Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

What about walalahoi ambao wamekuwa wakipigia kelele kuhusu suala la rushwa mahakamani? Wao si mashujaa. Katokea mtoto wa Mkubwa na kulisema lile lile ambalo walahoi wamekuwa wakilisema, all of sudden,anaitwa shujaa. Intersting!
 
Japo ni mtetezi wa kufuata sheria, lakini nafikiri sasa wakati umefika wa kutumia kila njia hata kama ni kurusha makonde kupambana na hawa wanaotuibia haki zetu.

Inabidi ifike mahali Watanzania na hasa wasomi tukatae kunyanyaswa kwenye nchi yetu.

Kama wakili Karume aliendesha hayo mapambano kwa misingi hiyo, mimi namuunga mkono kabisa. Wakati umefika wa kuwaambia hawa
majuha wanaotumia vyeo vyao serikali kunynyasa wananchi kwamba NO, hata sisi tumesoma na hatutaki upuuzi wenu.
 
Serikali yamuunga mkono mtoto wa Karume
*Yasema kitendo alichofanya Mahakama ya Kisutu ni cha ujasiri

*Yawataka mawakili kuiga mfano wake ili kumaliza rushwa

Na Muhibu Said

SERIKALI imekiri kwamba, vitendo vya rushwa vimekithiri katika mahakama nchini na kumuunga mkono mtoto wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Wakili Fatuma Karume kwa kitendo chake cha kuituhumu hadharani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kuwa imekithiri kwa rushwa.

Kauli hiyo ya serikali ambayo ni ya kwanza kutolewa, ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, alipozungumza na waandishi wa habari, Ikulu, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema ni jambo lisilopingika kuwa rushwa imekithiri katika mahakama nchini na kwamba, hatua ya Karume ambaye ni wakili wa kujitegemea ya kufichua uwapo wa rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ni ya kijasiri na inapaswa kuigwa na mawakili wengine ili kutokomeza rushwa hapa nchini.

"Rushwa katika mahakama imekithiri, Wakili Karume anastahili kupongezwa kwa kufichua rushwa pale Kisutu. Yule ni jasiri sana. Tungepata mawakili jasiri kama yeye rushwa ingepungua pale mahakamani hapo," alisema Marmo.

Wakili Karume alitoa tuhuma hizo siku chache baada ya kumtolea maneno makali Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Addy Lyamuya na kusababisha hakimu huyo kujitoa kusikiliza kesi ya madai ya ndoa namba 60 ya mwaka 2006.

Sakata hilo lilitokea katika mahakakama hiyo mwezi uliopita, baada ya Hakimu Lyamuya na wakili Karume kutofautiana tarehe ya kuanza kusikiliza shauri hilo la ndoa kati ya Sadick Ahmed Walji na Saeeda Hassam ambao wanagombania mtoto.

Tofauti hiyo ya kupanga tarehe ya kusilizwa kwa kesi hiyo, ilisababisha Wakili Karume kufoka na kumtolea maneno makali Hakimu Lyamuya.

Karume alimwambia Hakimu Lyamuya kuwa: �Wewe umeniona mimi kwa mara ya kwanza, hunijui mimi ni nani, nitakuonyesha na nitaandika barua kwa wakuu wako wa kazi, sijui kwa nini wamekuweka hapo wakati hujui kazi.�

Mara baada ya Karume kutoa maneno hayo, Hakimu Lyamuya alijitoa kusikiliza kesi hiyo ili kupisha mahakimu wenye nafasi za tarehe anayoitaka Karume kuendelea kusikiliza shauri hilo.

Hata hivyo, baada ya Hakimu Lyamuya kujitoa kusikiliza shauri hilo, Wakili Karume alikuja juu na kumnyooshea kidole Lyamuya huku akiendelea kutoa maneno mengine makali na kumshangaza hakimu huyo.

