Bodi ya Pamba: Mfano wa kuigwa Duniani

Bodi ya Pamba: Mfano wa kuigwa Duniani

Bahati nzuri mtumbua majipu naye alishalima pamba anajua uozo wenu,mnauza mbegu hazioti,hamna mkakati wa kufufua zao,hata register ya wakulima hamna,jineri zimekufa mbele ya macho yenu,mmeishia kuwatoza wakulima tozo mbalimbali,jipu la bodi ya pamba linatoa usahaha,unadondoka wenyewe kabla dokta hajafika,na akifika helmet ni muhimu kutokana na wingi wa usaha,nafikiri pengine yale magari ya kufyonza kinyesi yangefaa,mpira uwekwe kwenye tundu la jipu gari lifyonze
Hata mi nimeshindwa kumuelewa huyu jamaa, nadhani ameleta mada ili uozo wa hii bodi ujulikane. Mi sioni majukumu yake kabisa, tena kwa taarifa tu, ktk mazao yanayoelekea kutoweka nchini ni pamoja na zao la pamba.

Hili zao lina gharama kubwa kulizalisha na faida yake ni ndogo, wananchi wamepata mazao mbadala, jamii ya mikunde na alizeti. Pamba itakufa tu. Tatizo ni mnunuzi wa kati, huyu hupata faida kubwa kuliko mkulima. Aondolewe.
 
Uzuri wa taasisi yoyote ni pale ambapo inaweza kuwasaidia watu wakati wa matatizo. Kwa kusema hivyo nina maana bodi ya Pamba kama imeweza kuwasaidia wananchi wake kupata soko wakati wa matatizo ya soko ni bodi nzuri. Kama soko limepatikana tu kwa sababu ya nguvu ya soko yaani mahitaji ya pamba ni makubwa duniani na hivyo kupelekea bei kuwa juu bodi haihitaji kusifiwa sana
Hawajawahi kufanya lolote kati ya hayo, hii bodi ni ya kuvunjwa tu.
 
Tanzania inajitaji akina MAGUFULI kama 20 kwa pamoja ndipo akili yetu inaweza kukaa kwenye mstari!

Watendaji sa serikali wengi ni mzigo kwa wananchi. Hizi bodi na idara nyingi wanakula pesa wasiyoifanyia kaz. Wanalelewa na wananchi
 
Tanzania ni nchi pekee yenye kuzalisha pamba safi duniani (Anonymous, 2017).
 
KIONGOZI: Pamba safiiiiiii......
WaNANCHI: Safiii
KIONGOZI: tumezalisha pamba kuliko nchi yoyote Duniani wazungu wanatuonea wivu....sitakubali watuibie pamba yetu.
 
Tunajivunia bodi hii kwa kutuinua wakulima wa pamba nchini. Asanteni sana
 
Sisi wakulima wa Pamba kanda ya Ziwa tunajivunia bodi ya Pamba Tanzania kwa kufanya kazi zake kwa WELEDI mkubwa katika kututafutia masoko ndani na nje ya nchi kwa uharaka sana. Wakulima wenzangu wa pamba ni mashahidi kwa hili kwani tunajivunia pamba na jasho letu wengi wetu tumeweza kuwekeza katika miraid mikubwa mikubwa ya maendeleo na kilio cha kisasa kabisa (Teknolojia za kisasa) Kama ingekuwa uwezo wangu ningepandisha hadhi bodi hii na iwe wizara kamili (WIZARA ya MAENDELEO ya PAMBA)
** WEBSITE: www.cotton.or.tz
NB: Wafanyakazi wa bodi hii wanastahili pongezi kila siku mpya inapowadia.
**PAMBA KWA MAENDELEO YA VIWANDA.
Duniani? Au kanda ya Ziwa?
 
Back
Top Bottom