Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

Binti wa Karume azua mtafaruku kortini Dar

Magistrates are not demi-gods! And in Tanzania, they are corrupt! Ripoti ya Warioba iliweka wazi kwamba hili ni tatizo kubwa, na pia alikiri baadaye kwamba halijafanyiwa kazi! Fatma Karume alichofanya ni kuchallenge the system. Naomba niulize mnaotetea kwamba alimvunjia heshima hakimu, heshima iko wapi kama anaomba rushwa?! Ni kama traffic police! Unafikiri ni mara ngapi polisi akitaka kusimamisha magari kwa visingizio, watu huwapuuza!? Nimeshuhudia kwa macho yangu mara nyingi tu madereva wanapita na kuwapuuza! Na si 'watoto wa vigogo' wanaofanya hivyo! Tumechoka kuogopana! Wao wanaotakiwa kuenforce the law hawafuati sheria, alafu wanategemea tuwaheshimu! No way!
Anika dada Fatma! Na utupe taarifa zaidi. Naomba mtu a-post article iliyotoka jana katika gazeti la majira.

Ndugu, Umesoma hii thread toka mwanzo au umesoma mwisho na kutoa hukumu?!? huyo hakimu aliefanyiwa "fujo" hakuwa amedai rushwa., ningeshauri in future usome thread nzima kabla ya kuuliza/kucomment.

Ushauri wa bure tu ndungu yangu mtanganyika/mdanganyika mwenzangu.
 
Lakini kwa sie walala hoi Binti Karume katuwakilishia kilio chetu ingawa ni kiaina, Dudu Rushwa linatamba kote na sio pale Kisutu tu, nenda mahakama za Kinondoni, Ilala etc mtindo ni huo wa Wakili kula na hakimu kupindisha Haki, kwa aki ya mun mie namkubali kuwa anawajua na ndio kiboko yao,fuatilieni kesi za watu wanavyozulumiwa inatia woga mahakama zimeoza, huko Polisi kumeozaaaa, mawakili wengi nao siku hizi wameozaaaa,basi alimuradi ni vurugu tupu
 
Kuna fununu kuwa huyu hakimu alimpigia simu mteja wa huyu Wakili Msomi wakutane Sea Cliff Hotel. Kisha huyu mteja akampigia Wakili Msomi kumweleza kwamba Hakimu kamtaka wakutane Sea Cliff Hotel, mteja kwa kuwa kisha ombwa sana rushwa na huyu hakimu akamweleza Wakili Msomi kwamba safari hii atamrekodi mazungumzo yake. Wakili msomi akamruhusu kufanya hivyo, baada ya kufika Sea Cliff inasemekana Hakimu katika mazungumzo yake alimtahadhalisha huyu mteja (mdai) kwamba aachane na kesi hiyo ya madai ya kutaka kuwa na mtoto yasije yakampata yaliyompata Babu Seya. Kwa hiyo kwa kuwa huyu mama alikuwa rekodedi kidogo taswira ya nini ilikuwa sababu ya kucharuka kwake tunaanza kuipata. Lakini je alikerwa ndiyo je alitakiwa kufanya nini badala ya kucharuka?
 
Kuna fununu kuwa huyu hakimu alimpigia simu mteja wa huyu Wakili Msomi wakutane Sea Cliff Hotel. Kisha huyu mteja akampigia Wakili Msomi kumweleza kwamba Hakimu kamtaka wakutane Sea Cliff Hotel, mteja kwa kuwa kisha ombwa sana rushwa na huyu hakimu akamweleza Wakili Msomi kwamba safari hii atamrekodi mazungumzo yake. Wakili msomi akamruhusu kufanya hivyo, baada ya kufika Sea Cliff inasemekana Hakimu katika mazungumzo yake alimtahadhalisha huyu mteja (mdai) kwamba aachane na kesi hiyo ya madai ya kutaka kuwa na mtoto yasije yakampata yaliyompata Babu Seya. Kwa hiyo kwa kuwa huyu mama alikuwa rekodedi kidogo taswira ya nini ilikuwa sababu ya kucharuka kwake tunaanza kuipata. Lakini je alikerwa ndiyo je alitakiwa kufanya nini badala ya kucharuka?[/QUOTE]

Hapa ndo shida ilipo.. kwamba naye anatafuta pa kutokea kwamba huko nyuma mteja wake aliombwa rushwa na hakimu ambaye siye huyu aliye muwakia!

