Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Ni mwaka wa 2018, ulimwengu ulizizima kwa uzinduzi wa filamu ya Black Panther, kazi ya Marvel Studios iliyoongozwa na Ryan Coogler. Kwa wengi, ilionekana kama ushindi wa uwakilishi wa Waafrika na Wamarekani Weusi kwenye sanaa ya Hollywood. Watu walifurika sana kwenye kumbi za cinema kutazama filamu hii.
kumbi kama Nyali Cinemax, Cinema Multisala Fiamma, AMC- KAFD Riyadh. Lakini kwa macho ya wachambuzi wa historia, wanaharakati wa haki za watu weusi na watafiti wa historia ya siasa, filamu hii ilikuwa zaidi ya burudani—ilikuwa kifuniko cha kufuta na kupotosha historia halisi ya Harakati ya Black Power, hasa chama cha Black Panther Party for Self-Defense.
Hadithi Mbili Zenye Jina Moja, Zenye Taswira Tofauti.
Black Panther wa Marvel alizaliwa mnamo mwaka wa 1966, ndani ya kurasa za mfululizo wa comics za Fantastic Four #52, akiwa ni mfalme wa taifa la kufikirika la Wakanda. Kwa bahati (au makusudi), mwaka huo huo, Huey Newton akiwa na Bobby Seale ndio waliasisi chama cha Black Panther Party for Self-Defense huko Oakland, California.
Tofauti na Wakanda ya kubuni, Black Panther Party ilikuwa ni harakati halisi iliyolenga kukabiliana na ukatili wa polisi, ubaguzi wa rangi na kimfumo, ukosefu wa ajira, na huduma duni za kijamii kwa watu Weusi nchini Marekani. Kupitia mpango wao maarufu wa 10-Point Program, waliweka wazi madai yao ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Hii hakuwa ni hadithi ya mfalme wa kifalme mwenye teknolojia ya ajabu, bali ya vijana wa mtaa waliojizatiti kulinda jamii zao dhidi ya mfumo dhalimu wa watu weupe.
Katika karne ya 21, filamu ya Black Panther iliwasilishwa kama ishara ya “empowerment” ya Waafrika na watu Weusi duniani, kitu ambacho sio kweli. Wachambuzi kama Jared Ball, mwandishi wa kitabu cha “The Myth and Propaganda of Black Buying Power”, pamoja na Dr. Keeanga-Yamahtta Taylor, mwandishi wa “From #BlackLivesMatter to Black Liberation”, wanapingana na fikra hii.
Watalaamu hawa wanasema kuwa filamu hizi hazina lengo la kweli la kuhamasisha ukombozi wa watu Weusi, bali zinasaidia kueneza simulizi za hadithi ambazo hazina msingi wa mapambano halisi ya kihistoria.
Wakati Black Panther Party walikuwa wanapinga waziwazi ubepari na walikuwa wakihubiri mapinduzi ya watu waliokandamizwa, filamu ya Marvel inamvisha Black Panther “T’Challa” sifa za kifalme, utii kwa taasisi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa, na kukataa mapinduzi ya kweli kama ilivyopendekezwa na Erik Killmonger, ambaye alionekana kama “muasi” ndani ya filamu—wakati kwa wengi, alisimamia hoja halali za ukombozi wa watu wa Afrika waliotawaliwa.
Yaani unakataza kushare teknolojia yako na nchi za Afrika ambazo umejificha na unakwena kuwapatia teknolojia hiyo UN?! Wakanda walikuwa wana teknolojia ya hali ya juu ya matibabu, waliweza kumtibu Agent Everett Ross uti wa mgongo ndani ya masaa 24 pekee, ila hawakuweza kutengeneza tiba kwa ajili ya waafrika wenzao ambao wanaishi nao kwenye bara moja? Magonjwa kama Pneumonia, UKIMWI, Malaria, Kifua Kikuu, Saratani na kadhalika.
Mtu pekee ambaye alionekana kuwa anataka kuisaidia Afrika kwa mtazamo wake alikuwa ni Erik Killmonger ambaye jambo la kuiweka Wakanda iwe siri alikuwa kinyume nalo.
Ni jambo la kushangaza kuona jinsi taswira ya Black Panther Party imepotoshwa na kugeuzwa kuwa bidhaa ya burudani. Badala ya kujadili mafanikio yao ya kihistoria kama huduma za afya bure, shule zenye kutoa elimu bora, au mpango wa chakula kwa watoto (Breakfast Program), vijana wa kizazi kipya wanavutiwa na Wakanda na madini ya vibranium—vitu vya kubuni visivyowahi kuwepo.