Wakati Lyamuya akiendelea kumshangaa wakili huyo, aliinua mikono yake juu jambo ambalo Wakili Karume alilitafsiri kuwa kunyoosha mikono juu kinaashiria yeye kuwa ni 'chizi'.

Siku chache baadaye, Hakimu Lyamuya aliwasilisha malalamiko katika Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) dhidi ya wakili huyo kwa kumfokea mahakamani na kumtolea lugha ya vitisho.

TLS ilithibitisha kupokea malalamiko dhidi ya wakili huyo na kwamba chama kinajukumu la kumtetea au kumuadhibu mwanachama endapo atabainika kukiuka maadili ya taaluma hiyo.

Alisema tatizo la rushwa ni kubwa na kwamba pamoja na serikali kuweka misingi muhimu ya kupambana na tatizo hilo, kazi ya kupambana na tatizo hilo bado ni kubwa.

Alisema utekelezaji wa NACSAP ulikumbana na changamoto kadhaa, ikiwa upungufu wa watumishi, hasa wenye uwezo na utaalamu wa kusimamia michakato inayohusiana na kudhibiti rushwa katika jamii na udhaifu wa vyombo vya kusimamia utawala bora nchini.

Vyombo hivyo, alivitaja kuwa ni pamoja na Kitengo cha Utawala Bora (GGCU), Takukuru, Sekretarieti ya Maadili, National Audit Office, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA).

Alisema changamoto nyingine, ni ushiriki mdogo wa jamii ya Watanzania katika vita dhidi ya rushwa na wanachi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu rushwa.

Hata hivyo, Waziri Marmo alisema serikali imeupitia upya mpango wake wa kutekeleza mkakati huo na kwamba sehemu kubwa ya mwaka wa fedha wa 2006/2007, ilitumika kwa kazi ya marekebisho na kuandaa mpango mpya utakaotekelezwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2007/2010.

Alisema mkazo mkubwa katika utekelezaji wa NACSAP utakuwa kwenye mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupanua wigo mapambano dhidi ya rushwa, kuendeleas kuboresha na kuimarisha utoaji huduma kwa umma na kuimarisha taasisi na asasi zinazojishughulisha na rushwa na utawala bora.

Mengine ni kuboresha na kuimarisha mifumo ya sheria na mahakama, kusaidia, kushirikisha na kuendeleza sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, vyama vya hiari na vyombo vya habari ili kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya rushwa, kuendeleza jitihada za kupambana na rushwa na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu rushwa.

Marmo alisema Tanzania imshatia saini na kuridhia mikataba muhimu ya kimataifa iliyoanzishwa kwa madhumuni ya kupambana na rushwa.

"Mikataba hii ni muhimu sana katika vita dhidi ya rushwa na itaisaidia Tanzania katika kuboresha mbinu zake na kuiwezesha nchi kushirikiana na mataifa mengine katika mapambano hayo," alisema Marmo.

Alisema mwaka huu, serikali imedhihirisha dhamiria yake ya kuendelea kutekeleza mkakati wake dhidi ya rushwa kwa nguvu na kasi zaidi kwa kutoa kibali kwa Takukuru kuendesha utafiti maarufu kama "National Governance and Corruption Survey", kupitisha Sheria mpya ya kuzuia na kupambana na rushwa ya Aprili 2007.

Pia kujadili kwa kina na kwa mapana ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Mahesabu ya Serikali (CAG) ya mwaka wa fedha wa 2005/06 na kuweka utaratibu wa kufuatilia utekelezaji na ushauri wa CAG.

Waziri Marmo alisema pamoja na hayo, serikali inatarajia pia kutunga sheria muhimu kwa utekelezaji wa matakwa ya NCSAP.

Katika hatua nyingine, serikali ya awamu ya nne, imeanzisha utaratibu mpya kwa kuwapangia mawaziri wote ratiba ya kuwasiliana na umma kupitia vyombo vya habari kila siku.