Yeye wakili msomi anelewa sana kipi alitakiwa afanye kumuwajibisha ama kufukua uozo wa rushwa lakini si kujidharililisha ama kutumia ubabe wa kutaka atambuliwe na kuheshimiwa kama mtoto wa raisi ( eti unanjua mi ninani?)

Pia sidhani kama nia yake ni kufunua uozo ulioko mahakamani kwani haya aliyajua siku nyingi na ushahidi alikuwa nao.. kwanini hakufanya hivo siku zote mpaka asubili alipokamatwa na kosa la kukiuka miiko yake ya kazi nda anajifanya anafukua mabaya??

Well, anachosema kina ukweli lakini kwa namna alivo kianzisha inatia walakini kwamba anatafuta kujisafisha zaidi badala ya kutetea haki/ama kufichua uozo kama anavo dai yeye!
 
Nionavyo mimi huyu binti anaweza kukosa haki zake za muhimu. Kwa sababu inawezekana alifanya haya yote kwa ajili ya kutete haki za mteja wake na kukomesha rushwa, lakini itaonekana kuwa kafanya vile kwa sababu yeye ni mtoto wa Rais.

Kuwa kwake mtoto wa Rais kunamponza. Hayo yote angekuwa kafanya mtu kama mimi sijui kama watu wangejadili hivi.
 
Hatuwezi kukana kuwa huyu wakili msomi anatoka katika ukoo wenye nafasi kubwa katika jamii yetu. Ni mzigo ambao ni lazima aukubali. Yeye sio kama sisi. Pamoja na faida za kutoka katika koo hizi, kuna responsibility. Alitakiwa kuwa na "decorum", "maturity" na "professionalism" katika utendaji wa kazi yake, ili asionekana anatumia nafasi yake isivyotakiwa. Tusisahau kuwa huyu ni hakimu wa tatu kupangiwa kesi yake na wawili wa awali walijitoa baada ya yeye kutokuelewana nao. Ugomvi katika hili ulizuka baada ya hakimu kuonekana kutokubali tarehe ambazo wakili msomi alizipendekeza. Kitu ambacho kinampelekea mtu kumuamini Hakimu Mingi aliyejitoa baada ya wakili msomi kudai kuwa anaiendesha isivyopasa. Ni wazi kuwa wakili msomi ana access katika "corridors of power" ambazo watu wa kawaida hawana, na hii inatokana kwa kiasi kikubwa na ukoo aliotokea. Akikutishia atakuchongea inabidi umchukue serious maana anaweza kufanya kweli. Haya anayodai ya rushwa yangekuwa more "credible" kama angeyatamka kabla ya hii purukushani. Kwa kuyatoa sasa yanaonekana kama "smoke screen" ili kupoteza lengo. Mimi nadhani angeomba msamaha na kukubali adhabu yeyote ambayo mahakama itatoa kutokana na vitendo vilivyotokea. Hii itaonyesha maturity na kukataa kwake kupendelewa kutokana na nafasi yake. Kama anasingiziwa, atoe ushahidi na simulizi zinazopinga madai dhidi yake, hususan ,kufanya fujo n.k na sio kuingiza masuala mengine. Ataifanyia jamii ya kitanzania msaada mkubwa kama atalifuatilia suala la rushwa nje ya hili la fujo ili watu waweze kufocus kwenye hilo tu na si lingineyo. Akifanya hivyo, SOTE tutakuwa nyuma yake maana tutaamini anafanya hivyo kwa uchungu alionao na si kwa sababu ana "ulterior motives".
 
Aanze kwa kumsaidia baba yake aondoe rushwa maana baba yake anao uwezo!!
 
