Boda boda sio sifa ni uchafu na umasikini mkubwa

Ukiachilia mbali kero ya uendeshaji wao, pia Kelele..

Mie naona Askari wa barabarani wameshindwa kazi yao..
Napendekeza ushuru uongezwe kwenye hizi bodaboda, iundwe kodi maalum kwa bodaboda.

Mbili, Bima iwe ya lazima ili awe bodaboda lazima awe na bima ya afya na ya chombo chake.

Tatu, mjini isikanyage.. akiingia na kukamatwa awe wa mfano, ikiwemo kutaifisha hiyo pikipiki.

Uzembe wa ajali za kugonga mtembea kwa miguu, ni kumfunga jela miezi 6+ na viboko 50 kila wiki.

Vishandu, hawa ndio wezi na wasumbufu.
Kuna operation iliendeshwa kipindi fulani, miili ilikuw inapelekwa monchwari ndg mkafate mzike.
 
Jamani, nimepitia hapa naona mjadala ni mzito na kila mtu ana hoja yake ya msingi. Ni kweli kabisa, suala la bodaboda lina changamoto zake nyingi, kuanzia kwenye usalama barabarani kama alivyoeleza Skull dance, kelele, na hata namna zinavyoendeshwa bila kufuata sheria. Hoja ya Kamundu kwamba si sifa ni ya msingi kabisa, na mawazo ya Gentlemen_ kuhusu bima na utaratibu bora yanaweza kutusaidia sana kuleta nidhamu.

Lakini tusisahau pia kwamba kwa vijana wetu wengi, bodaboda imekuwa kimbilio la ajira na njia muhimu ya kujipatia kipato, hasa kutokana na ukosefu wa fursa nyingine. Badala ya kuziondoa kabisa, labda tuangalie namna bora ya kuzisimamia na kuziboresha. Kuanzisha mafunzo mazuri, kuweka sheria kali na kuzisimamia, na muhimu zaidi, kuwekeza kwenye fursa zingine za ajira kwa vijana wetu, ndio kutaleta mabadiliko chanya tunayoyataka. Ni suala linalohitaji suluhisho la jumla na la kisera zaidi, litakalozingatia pande zote.
 
Boda boda sio sifa ni uchafu na umasikini mkubwa. Hatuwezi kama nchi kutegemea usafiri kwa madereva holela wa pikipiki ambao hawafuati sheria, pikipiki hazijatengenezwa kwa lengo la kubebea watu.

Vijana wanaendesha bila leseni. Boda bora zinatakiwa ziruhusiwe vijijini tu na kwa mijini ziruhusiwe tu kwa safari binafsi na kuwe na sehemu maalumu kwa maiskeli na pikipiki kama nchi nyingine. Hatuwezi kuendeleza vitu kisiasa tu vijana watafutiwe ajira na tuweke katiba bora ilete uwekezaji.
CCM wanajivunia kutengeneza ajira kupitia bodaboda🙆
 
Unajua byke zimetoa ajira kwa vijana wangapi?
unajua byke zimeua na kuzalisha vilema wangapi
Sheria iwekwe sharti dereva boda boda uwe kuanzia miaka 50, ni kazi isiyotumia nguvu wala akili
Vijana wafanye uzalishaji, nishati ujana inapotelea juu ya siti ya bodaboda mnakuja kusifia ujinga ujinga tu hapa
 
Nilikwenda South Africa hakuna Huo Upumbavu.

Boda boda ni Total Fairule.
Imagine ile Nguvu ingeenda viwandani.
 
Boda boda sio sifa ni uchafu na umasikini mkubwa. Hatuwezi kama nchi kutegemea usafiri kwa madereva holela wa pikipiki ambao hawafuati sheria, pikipiki hazijatengenezwa kwa lengo la kubebea watu.

Vijana wanaendesha bila leseni. Boda bora zinatakiwa ziruhusiwe vijijini tu na kwa mijini ziruhusiwe tu kwa safari binafsi na kuwe na sehemu maalumu kwa maiskeli na pikipiki kama nchi nyingine. Hatuwezi kuendeleza vitu kisiasa tu vijana watafutiwe ajira na tuweke katiba bora ilete uwekezaji.
Wewe umewapa ajira ngapi hao vijana
Au kazi kupiga domo hapa
Boda zizuiliwe utalisha familia za hao vijana
 
Nilikwenda South Africa hakuna Huo Upumbavu.