Utaratibu huo ulitangazwa na Waziri Marmo na kusisitiza kwamba uamuzi huo umefikiwa na serikali ili kuupa fursa umma kufahamu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya serikali katika kuliletea taifa maendeleo.

Utaratibu huo mpya, ulianza kutekelezwa jana na Waziri Marmo kwa kuelezea umuhimu wa dhana nzima ya utawala bora nchini.

Waziri Marmo alisema katika utaratibu huo mpya, waziri anayehusika na ratiba ya siku inayohusika atakuwa akitoa taarifa za utekelezaji wa mipango hiyo katika wizara anayoiongoza.
 
Mimi nakubali kuwa suala la rushwa inabidi lipigwe vita kwa njia zozote zinazowezekana. Wasiwasi wangu ni kuwa matumizi kama haya, ya kuficha masuala mengine, yanapunguza makali ya vita yenyewe! Wakili Msomi alikuwa anapinga kupigwa tarehe kesi yake ( ninavyoelewa mimi) na si kuombwa rushwa. mimi ningemwelewa zaidi kama angemkataa hakimu mapema kwa msingi kuwa ni mla rushwa! Lakini maadam alikubali kuingia ulingoni, pamoja na personal issues alizokuwa nazo na mahakimu wa Kisutu, alitakiwa kuwa na decorum. Hatuwezi wote tukawavamia mahakimu mahakamani hata kama wametuudhi vipi! Njia za kumshughulikia zipo na kwa mtu mwenye nafasi yake ya kuweza kuchongea kwa wakubwa angeweza kuzitumia kikamilifu kuliko sisi wengine. sasa suala zito kama hili,linalowaumiza wanyonge wengi, linaonekana kama ni fig leaf!
 
Kwa hili, Mheshimiwa waziri anatangaza open season kwa mahakimu wote ( maana wote ni wala rushwa)! Akikupangia tarehe usiyoitaka wewe ni kumvaa tu! Na wale walio keko miaka nenda rudi waanze kurusha vinyesi( samahani kwa kutumia kifaransa)? Nao tutawaita mashujaa? Hatutafika kwa mwendo huu!
 
Tungepata mawakili wengi wa aina hii mahakimu wasingethubutu kuomba rushwa.Ujasiri aliounesha na kupambana na uoza nadni ya Mahakama ni jambo la kuungwa mkono hata kama ni mtoto wa Karume,maana wengine naona wanadhani ameweza kufanya hivo kwa sababu tu ni binti ya Karume.
 
Waziri Mkuu mstaafu Warioba alisema mahakama zimejaa rushwa. Jaji Mkuu mstaafu Samatta alisema tatizo la rushwa mahakamani limemkosesha usingizi! Leo Wakili Msomi Karume amesema, anaonekana shujaa! Tunamwona mkombozi wetu sisi wanyonge, maana sasa wala rushwa wote wa mahakamani watashika adabu! Angekuwa mtetezi wa hao wanyonge, kesi ngapi anazifanya pro bono? Tatizo ni vitendo alivyovifanya mahakama ambavyo haviendani na heshima ya mahali pale! Kwa hili ndio anatakiwa kutetewa na/au kuhukumiwa na si kwa hii smoke screen! Kama ilivyowahi kuulizwa, sasa amewaumbua, itakuwaje? Au mwenzetu alitazamia kwa vile kapeleka "ushahidi" PCB, basi mahakimu wote Kisutu wangekamatwa na kufungwa? Mbona tunaambiwa kila siku kuwa ni lazima uchunguzi ufanyike kabla ya mtu kufunguliwa mashtaka. Asituzuge wenzake!
Ninacho Jifunza humu ndani specifically ktk hoja hii ni watu wengine kutaka kumuhukumu huyu Binti just bcs ni mtoto wa Karume.