Kwa mujibu wa Yohuru Williams katika kitabu chake “Rethinking the Black Power Movement”, hili ni suala la “cultural erasure”—kusahaulisha kwa makusudi historia ya mapambano halisi ili nafasi hiyo ichukuliwe na hadithi za uwongo zinazoonekana ‘salama’ na zisizotishia mfumo uliopo. Hakuna mapambano wala historia yoyote ambayo kijana anaweza kujifunza kupitia filamu hii zaidi ya burudani.
Filamu ya Black Panther haikuwa na lengo la kweli la kuendeleza harakati za Black Power wala ukombozi wowote wa mwafrika hata kidogo. Badala yake, ilisaidia kufunika historia ya mapambano, kuchukua jina la kiharakati, na kuigeuza kuwa bidhaa ya burudani isiyo na madhara kwa mfumo wa kikoloni wa kisasa. Kama jamii ya Waafrika na watu wenye asili ya Afrika, ni muhimu tusome vitabu kama “Seize the Time” cha Bobby Seale na “Revolutionary Suicide” cha Huey Newton ili kuelewa tofauti kati ya sinema na historia halisi ya ukombozi.
Ni wakati wa kujifunza historia yetu kutoka kwa vyanzo halisi—si kutoka kwa Marvel Studios, Walt Disney Studios, Warner Bros., Paramount, Universal Pictures wala Sony Pictures. Historia ya mababu na mabibi zako ikiandikwa na anayekunyanyasa fahamu tu ukweli kuhusu maisha ya wazee wako utapindishwa kwa sehemu kubwa sana.
Kumbuka kuwa, historia ya Alfred the Great wa Uingereza na maisha yake enzi hizo Uingereza ikiwa na Northumbria, Mercia, Wessex, Sussex, Kent, Essex pamoja na East Anglia imeandikwa na waingereza wenyewe, watu kama Bede the Venerable, William of Malmesbury, pamoja na **Matthew Paris.
Hata historia za ukoo wa kifalme wa Tudor imeandikwa na watu kama Raphael Holinshed, William Camden. Kwa sasa watu ambao wanaweza kukusimulia historia ya Uingereza kwa undani tena wakiwa wanajivunia ni Antonia Fraser pamoja na Alison Weir sio mwafrika wala mtu mweusi.
Je tujiulize historia ya Waafrika kwanini waandishi wengi sio waafrika? Leo Africanus, Mungo Park, David Livingstone, Heinrich Barth, Frank Lugard, Basil Davidson, pamoja na Roland Oliver. Kuandika historia ya Afrika wala sio kitu kibaya ila Eurocentric bias haijawahi kuisaidia historia ya mwafrika hata sekunde moja.
Je unadhani kuna muingereza ambaye anaweza kumuelezea vyema Shaka Zulu zaidi ya Steve Biko? Je kuna mtu kutoka Ufaransa ambaye anaweza kufafanua harakati za Mansa Musa kuzidi kalamu za Amadou Hampate Ba? Ama kuzidi Massa Makan Diabate? Yambo Ouologuem? Doumbi Fakoly?
Ukipata kukutana na Catalan Atlas ya mwaka 1375 ambayo ilitengenezwa na wazungu, walimjumuisha Mansa Musa ila sio tena kama mtu ambaye ni tajiri kupita maelezo na sio mfalme bali amekaa tu kwenye kiti chake akiwa na kofia ya kifalme ya dhahabu na fimbo yake.
Bwana Mkubwa, Shaka Zulu kwa kalamu za wazungu anaonekana kama mtu katili sana na mwenye kupenda kutumia nguvu za giza wakati wa vita, sio maneno yangu bali ni kazi ambazo zimeandikwa na watu kama Nathaniel Isaacs pamoja na mwenzake Henry Fynn, ila ukisoma visasili na hadithi za Wazulu utaona kuwa Shaka** hakuwahi kuwa mchawi wala mtu katili.
Ukisoma Izimbongi utaona huyu mwamba alikuwa na roho sawa Genghis Khan na wote ni makamanda wa vita haswa, mpaka leo Mongolia wanaimba sifa za Genghis Khan kwa kujivunia sana ila Afrika hakuna ambaye anamtazama Shaka Zulu kama kamanda.
KAZI KWETU WAAFRIKA TUTAZAME KWA UMAKINI TUNACHOLISHWA KWENYE LUNINGA.