba hawataki hata kulisikia.
 
Back
Top Bottom