Kwa waumini wa Dini ya kiislamu watakumbuka kua MTUME MUHAMAD ALITUFUNDISHA NJIA ZA KUONDOA UOVU.
1;KUUKEMEA.
2;KUKAA KIMYA ( ila njia hii ni udhaifu wa imani)
3;KUONDOA KWA MIKONO YETU.
Binti karume alichfanya ni mafundisho ya dini yake na uzalendo wake kama mtanzania.ikumbukwe kua MEDIA ilicover hili tukio kama story ili wauze gazeti,inawezekana tukio kama hili lilishawahi kutokea lakini either halikuandikwa, au isha andikwa hatufahamu.

Fundi Mchundo,kumbuka Jamii inapochoka lazima watokee wakujitoa muhanga wat she DID is right kama unavosema alishapeleka ushahidi PCCB,na pia umewanukuu kina warioba kua kuna rushwa then wat ulitaka afanye?kuna msemo una sema AIM JUSTIFY THE MEANS. our aim is to fight coruption(illigal action)i was expecting watu wote wamuunge mkono kwa hili let her be.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
ZIDUMU FIKRA ZA MWALIMU NYERERE.
 
Hii Serikali yetu hi jamani..sasa huyo Marmo kinamuwasha nini kuingilia taratibu za kimahakama???!!! Kwa maneno yake hayo ina maana anakubali kuwa mahakimu ni wala rushwa (sababu Fatmu Karume kasema), lakini hawachukuliwi hatua yoyote.

Unanishangaza ndugu hapa,
Inaonyesha wewe ni kati ya watu wale wanao kataa ukweli hata kama it stares them in the face.
Wenyewe wameamua kutoka na kusifia yale amboyo wao wanashindwa kufanya kwa kuoneana haya wewe bado uko nao tu huko gizani,angalia watakuacha pekee yako wakija wote kwenye mwanga!
Please ,welcome to the world Tanzania inabadilika njoo nasi kwenye mwanga.
CHANGES ALWAYS STARTS WITH ONE PERSON,OTHERS FOLLOW.
Fatmah ameanza ni haki na wajibu wetu kufata mapambano yaliko uoga na haya iende.........!!!????

Oyee............Fatmah!!!!
 
Kwa hili, Mheshimiwa waziri anatangaza open season kwa mahakimu wote ( maana wote ni wala rushwa)! Akikupangia tarehe usiyoitaka wewe ni kumvaa tu! Na wale walio keko miaka nenda rudi waanze kurusha vinyesi( samahani kwa kutumia kifaransa)? Nao tutawaita mashujaa? Hatutafika kwa mwendo huu!

Natafuta neno zuri la kukuambia ili usihisi nakutukana ila silipati,
Wachanikuambie unasikitisha...!lkn ni haki yako kwenye hii forum kutoa yako maoni na hayo ni maoni yako!
i can not help to think,kama umetumwa vile........!
 
wewe unafikiri huyo hakimu taratibu hazijui kwanini hakuchukua hatua? eti alipigwa na butwaa ni kwa sababu haijawahi tokea na hakutegea she took her by suprise wamezoea kuabudiwa
pia yaliyosemwa ni kweli sasa unafikiri nini dhmira ilimsuta .Honera fatuma hata na sisi tutaanza kupambana nao kama si mahakamani nje ya mahakama ama sivyo wajirekebishe,
Elfu hamsini anesma ndogo wakati ni zaidi ya kima cha chiini cha mshahara .Sijawahi kuona maana hata muhimbili wanachukua 2000 tu manesi ,leo hakimu unyefunga mtu.wewe na nesi bora nani?mjirekebishe
 
Rais nae inabidi afuate mfano wa huyu binti kwani ameshatuambia kuwa anayo orodha ya wala rushwa ila anawapa muda wa kujirekebisha.

Ila kwa upande mwingine, hivi unafikiri haya mambo angefanya wakili mwingine wa kawaida angekuwa wapi saa hizi? lazima angewekwa ndani kwanza kwa kuidharau mahakama. Ila kwa vile ni mtoto wa Rais basi she is untouchable. Tanzania tuna safari ndefu sana kuelekea utawala wa sheria.
 