Boda boda ni Total Fairule.
Imagine ile Nguvu ingeenda viwandani.
Hivo viwanda mnavyo sasa??
Wewe umetengeneza viwanda vingap ukaajiri vijana?
 
Et boda boda sio kaz mbona mpaka kwenye inchi zilizoendelea zipo hizo boda boda
 
Bodaboda ziondolewe ndo nikapande mwendokasi au ??

Tatizo la baadhi ya bodaboda na wanaoharibu taswira ya kazi hiyo ni wale wapiga kelele, wezi, wasiofuata sheria za barabarani, na kujifanyisha ukichaa mnapotofautiana mtu mwenye gari na mtu wa bodaboda

Bodaboda ni usafiri wa haraka kidogo ukilinganisha na usafiri mwingine km daladala au hizi Rapid transit

Nadhani sheria ziboreshwe kwa wote waliopo huko na wanaotarajiwa kuingia huko ili kulinda maslahi yao binafsi, ya abiria wengine barabarani pamoja na usalama wa vyombo vyote vya moto.

NB bodaboda smart bado wapo na nikikutana na ambaye sio ntamuelkeza mpk aingie kwenye line
 
Sheria itungwe boda iwe ni kubeba mizigo na kufanya delivery tu.
 
Tuwahurumieni Hawa ndugu zetu boda, Ajira hamna, fursa za biashara sio rahisi kiivo, Cha msingi ni kufuata Sheria barabarani.
Xboda hapa.
 
Hali ni mbaya kwa kweli siku hizi ukitembea barabarani unaweza kupita kwenye zebra ukakuta magari yamesimama lakini cha kushangaza pikipiki hazijali zenyewe zinapita bila mpangilio na zimekuwa chanzo kikuu cha ajali na vilema wapya, wa kulaumiwa ni serikali iliyoshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa ajira hali inayopelekea vijana wengi hasa wavuta bangi na wahuni kugeukia pikipiki kama sources ya ajira, pikipiki zimejaa kama njugu
 
Nyie mnaosema bodaboda ziondolewe mmetengeneza ajira ngapi hadi sasa? Kuna viwanda mmejenga tayari ili kutoa hizo ajira? Acheni upuuzi. Wengi wenu ndo mkipata hela mnanunua Magari ya kifahari badala ya kuanzisha miradi itakayowasaidia vijana kupata ajira. Mmejaa unafiki sana.
 
Ukiachilia mbali kero ya uendeshaji wao, pia Kelele..

Mie naona Askari wa barabarani wameshindwa kazi yao..
Napendekeza ushuru uongezwe kwenye hizi bodaboda, iundwe kodi maalum kwa bodaboda.

Mbili, Bima iwe ya lazima ili awe bodaboda lazima awe na bima ya afya na ya chombo chake.

Tatu, mjini isikanyage.. akiingia na kukamatwa awe wa mfano, ikiwemo kutaifisha hiyo pikipiki.

Uzembe wa ajali za kugonga mtembea kwa miguu, ni kumfunga jela miezi 6+ na viboko 50 kila wiki.

Vishandu, hawa ndio wezi na wasumbufu.
Kuna operation iliendeshwa kipindi fulani, miili ilikuw inapelekwa monchwari ndg mkafate mzike.
Acha upumbavu. Hamia Burundi ukatoe haya maoni yako ya kishenzi.
 
unajua byke zimeua na kuzalisha vilema wangapi
Sheria iwekwe sharti dereva boda boda uwe kuanzia miaka 50, ni kazi isiyotumia nguvu wala akili
Vijana wafanye uzalishaji, nishati ujana inapotelea juu ya siti ya bodaboda mnakuja kusifia ujinga ujinga tu hapa
Kuongea ni rahisi sana. Hizo kazi za uzalishaji umetengeneza ngapi kwa uwezo wako?
 
Back
Top Bottom