Bodaboda wote wahakikiwe na kupatiwa leseni ya kozi maalum ya kubeba abiria

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Hatuwezi kusema moja kwa moja kazi ya boda ni laana!

Lakini matendo ya madereva bodaboda wengi wao nikama wana laana!

Huko barabarani honi ndiyo breki, hawana kusubiri, wanaovateki hovyo wakiamini wapo sahihi muda wote!

Bahati mbaya boda anapoovateki kushoto na mwenye gari ikawa anakwepa shimo ghafla na kumgonga boda huwa anaamini yupo sahihi hata kuhatarisha chombo cha mtumia!

Nashauri kwa tabia zao nyingi mbaya!
Jeshi la polisi lipitishe kanuni mpya za usalama barabarani!
Pia tufanye marekebisho ya sheria ya usalama!
Kwamba boda boda za abiria ziwe na leseni maalum! Ambayo itolewe baada ya mafunzo semina ya jeshi la polisi!

Ili kuepusha udanganyifu kutoka kwa maafisa wa polisi wasio waaminifu, kuwepo na kanzu data ya kusajili wanaoanza mafunzo hata wanaomaliza mafunzo na kukabidhiwa leseni hizo maalum!

Wafundishwe utii wa sheria, ulinzi na usalama wa wengine!

Pia nashauri kwa madereva wanaofanya uhalibifu wa mali za wengine wanapo kamatwa adhabu ziwe kali ikiwemo kupokonywa leseni, fidia kwa mhanga, faini kubwa, kifungo na adhabu kubwa ikiwemo bakola 70!
 
Nimetoka sasahivi kugombana na bodaboda baada ya kuigonga side mirror yangu nilikuwa nakwepa mashimo huku bodaboda akija mbele yangu tena speed kubwa...
Ni bahari Tu side mirror iko vizuri, hii Ajira ya bodaboda ni matatizo mno Kwa vijana
 
bodaboda wengi hawana ajira ,hawana mshahara WA mwezi hawana connections sometimes wanafosi tu Ili kuleta chakula mezani

Tuwaache wapambane
 
Ajabu sana na mda wote wao wapo sahihi hawajui kukosea
 
Serikal ni kama imewaachia waji regulate wenyewe, matokeo yake wanageuka kuwa gangs. Serikali
bodaboda wengi hawana ajira ,hawana mshahara WA mwezi hawana connections sometimes wanafosi tu Ili kuleta chakula mezani

Tuwaache wapambane
Ni ahira isiyo rasmi bur haimaanishi isiwe regulated
 
Back
Top Bottom