Bodi ya Pamba: Mfano wa kuigwa Duniani

Andrew123

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
8,281
10,794
Sisi wakulima wa Pamba kanda ya Ziwa tunajivunia bodi ya Pamba Tanzania kwa kufanya kazi zake kwa WELEDI mkubwa katika kututafutia masoko ndani na nje ya nchi kwa uharaka sana. Wakulima wenzangu wa pamba ni mashahidi kwa hili kwani tunajivunia pamba na jasho letu wengi wetu tumeweza kuwekeza katika miraid mikubwa mikubwa ya maendeleo na kilio cha kisasa kabisa (Teknolojia za kisasa) Kama ingekuwa uwezo wangu ningepandisha hadhi bodi hii na iwe wizara kamili (WIZARA ya MAENDELEO ya PAMBA)
** WEBSITE: www.cotton.or.tz
NB: Wafanyakazi wa bodi hii wanastahili pongezi kila siku mpya inapowadia.
**PAMBA KWA MAENDELEO YA VIWANDA.
 
Bodi hizi zitazamwe upya ni mzigo kwa mlipa kodi wa Tanzania. Wafanyakazi kibao ufanisi SIFURI
 
kama ni kweli sifa hizi, mnastahili pongezi za haja. ila hilo la kuundiwa wizara yenu peke yenu siliafiki linakwenda kinyume na dhana ya kubana matumiz
 
Kilimo cha Pamba kilipaswa kuwa mkombozi wa wana kanda ya ZIWA! iwe na viwanda vingi vya nguo sijui mpaka leo kuna viwanda vingapi
 
Siku zote najiuliza iweje zao lilimwe Tanzania na kupelekwa nchi jirani kwa bei nzuri kwa mkulima lakini kwenye bodi zetu mkulima apate bei ndogo?
Wapi kuna tatizo?
Magufuli tumbua hilo kuwasaidia wakulima
 
Bodi hii ni ya kuongezewa jukumu ikiwemo lile la UTALII ili tupate ufanisi wa hali ya juu
 
Bahati nzuri mtumbua majipu naye alishalima pamba anajua uozo wenu,mnauza mbegu hazioti,hamna mkakati wa kufufua zao,hata register ya wakulima hamna,jineri zimekufa mbele ya macho yenu,mmeishia kuwatoza wakulima tozo mbalimbali.

Jipu la bodi ya pamba linatoa usahaha,unadondoka wenyewe kabla dokta hajafika,na akifika helmet ni muhimu kutokana na wingi wa usaha,nafikiri pengine yale magari ya kufyonza kinyesi yangefaa,mpira uwekwe kwenye tundu la jipu gari lifyonze.
 
Kiukweli tunatakia kila la heri bodi ya pamba kwa malengo waliojiwekea ni taasisi ya kupigiwa mfano dunia nzima
 
Ukiwauliza kwa nini bei ya Pamba inashuka wanapepesa midomo,soko kubwa na wanunuzi Wakubwa wa pamba akina Nani duniani hawajui ukiwawailiza walivutia viwanda vingapi vya nguo za kisasa vije nchini,acha vile vya kaniki na khanga,hakuna,wanawqza kuuza Pamba nje miaka nenda rudi wanapanda ndege kwenda ulaya,eti kusaka soko,
 
Sisi wakulima wa Pamba kanda ya Ziwa tunajivunia bodi ya Pamba Tanzania kwa kufanya kazi zake kwa WELEDI mkubwa katika kututafutia masoko ndani na nje ya nchi kwa uharaka sana. Wakulima wenzangu wa pamba ni mashahidi kwa hili kwani tunajivunia pamba na jasho letu wengi wetu tumeweza kuwekeza katika miraid mikubwa mikubwa ya maendeleo na kilio cha kisasa kabisa (Teknolojia za kisasa) Kama ingekuwa uwezo wangu ningepandisha hadhi bodi hii na iwe wizara kamili (WIZARA ya MAENDELEO ya PAMBA)
** WEBSITE: www.cotton.or.tz
NB: Wafanyakazi wa bodi hii wanastahili pongezi hasa tukiazimisha siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)

Mkuu umenigusa aisee.
Hii ndo imenisomesha mpaka sasa nakula bata mjini.
Hili zao pamoja na kwamba tulikuwa tunanyonywa sana enzi hizo kuhusu bei, lakini ndo mkombozi wa maisha yangu.

