Upofu wa Jeshi la Polisi juu ya bodaboda

SE-CHANDO

Member
Oct 18, 2023
5
2
Usafiri wa boda boda ni moja ya usafiri pendwa sana katika nchi yetu, Pia ni moja ya njia ya usafirishaji inayokuwa kwa kasi sana katika nchi yetu.

Hebu angalia hapa kitakwimu tu, kutoka mwaka jana ,2022/2023 mpaka kufikia mwezi machi zilikuwa zimetumika karibia Dola milioni 139 sawa na Pesa madafu za Tanzania Tsh 320 bilioni mzigo huo wote ulitumika kuagiza Pikipiki kwa kipindi hicho tu.

Licha ya hivyo serikali ilijitanabaisha kuwa boda boda ni moja ya ajira kwa vijana , nikitaka kufikiri naweza kuwaunga mkono pia, kwamaana na washikaji zangu wapo kwenye kada hii na tumemaliza nao kozi nzuri tu, nao sasa ni madereva boda boda na wanaishi Maisha yao yanaenda safi tu,

Na sio swala la kujiuliza sana ukienda vijijini utawakuta na ukiwa kwenye kila mji utawakuta tunao vijana wengi ambao wamejiajiri kwenye hii kada.

Chakushangaza Sasa, licha ya wanasiasa kuwatumia kila kukicha kwenye misafara yao yakisiasa huko na huko lakini wamewakalia kimyaa wamebaki kuwatanguliza mbele tuu.

Hawa watu mimi binafsi naona wameachwa, wametelekezwa, yaani wamekatiwa tamaa kabisa,

Ngoja niende kwenye lengo kuu, kiukweli mimi nimtumiaji wa barabara tatu kuu kila siku lazima nipite Barabara ya mandela, kilwa na Morogoro, niseme tu ukweli kwenye njia hizo nazopitia mimi kila mwezi lazima nikutane na ajali moja ya boda boda yani hiyo ajali lazima ihusishe watu kama sio watatu basi wawili nao hali zao duuh hawafiki hata dk 5 tunawaita marehemu

Maana hata wewe mwenyewe inafka muda unasema duu ni hatari, kwa mfano mwishoni mwa mwezi Nov pale vetinari duu alooh palikuwa kama machinjio maaana watu walikuwa wanaokota bandama na maini tuu…

Sasa nikawaza hii wizara ya mambo ya ndani ndio mtunga sera hivi hawana sera kwa ajili ya kupunguza ajali hizi za boda boda na wizi wa bodaboda…

Kwa watu wanaosimamia usalama wa barabarani ambalo ni jeshi la polisi sijui niseme wamelala au wamewakatia tamaa hawa ndugu zangu maana sioni measures yoyote ambayo wanayo kama mikakati au mipango ambayo inachukuliwa kwa ajili ya kupunguza hizi ajali…sijui labda maana nilisikia kauli ya mtu mmoja kwenye jeshi la polisi akihojiwa nakusema bodaboda ni kichefu chefu.

Na hata wale watu maana hata sijui kama ni askari ni wakina nani wanaokamata boda boda kwenye mataa wanakamata kwa utaratibu upi au ni wasaka tumbo tu, yaani wala rushwa tu maana hata sioni umaana wao kabisa kabisa

Rai yangu kwa serikali kupitia Jeshi la polisi ni mwanzo sasa wakuona hii sasa inatosha mpange mikakati maalum kwa ajili ya kudhibiti ajali hizi za boda boda mimi naamini hamjashindwa na mkitaka basi mnaweza.

Mosi, anzisheni kikosi maalum kwa ajili ya ufwatiliaji wa bodaboda ukaguzi na uendeshaji wao kama ilivyo kwa vyombo vingine vya moto, Uanzishwaji wa kikosi hicho unatokana na umuhimu na ukuaji wa kada hiyo ya boda boda, kupitia hili isiwe ndio mwanzo wakufungua mianya ya rushwa kwa kikosi hicho maana tunajuana anzisheni sheria ambazo zinatumbuguza rushwa kama ilivyokushushwa kwa adhabu kwenda elfu 10,000 pia mnaweza kuweka sheria ambazo zinafanya kuonya na zitapunguza rushwa kwa mfano kama atakamatwa kwa kutokuwa na kofia ngumu basi mnunulishe hiyo kufia Ngumu na zinginezo ambazo zitakuwa zinaonya na kufundisha pia.

Pili, Kabla ya kuanza hilo kupitia vikundi vyao vya boda boda kwenye kila kijiwe chao piteni wapeni elimu na sheria zenu ilikuweza kufahamu taratibu ziliopo na mambo muhimu yakufwata uwapo barabarani na mengine mengi mazuri.
 
Back
Top Bottom