May be and may be NOT!

Positive thinking is always the best way to start solving difficulties
 
Rais nae inabidi afuate mfano wa huyu binti kwani ameshatuambia kuwa anayo orodha ya wala rushwa ila anawapa muda wa kujirekebisha.

Ila kwa upande mwingine, hivi unafikiri haya mambo angefanya wakili mwingine wa kawaida angekuwa wapi saa hizi? lazima angewekwa ndani kwanza kwa kuidharau mahakama. Ila kwa vile ni mtoto wa Rais basi she is untouchable. Tanzania tuna safari ndefu sana kuelekea utawala wa sheria.

Wala rushwa ni wabaya sana na kama Muungwana aliingia kwa gia kwamba atapambana nao hadi kuwa maliza na tukamuamini lakini leo anawakumbatia kwa kuwaachia muda eti wajirekebishe kwanza ametusaliti pili kama si kutusaliti basi orodha hiyo political hana hata jina la Karamagi na wenzake.
 
Natafuta neno zuri la kukuambia ili usihisi nakutukana ila silipati,
Wachanikuambie unasikitisha...!lkn ni haki yako kwenye hii forum kutoa yako maoni na hayo ni maoni yako!
i can not help to think,kama umetumwa vile........!

Samahani kama nimekukosea.Unaweza kunitukana tu hamna shida! Mimi naamini humu ndani tunabadilishana mawazo na kuangalia hoja ilio mbele yetu kutoka kila angle. Kuna wakati tunaweza kukubaliana na wakati kupingana! Sasa kwa vile sikubaliana na wewe, basi inakuwa nimetumwa? Nani basi anitume? Hao mahakimu wala rushwa? Ili iwaje? Hivi unaamini kweli ninachokisema mimi, Fundi, kita affect kwa njia yeyote maamuzi yatakayofanyika kuhusu suala hili?
Ninachokisema humu ndani ni kuwa hii hoja ya rushwa haijaniingia kichwani. Ni nani anaweza kupinga kuwa hakuna rushwa mahakamani? Hao wa Keko niliowazungumzia, kila kukicha wanalia kutotendewa haki na moja ya sababu kubwa wanazotoa ni rushwa. Na hiyo ya kutupa nilichokitaja wameishafanya! Wengine wamefikia hatua ya kujipaka mwili mzima! Nani asiyejua hayo? Ninachokataa ni mtu kutumia hii hoja ambayo inawaumiza wengi wanyonge na wasio na hatia katika hali inayoweza kui-dilute. Watu wametumikishwa kifungo kwa ajili ya kutokutoa rushwa. Ni tatizo lisilostahili kufanyiwa mzaha. Sasa huyu tunayemzungumzia (nakiri mimi simfahamu) inasemekana alifanya fujo baada ya kutoridhishwa na tarehe ya kusikilizwa kesi yake na si kinginecho,kutoka na hilo akamtishia ( inasemekana) hakimu na kusema kuwa hajui kazi yake (si kuwa amemdai rushwa) badala ya kujibu tuhuma hizi, anaingiza suala zito kama rushwa ndipo mimi nashindwa kumuelewa. Kwa kuliingiza suala la rushwa kwa jinsi alivyofanya kunalipunguzia makali yake. Hivi unaamini kweli kama wakili mwingine wa kawaida angefanya haya na kudai kuwa alifanya hivyo kutokana na kuombwa rushwa,tungemwita shujaa? Nitaungana nae kupiga vita rushwa kwa nguvu zangu zote lakini si kwa njia hii aliyoitumia.
 
Tatizo lenu nyinyi Watanzania ni wanafki, mnapenda kulalamika chini kwa chini, lakini anapotoke mtu mmoja kujalibu kwawawakilisha mnamuona mjinga.

Narudia tena kusema WAkili Fatma alifuata proses zote na PCCB hakuna walichokifanya.