Siku ya kuuza kulikuwa na Mzee mpimaji wa mizani (mzee Mwanzalima) lilikuwa linatuibia kilo zetu. hahahahaha, Mzigo ni kilo 90 lenyewe litasema 85 kilo tano hapo zimeondoka. Na hauwezi kuhoji. Nashangaa kwanini serikali imeshindwa kulithamini zao hili jamani. Hata Mh. Magufuli pale kwao Rubambangwe walikuwa wanalima sana pamba.
 
Ukiwauliza kwa nini bei ya Pamba inashuka wanapepesa midomo,soko kubwa na wanunuzi Wakubwa wa pamba akina Nani duniani hawajui ukiwawailiza walivutia viwanda vingapi vya nguo za kisasa vije nchini,acha vile vya kaniki na khanga,hakuna,wanawqza kuuza Pamba nje miaka nenda rudi wanapanda ndege kwenda ulaya,eti kusaka soko,
Pamoja na kwamba mtoa hoja kawapamba bodi isivyostahiki na pengine kaamua tu kutoa hoja ili asikilize perception ya watu kuhusu bodi, bahati mbaya na wewe pia comments zako zinaonesha usivyojua kitu. Suala la bei kwa mfano mpaka uwaulize bodi, kwa hivyo bei ya petroli mpaka uwaulize ewura, shame on you.

Kwamba soko kubwa la pamba duniani nalo mpaka uwaulize bodi (great thinker). Labda Kwenye issue ya kuvutia uwekezaji hapo unaweza kuwa na hoja, lakini kabla ya kuwalaumu tcb ulitakiwa uje na mifano ya taasisi ndogo kama tcb ambayo imevutia huo uwekezaji.

Hili ni suala kubwa linalohitaji mkono wa serikali. Tcb walaumiwe kama hawajawahi kushauri chochote serikalini lakini vingine usichangie kitu usichokijua.
 
Sisi wakulima wa Pamba kanda ya Ziwa tunajivunia bodi ya Pamba Tanzania kwa kufanya kazi zake kwa WELEDI mkubwa katika kututafutia masoko ndani na nje ya nchi kwa uharaka sana. Wakulima wenzangu wa pamba ni mashahidi kwa hili kwani tunajivunia pamba na jasho letu wengi wetu tumeweza kuwekeza katika miraid mikubwa mikubwa ya maendeleo na kilio cha kisasa kabisa (Teknolojia za kisasa) Kama ingekuwa uwezo wangu ningepandisha hadhi bodi hii na iwe wizara kamili (WIZARA ya MAENDELEO ya PAMBA)
** WEBSITE: www.cotton.or.tz
NB: Wafanyakazi wa bodi hii wanastahili pongezi hasa tukiazimisha siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)
Wakulima wanakimbia kulima zao la pamba kwa sasa,wanahamia katika kilimo cha alizeti,ufuta.Bei ya pamba ni hovyo kabisa
 
Sisi wakulima wa Pamba kanda ya Ziwa tunajivunia bodi ya Pamba Tanzania kwa kufanya kazi zake kwa WELEDI mkubwa katika kututafutia masoko ndani na nje ya nchi kwa uharaka sana. Wakulima wenzangu wa pamba ni mashahidi kwa hili kwani tunajivunia pamba na jasho letu wengi wetu tumeweza kuwekeza katika miraid mikubwa mikubwa ya maendeleo na kilio cha kisasa kabisa (Teknolojia za kisasa) Kama ingekuwa uwezo wangu ningepandisha hadhi bodi hii na iwe wizara kamili (WIZARA ya MAENDELEO ya PAMBA)
** WEBSITE: www.cotton.or.tz
NB: Wafanyakazi wa bodi hii wanastahili pongezi hasa tukiazimisha siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)
Hizo sifa sizo kaka. Suala la bei ikiwa ndogo ama kubwa si lawama wala si sifa kwa tcb. Tcb ama serikali haina la kufanya katika bei ya pamba duniani, Hiyo teknologia unayoitaja ni ipi? Ni kweli kuna mambo wanayostahiki pongezi lakini siyo hizi za kwako.
 
Back
Top Bottom