Bodaboda hawana Haki

Bodaboda hawana Haki

Bodaboda hizi na sasa hivi naona bajaj zinachukua kasi
Hawa nao ni wale wale. Ukibahatika pita njia kama Moroko nwenge au daraja la Tanzanite unakuta kushoto bajaj kulia bajaj wote mwendo mmoja hawakupishi . Wanaboa sana kama vile njia ni yao tu. Au pita mtaa wa samora vile vinavyotoka feri mpaka stesheni ni kero tupu.
 
BabaMorgan kwa picha ya haraka unaweza kuwatetea bodaboda na kuwalaumu wanaowalaumu bodaboda hasa kwenye hizi ajali za barabarani.. Lakini bodaboda ni pasua kichwa hasa japo sio wote

Tunacholaumu wengi wetu ni matokeo na sio chanzo ama asili ya tatizo
Maono kimo cha mbilikimo ya mamlaka ya kisiasa ndio asili kuu. Ili kupunguza kelele za ajira wakaamua kuruhusu biashara huria ya pikipiki kama aina ya usafiri wa haraka bila maandalizi ya kutosha na bila kujali viwango vya chombo husika

Mwendelezo wa tatizo ni pale kijana asiye na mafunzo kamili na sahihi kukabidhiwa chombo cha moto kwa ajili ya biashara ya kubeba binadamu

Huyu kijana hana mafunzo kamili na sahihi ya kuendesha chombo cha moto, sheria na kanuni za barabarani, usalama wake na wa wengine, elimu ya uchumi nk.. Na hii yote inasababishwa na uwezo wa kifedha,, mafunzo ya udereva yanahitaji hela na kijana hana

Rushwa na ufisadi
Ili kijana athibitishwe ni dereva na amefuzu mafunzo ya udereva na kufaulu anahitaji nyaraka zinazothibitisha hilo.!! Leseni.. Kuipata leseni kwa kufuata utaratibu wa kisheria kunachukua muda na ni gharama
Kupitia vishoka na watendaji wa mamlaka ya mapato na jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wasiojali usalama wa raia na mali zao kijana anapata leseni chap kwa haraka na kwa bei poa
Kuna ukiukwaji mkubwa sana kwenye kupata leseni za udereva

Sasa kijana ana leseni na ana chombo cha moto anaanza biashara bila kufahamu walau kanuni moja tu ya kupita makutano ya barabara penye taa nyekundu

Majumuisho haya ya wanasiasa, watendaji wa serikali wasio waaminifu na vijana wasio na ajira matokeo yake ndio haya ya ajali zisizokoma, zinazoteketeza nguvu kazi ya taifa na kuleta uhujumu mkubwa wa uchumi kupitia vifaa tiba, vilema, uharibu wa vyombo na vifo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo uliyoandika ni sahii kabisa ila in advanced level.
Ajali nyingi za bodaboda huwa ni issue ya common sense kabisa na wala siyo elimu ya kufundishwa.
 
Kiukweli nachukizwa sana na wengi wa mabodaboda wabavyo behave

Huwa tunawasubiri hadi kwenye zebra wanakupigia honi, in short kwenye barabarani huwa sina tahadhari sana na magari kama ambavyo huwa nachukua kwenye hawa watu boda boda

Nimeshuhudia wakimgonga bimdada mmoja zebra, can you imagine mtu anagongwa zebra, afu wenzake wanamtetea eti bi Dada alivuka kwa mapozi sana, hivi zebra mtu anaweza tumia zaidi ya sekunde 30 kuvuka?? Sasa una haraka gani hiyo hadi ya 30s kuwa barrier kwako

Wajirekebishe
 
Alikuwa akikatisha barabara ya mwendokasi.
ukikatisha barabara kuu basi wewe unaekatisha iwe gari au bajaji au pikipiki uangalie pande zote na sio aliekuwa barabara kuu (STOP) mwingine akiona hakuna taa anaona kama ana haki.