Alipokwenda mahakamani siku ile hakuwa na nia ya kufanya fujo kwa kisingizio cha rushwa ila alipoona mahakimu wote wanapuuza kesi ya mteja wake kwa sababu tu amepeleka taarifa ya rushwa PCCB, hapo ndio akaamua kufichua yote ambayo PCCB walitakiwa wayafanyie kazi na hawakuyafanyia.

Watanzania tuamke.
 
Sawa Mkuu! Kwa nini basi badala ya kufanya "fujo" asiite press conference pale Maelezo au hata nje ya Mahakama na kuyaanika yote hadharani? Nia nzuri pengine alikuwa nayo, lakini njia aliyoitumia si sahihi! Kuna kitu kinaitwa professionalism lakni yeye kwa bahati hakuonyesha hiyo. Atetewe kwa kupigana na rushwa lakini si kwa kufanya fujo mahakamani. Wenyewe mawakili mna neno linaitwa precedent!
 
Mkuu,

Wao wanapofanya madudu mbona hawaangalii professionalism? Wa kulaumiwa ni PCCB. Laiti wangechukua hatua huyo mama asingelifikia hapo alipofikia.

Itabidi hata mimi sasa ninunue camera ya siri, kuna ujinga mwingi sana kwenye vyombo vya serikali.

Huyo hakimu mkuu wa Kisutu inabidi aachie ngazi, hiyo ndio professionalism, mkuu wako wa kazi akipoteza imani kwako unaachia ngazi, hasa kwa kazi kama ya hakimu mkazi.
 
Tukitaka kuijadili hii issue vizuri inabidi tusimuangalie huyu binti kama mtoto wa Rais Karume. Tuiangalie in a bigger picture. Tumuonen huyu binti kama wakili aliyefanya kile ambacho watanzania wengi hatuwezi: ujasiri wa kusema na kutenda yaliyopo moyoni mwako bila kujali wengine watakuonaje. Ningeelewa kwamba amependelewa kama hakimu angemchukulia hatua ya kisheria then hiyo hatua isitekelezewe au itenguliwe. Sasa hivi tunaposema angekuwa sio mtoto wa Rais asinge..inatoka wapi? mambo kama haya ndio yanakatisha tamaa watu wenye ujasiri katika nchi yetu.
 
Mkuu Kitila, nina uhakika kuwa mpaka hapo ulipo umeshawahi kuombwa rushwa kwa namna moja au nyingine, je ulifanya nini? Ulikuwa jasiri wa kupambana na aliyekuomba rushwa au ndio kama waliowengi ulikuwa mwoga ukatoa. Kama Rais wako anajiuma kuwashugulikia wala rushwa, mwanzangu na mimi utaanzia wapi? All you can do ni kusema hapa JF huku wenyewe wakiendelea kula nchi. Sikatai kuwa wanachi wasipige vita rushwa ila juhudi lazima zitoke juu ama sivyo tutabaki kupiga domo tu hapa bila ya chochote kufanyika.
 
Sawa Mkuu! Kwa nini basi badala ya kufanya "fujo" asiite press conference pale Maelezo au hata nje ya Mahakama na kuyaanika yote hadharani? Nia nzuri pengine alikuwa nayo, lakini njia aliyoitumia si sahihi! Kuna kitu kinaitwa professionalism lakni yeye kwa bahati hakuonyesha hiyo. Atetewe kwa kupigana na rushwa lakini si kwa kufanya fujo mahakamani. Wenyewe mawakili mna neno linaitwa precedent!

Nadhani wewe ndugu unachofikiri huyu binti alifanya hivyo cos yeye ni mtoto wa Rais ndio maana unangangania alifanya fujo.

Mimi, wewe na yule hakuna hata mmoja aliyekuwepo mahakamani, na aliyepeleka hiyo habari kwenye media na huyp hakimu anayedai alitaka kupigwa. sasa hapo unategemea habari itasema nini??? hata hao waandishi wa habari hawakuwepo zaidi ya kusimuliwa
 
Back
Top Bottom