Ajali za barabarani nyingi kusababishwa na waendesha bodaboda, nini kifanyike kudhibiti na kuzipunguza?

ong'wafaza

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
243
100
Nimkuwa nikifuatilia kwa muda mrefu takwimu zinazotolewa na polisi kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na janga la Ajali za barabarani zikionyesha kuwa bodaboda ndo chanzo kikuu Cha Ajali hizo hasa mijini.

Pamoja na ukweli huo kudhihirika,Bado mamlaka zinazohusika hazichukui hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo.
Pamoja na hatua kidogo ambazo mamlaka zinachukua Ili kupunguza Ajali hizi,Mimi napendekeza yafuatayo;-

1. Halimashauri na Serikali za mitaa zitunge Sheria ndogondogo za kuhakikisha kuwa Sheria za usalama barabarani zinafuatwa kikamilifu katika maeneo yao.

Kwa mfano,wamiliki wote wa bodaboda wasajiliwe na Serikali zao za mitaa/vijiji kwa masharti maalumu.
Ingependeza kama sharti la dereva kuwa na leseni liwe miongonii nwa masharti hayo.

2. Sheria ndogondogo hizo ziwabane madereva wa bodaboda pamoja na abiria wao kuhusu ukiukwaji wa Sheria hizo.

Kwa mfano,dereva akikamatwa Hana leseni na amepakia abiria,yeye na abiria wake wachukuliwe hatua Kali ikiwemo kutozwa faini .

Hii itawafanya abiria kudai leseni kwa dereva kabla hajapanda hiyo badaboda.

Na kwa hali hiyo,wamiliki na hata madereva wenye mapungufu mbalimbali watakosa abiria na hawatakuwa barabarani wakiendesha vyombo hivyo tena.

Mambo haya yakitekelezwa kikamilifu sio tu yatapunguza Ajali za barabarani zinazosababisha na bodaboda,Bali pia yataongeza mapato ya Serikali zetu za mitaa na vijiji kupitia faini watakazokuwa wanakusanya.

Swali;
Je, rushwa haitachukua mondo wake?
Naomba kuwasilisha.
 
Suluhisho la kudumu ni kupunguza ajira za bodaboda na kuongeza ajira nzuri zaidi
 
Ajira rasmi ndyo suluhisho sahihi,na hapo watabaki wenye uchungu na kazi yao ya bodaboda ndyo hutaskia ajali
 
Serikali ifanye hima hawa madogo wapewe mafunzo ya lazima ya matumizi ya barabara na sheria!! Wengi hawajui sheria na ndicho kinasababisha ajali!!

Na kwa sababu hiyo wenye magari hasa makubwa wanawapelekea tu si wanajua kosa ni lao!! Wanajaa maanina ikiangaliwa mwenye kosa nani boda na keshakufa na abiria wake!!! Jamaa anasepa zake, hili nililiona live mahali!!

Kingine: Siku hizi boda anafanya kosa then abiria aliyepakiwa anamjia juu mwenye gari!! Hivi wanajuaga wanakitetea kweli? Abiria nao wawe serious pengine boda watabadilia
 
Suluhisho lako ni zuri kiasi ila sio sahihi kwa bongo hii.

Ishu ya kofia ngumu. Hakuna asiejua msaada wa hizi kofia ngumu si dereva si abiria lakini abiria wenyewe tu hawataki kuzivaa hata kama zipo. Huyu abiria ndo amuulize boda leseni
 
Asilimia kubwa ya bodaboda ni wahuni tu ambao walikuwa vijana wa kijiweni kabla ya ujio wa hizi bodaboda, hawana uelewa wwte wa sheria za barabaran Kila muda wako race tu kiufupi Hawa watu ni majanga
 
Back
Top Bottom