4waystop.jpg
 
Bodaboda huwa hawajali sheria za barabarani unakuta taa hazijaruhusu wao wanapita tu tena bila tahadhari yoyote. Mara nyingi wanagongwa na mwendokasi pale mataa ya Shekilango.
 
Leo asubuhi pametokea ajali maeneo ya DIT iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki maarufu Bodaboda sina details za kutosha kuhusu madhara yaliyotokea kwa maana ya majeruhi au kama kuna kifo chochote lakini so far ni ajali mbaya maana time niliyokuwa napita basi la Mwendokasi lilikuwa linapigwa jeki na Pikipiki inatolewa chini ya uvungu mwa basi.

Kila mtu baada ya kuona mazingira yale alikuwa anatoa lawama kwa dereva bodaboda bila hata ya kuwa na picha halisi ya kile kilichotokea mpaka kusababisha ajali.

It's like ajali yoyote itakayohusisha bodaboda basi lawama zote atatupiwa bodaboda huu ni uonevu wa kiwango cha juu sio bodaboda wote hawaobey sheria za barabarani na sio kila dereva wa gari yupo perfect asilimia mia.

Tuheshimu Bodaboda nao ni Binadamu licha ya kuwa na mapungufu yao lakini still wana mema yao kama walivyo Binadamu wengine as long unajua kuendesha Pikipiki inabidi uwe mstari wa mbele kutetea bodaboda maana siku unaweza kuwa kwenye mizunguko yako ukapata mushikeli waka kuhukumu kama wanavyowahukumu bodaboda.
Boda boda wa DSM ndo kundi la wajinga zaidi bro , matrafiki wanatakiwa wawekeze nguvu Zaid Kwa hawa watu, usidhubutu kupanda boda katika any busiest road Dar es salaam
 
Mkuu
Ukiwa unapanda haya mabus ya mwendokasi kila siku, na ukawa unakaa pale mbele kabisa na dereva, utakubaliana na mimi kabisa kuwa bodaboda ni wapumbavu.

Na mbaya zaidi huwa wanajiaminisha kwamba hawezi kupatwa na hatari..
Gari ishatoka kasi, anaenda kujichomeka anavyopenda.

Mwendokasi huwa wanajitahidi mno kuwakwepa,
Muda mwingine hadi hupelekea gari lililobeba mamia ya watu kuyumba, kwa sababu ya mtu Moja aliyeamua kujitoa ufahamu na kukatiza bila mpangilio.


Kama mna ndugu zenu bodaboda na mnawapenda, tafadhali washaurini washikilie akili zao, badala ya kuziweka mfukoni.


Mwendokasi ina mapungufu mengi mno ila siyo kwa upande wa uendeshaji wa madereva .
Madereva wake wapo makini sana..
Laiti wangekuwa rafu kama wa daladala, ama wangekuwa na akili kama za bodaboda
Akiyanani kungekuwa na mamia ya misiba kila siku.
Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Boda huwa akili zao zinapita upepo muda mwingi, dereva huwezi ua watu 199 kumkwepa boda anaevuka mataa yakiwa yameruhusu upande wako nafikiri ndo ivo maana huwa wanafosi sana akikutana na dereva mstarabu uminya break ya gafla sasa abiria tuumie kwasabbu ya uzembe wa boda mmoja
Kuna siku dereva alikwepa bodaboda aliyejipachika
Gari iliyumba mno.

Siku nyingine tena hii ni last month..
Niligonga kichwa kwenye kiti cha mbele..
Hapo waliosimama sijui walikuwa na hali gani, kama siyo kuangukiana hovyo.
Yote Kwa sababu ya mtu aliyeamua kukatisha ghafla mahala ambapo taa hazijamruhusu.

Madereva wa mwendokasi ni wavumilivu mno,
Bodaboda wanatia hasira mno.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Namnukuu Godbless Lema..

