Bodi ya mikopo na serikali,je haya malipo ya shilingi 20,000/= ni sahihi ili kupata namba ya utambulisho wa makazi (NaPa) ?

Bodi ya mikopo na serikali,je haya malipo ya shilingi 20,000/= ni sahihi ili kupata namba ya utambulisho wa makazi (NaPa) ?

digba sowey

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
10,141
Reaction score
22,022
Bodi ya mkopo inapaswa isitishe mara moja kipengere Cha anwani ya makazi yaani National Physical Address (NaPa) kama kigezo kikuu Cha kutoa mikopo Kwa watoto wetu kwani kina changamoto nyingi sana ambazo kuzikamilisha inakuwa ngumu na pengine Kuna mianya ya rushwa.

Binafsi nakubaliana na huu mfumo ni mzuri maana umelenga kubaini wale wote wanaopewa mkopo wanajulikana walipo lakini pia nadhani taarifa za makazi yao ziko kwenye mfumo hivyo inakuwa ni rahisi kujua mhusika anayepewa mkopo ana hali gani ya makazi(maisha)

Changamoto zilizopo Kwa Sasa ni kuwa Kuna ucheleweshawaji wa utoaji wa namba ya utambulisho,Mimi nimeomba namba kwajili ya kijana wangu ,Sasa ni siku ya Tano Sasa sijapewa na wala ninavyoona hakuna dalili za kupewa hiyo namba,Sasa nabaki kujiuliza huu mfumo utatoa matokeo sahihi kweli na waombaji wa mkopo watafanikiwa kumaliza maombi Yao Kwa Muda sahihi ikiwa Toka niombe hakuna dalili ya kupata kile nilichooomba?

Pili Kuna mianya mikubwa ya rushwa ,huu mfumo uliopaswa kuwa wakujitegemea sio ili nipate namba Hadi ni mfuate Afsa mtendaji wa Kijiji ndo anipatie huduma, kama ndivyo serikali itoe semina Kwa watu wengi ili iwe rahisi kupata huduma hii,au iuache huu mfumo uwe self- service,mtu ajihudumie mwenyewe bila kuhitaji isaidizi wa mtu wa chini kama mtendaji wa Kijiji ambaye Kila tukio likija mbele yake anawaza rushwa ,juzi Kuna kijana amefika katika ofisi yangu kuomba mkopo nikamwambia aende Kwa mtendaji apate Namba ya NaPa,Cha kushangaza mtendaji anamwambia atoe shilingi 20,000 ili aende kusajiliwa nyumba yake.

Sasa najiuliza watanzania wengi hatuna elimu ya teknolojia ,mifumo na computer,je sisi kama watanzania wa chini tutajuaje kuwa nyumba imesajiliwa au haijasiliwa,naona hii ni kama njia ya maafisa watendaji kuvuna pesa Kwa watanzania wanyonge Kwa kigezo Cha nyumba Yako haijasajiliwa,na je hayo malipo ya shilingi 20,000 ni malipo halali ya serikali!?

Tatu, bodi ya mikopo kutumia namba ya anwani ya makazi (NaPa) inawapa shida wapangaji kwani ni kweli kuwa unakuta umepanga au nyumba Ina wapangaji zaidi ya wapangaji 5, na wote wanatumia anwani ya mtu moja yaani baba wa nyumba,Sasa uelewa duni baba wa nyumba akisikia kuwa taarifa za nyumba yake zinahitajika ili mtoto wa mpangaji wake apate mkopo hawezi kukubali, maana mtu akisikia mkopo anajua moja Kwa moja nyumba yake inatumika kama dhamana ya mkopo na mwisho wa siku itauzwa,hivyo baba /mama wa nyumba hawako tayari kutoa taarifa za nyumba zao ili kufanikisha zoezi hili na hivyo bodi ya mikopo ya mwaka huu haiko tayari kabisa kutoa nafuu Kwa mtoto wa masikini bali wanatamani kabisa asifanikiwe kuomba.


Mwisho naiomba bodi ya mikopo iache kuja na hoja za kuupamba huu mfumo,kwani haufai na unachangamoto nyingi sana,haufai kutumika kama kigezo Cha kuwanyima mikopo watoto wetu ambao tunajua ni watanzania na wala hawana Passport za nchi za ng'ambo kwamba watakimbia ili wasilipe mkopo huu, Pia bodi ya mikopo ijipe Muda ili kuweka mazingira mazuri ambayo yatakuwa rafiki Kwa Kila mtanzania anayehitaji huduma hii bila vikwazo.


Ahsante sana
 
kujisajili bodi ya mkopo 30000/= alafu samia anakwambia hana deni
 
Ndiyo mtumie namba za nyumba zenu.
Elewa msingi wa hoja,hiyo nyumba ni yako,sasa usije kutuna hapa eti na wewe ni baba wa nyumba,upuuzi mtupu,hoja yangu ni kuwa hata Mimi siwezi toa taarifa za nyumba yangu ili kufanikisha swala la mkopo kwa mtu


Sasa wewe umeona kapoint hako ili kujitutumua tujue kuwa na wewe ni baba wa nyumba
 
Huu ni wizi Mama Samia Angalia hili, namba ya Nida inatosha hizo napa sijui kitu gani ni kukiuka maagizo ya Raisi Mama Samia mifumo kusomana.
 
Back
Top Bottom