Mkuu
Ukiwa unapanda haya mabus ya mwendokasi kila siku, na ukawa unakaa pale mbele kabisa na dereva, utakubaliana na mimi kabisa kuwa bodaboda ni wapumbavu.
Na mbaya zaidi huwa wanajiaminisha kwamba hawezi kupatwa na hatari..
Gari ishatoka kasi, anaenda kujichomeka anavyopenda.
Mwendokasi huwa wanajitahidi mno kuwakwepa,
Muda mwingine hadi hupelekea gari lililobeba mamia ya watu kuyumba, kwa sababu ya mtu Moja aliyeamua kujitoa ufahamu na kukatiza bila mpangilio.
Kama mna ndugu zenu bodaboda na mnawapenda, tafadhali washaurini washikilie akili zao, badala ya kuziweka mfukoni.
Mwendokasi ina mapungufu mengi mno ila siyo kwa upande wa uendeshaji wa madereva .
Madereva wake wapo makini sana..
Laiti wangekuwa rafu kama wa daladala, ama wangekuwa na akili kama za bodaboda
Akiyanani kungekuwa na mamia ya misiba kila siku.
Sent from my TECNO CG6 using
JamiiForums mobile app