"Boda boda ni Laana"

Na mimi naongezea kwamba, Uafrika hasa utanzania ni laana.

Kwa nchi zilizo endelea, First world countries, Bodaboda ni uchafu mjini.

Na si bodaboda tu, hata Bajaji ni takataka.

Zinachafua miji.
 
Sio DIT kabisa ni nyuma kidogo pale kwenye mataa ambapo kuna barabara ya kwenda Lumumba kama sijakosea.. Muda mwingine madereva wa mwendokasi wanadharau mataa.
Pale Zanzibar reassurance bodaboda hujikatizia tu wanavyotaka bila hata mataa kuwaruhusu.


Hao mwendokasi unasema hawafuati mataa si kweli.
Na kama wapo, basi ni asilimia 0.5

Bodaboda asilimia 99 ni vichaa huko Morogoro road.


Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Hii ajari nimeishuhudia live. Tukiwa tumesimama kusubiria kwasababu taa zilikuwa zimeruhusu Mwendokasi zipite, boda boda yule akaona anachelewa, akaangalia upande mmoja akaona kweupe akataka kukatisha kuingia Lumbumba hamadi Mwendokasi hii hapa. Mengine ni history. Ni uzembe wa bodaboda kwa asilimia zote
 
Namnukuu Godbless Lema..

"Boda boda ni Laana"

Na mimi naongezea kwamba, Uafrika hasa utanzania ni laana.

Kwa nchi zilizo endelea, First world countries, Bodaboda ni uchafu mjini.

Na si bodaboda tu, hata Bajaji ni takataka.

Zinachafua miji.
Ningepewa nafasi ya kuishauri serikali
Ningeishauri bodaboda na Bajaj vitolewe kabisa main road hasa hii Morogoro Road.

Yaani boda ni vichaa namba Moja kwenye hii barabara.


Kijijini kwao wanajua mtoto anapambana
Yeye anakuja kujikatizia tu kwenye mataa anavyotaka.

Bodaboda asilimia kubwa hawajitambui.
Serikali iingilie kati iwaokoe hawa watu Kwa kuwapiga marufuku hizi barabara kubwa..
Waendeshe ndanindani tu.
Vinginevyo wataendelea kulimwa vichwa na kusababishia watu wengine majanga Kwa upumbavu wao wa kutotii Sheria.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Leo asubuhi pametokea ajali maeneo ya DIT iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki maarufu Bodaboda sina details za kutosha kuhusu madhara yaliyotokea kwa maana ya majeruhi au kama kuna kifo chochote lakini so far ni ajali mbaya maana time niliyokuwa napita basi la Mwendokasi lilikuwa linapigwa jeki na Pikipiki inatolewa chini ya uvungu mwa basi.

Kila mtu baada ya kuona mazingira yale alikuwa anatoa lawama kwa dereva bodaboda bila hata ya kuwa na picha halisi ya kile kilichotokea mpaka kusababisha ajali.

It's like ajali yoyote itakayohusisha bodaboda basi lawama zote atatupiwa bodaboda huu ni uonevu wa kiwango cha juu sio bodaboda wote hawaobey sheria za barabarani na sio kila dereva wa gari yupo perfect asilimia mia.

Tuheshimu Bodaboda nao ni Binadamu licha ya kuwa na mapungufu yao lakini still wana mema yao kama walivyo Binadamu wengine as long unajua kuendesha Pikipiki inabidi uwe mstari wa mbele kutetea bodaboda maana siku unaweza kuwa kwenye mizunguko yako ukapata mushikeli waka kuhukumu kama wanavyowahukumu bodaboda.
Kwahyo boda boda wana haki ya kupita kwenye barabara za mabasi yaendayo kasi? Angalia ajali nyingi za boda lazima kuna tatizo mtu wa gari hawezi kuchomeka gari au kupenya kwenye foleni
 
Back
Top Bottom