Bodaboda hawana Haki

Bodaboda hawana Haki

Kama ulimwambia akukimbize chap Kariakoo ulitegemea nini? Ndio maana wanashauri na wewe kama abiria kuchukua tahadhari unapoona dereva wako anakiuka sheria
Abiria uchukue tahadhari gani mkiwa mko kwenye mwendo tayari? Kuna muda unapanda tu unamwambia twende taratibu, akishaona vipi sijui anasahau anavuta mafuta. Best way ni kutokupanda boda kabisa kwa wanaoweza japo kuna muda boda hazikwepeki.

Mimi napanda boda barabara za mtaani tu, main road hapana. Serikali Ifanye jambo vijana wa boda wataisha.
 
Sio DIT kabisa ni nyuma kidogo pale kwenye mataa ambapo kuna barabara ya kwenda Lumumba kama sijakosea.. Muda mwingine madereva wa mwendokasi wanadharau mataa.
Madereva wa mwendo kasi wanaheshimu taa na wapo makini njiani nishaona sehem tofauti wakipiga breki kupisha boda wanaoingia kimakosa mfano mzuri barabara ya msimbazi
 
Leo asubuhi pametokea ajali maeneo ya DIT iliyohusisha basi la Mwendokasi na Pikipiki maarufu Bodaboda sina details za kutosha kuhusu madhara yaliyotokea kwa maana ya majeruhi au kama kuna kifo chochote lakini so far ni ajali mbaya maana time niliyokuwa napita basi la Mwendokasi lilikuwa linapigwa jeki na Pikipiki inatolewa chini ya uvungu mwa basi.

Kila mtu baada ya kuona mazingira yale alikuwa anatoa lawama kwa dereva bodaboda bila hata ya kuwa na picha halisi ya kile kilichotokea mpaka kusababisha ajali.

It's like ajali yoyote itakayohusisha bodaboda basi lawama zote atatupiwa bodaboda huu ni uonevu wa kiwango cha juu sio bodaboda wote hawaobey sheria za barabarani na sio kila dereva wa gari yupo perfect asilimia mia.

Tuheshimu Bodaboda nao ni Binadamu licha ya kuwa na mapungufu yao lakini still wana mema yao kama walivyo Binadamu wengine as long unajua kuendesha Pikipiki inabidi uwe mstari wa mbele kutetea bodaboda maana siku unaweza kuwa kwenye mizunguko yako ukapata mushikeli waka kuhukumu kama wanavyowahukumu bodaboda.
...kwa hiyo ulitaka basi la mwendokasi liipishe boda?
 
Siku moja nimepanda bodaboda natoka Ubungo naenda Kimara , tuko njiani mbele kuna semi trailer mbili zinatembea mwendo wa kawaida ziko sambamba kwenye barabara la lane mbili. Yule dereva wa bodaboda si akaona uchocholo kati ya zile semi trailer mbili. Naona jamaa anaongeza speed anataka apite katikati ya yale maroli. Ikabidi nimvute shati nikamwambia aache ufala tutakufa vibaya
 
Back
Top Bottom