Mkuu umenigusa aisee.
Hii ndo imenisomesha mpaka sasa nakula bata mjini.
Hili zao pamoja na kwamba tulikuwa tunanyonywa sana enzi hizo kuhusu bei, lakini ndo mkombozi wa maisha yangu.
Siku ya kuuza kulikuwa na Mzee mpimaji wa mizani (mzee Mwanzalima) lilikuwa linatuibia kilo zetu. hahahahaha, Mzigo ni kilo 90 lenyewe litasema 85 kilo tano hapo zimeondoka. Na hauwezi kuhoji. Nashangaa kwanini serikali imeshindwa kulithamini zao hili jamani. Hata Mh. Magufuli pale kwao Rubambangwe walikuwa wanalima sana pamba.