Unajua ni uoga ambao hauna kichwa wala miguu sasa kama hakimu anashindwa kumwadabisha mtu kisa mtoto wa mkubwa,si ata wananchi watakuzarau na kukuona hauko competent.
Alafu huyu mtoto wa kigogo analeta mambo ya kitoto mahakamani"samahani kwa ilo"nkimaanisha eti anadai hakimu alimwangalia kwa jicho baya alafu kwa mtzamo wa dharau.
Nashauri wamtie adabu tuu,naye izo tuhuma za rushwa anazodai azifuatilie ili mkondo wa sheria ushike hatamu.
since no one is above the law
 
Aanze kwa kumsaidia baba yake aondoe rushwa maana baba yake anao uwezo!!

Jamani samahanini ,ila nataka kujenga HOJA hapa!
Watanzania tukiendelea kuamini system inaweza kwenda bila ya kuulizwa tunakosea au kwa lugha nyepesi tukiendelea kuamini serikali na mifumo yake yote mitatu inaweza kuendesha nchi kama tusomewavyo kwenye vitabu vitakatifu pia tunakosea,'yaani kuamini kua(kutoa maisha ni dhambi)bila ya kuuliza kwanini ni dhambi?

Au kuamini "mtoto wa nyoka ni nyoka" pia tunakosea,mtoto wa nyoka si nyoka ila ni yai la nyoka.
U-nyoka anaupata kutokana na mazingila ya lile yai la nyoka kutotolewa na nyoka kumkuta mama yake anatabia za nyoka.Mimi binafsi naaamini yai la nyoka likitotolewa na Mjusi mtoto akitoka atakua na tabia za kimjusi mjusi.
Sasa kama hivyo ndivyo haka kabint kana haki yakutetea walalahoi hata kama baba yake anaruhusu rushwa huko Zenji,tujaribu kumpa support;wote tuwajua rushwa ipo kwenye hili
 
Jamani samahanini ,ila nataka kujenga HOJA hapa!
Watanzania tukiendelea kuamini systm inaweza kwenda bila ya kua quastioned tunakosea au kwa lugha nyepesi tukiendelea kuamini selikari na mifumo yake yote mitatu inaweza kuendesha nchi kama tusemewavyo kwenye vitabu vitakatifu pia tunakosea,'yaani kuamini kua(kutoa maisha ni zambi)bila ya kuuliza kwanini ni zambi?

Au kuamini "mtoto wa nyoka ni nyoka" pia tunakosea,mtoto wa nyoka si nyoka ila ni yai la nyoka.
Uonyoka anaupata kutokana na mazingila ya lile yai l;a nyoka kutotolewa na nyoka kumkuta mama yake anatabia za nyoka.Mimi binafsi naaamini yai la nyoka likitotolewa na Mjusi mtoto akitoka atakua na tabia za kimjusi mjusi.
Sasa kama hivyo ndivyo haka kabint kana haki yakutetea walalahoi hata kama baba yake ni anaruhusu rushwa huko Zenji,tujaribu kumpa support wote rtwajua rushwa ipo kwenye hili

Hakuna anaye sema asipewe sapoti kwenye kukemea rushwa kwa vile ni mtoto wa mkubwa

Hapana ndugu Matuta,

Hapa kinacho gomba ni kwamba asitake kutumia hii nafasi kuficha kosa lake la kukiuka miiko yake ya kazi. Awajibishwe kwa makosa yake bila kujali yeye ni nani.

baada ya hapo, kama ana nia ya kupambana na rushwa aipeleke katika mkondo unao kubalika. Hapo kila mmoja wetu atakubaliana naye na kumuunga si mkono tu bali hata miguu na kichwa! lakini kwa sasa alinywe kwanza alilo likoroga!
 
You have a point!
Lakini inaonyesha you are missing a big picture here.
Angalia tayari Kabint kameshaoonyesha na evedence ameshapeleka huku TAKUKURU a recorded conversationa ya Hakimu akiomba rushwa lkn hamana cha maana kilicho fanyika so far,Mbali ya yate na kwa kushangaza anatokea Boss wa mahakimu ana maka eti "Hakuna rushwa hapa mahakamani" anataka tuamini hilo
Please,msitufanye sisi watoto!
Ila wacha nikupe leads za kuanza kufikiri nini ought to be Bint Karume was thinking alipokua akifanya hilo;

1.Ufikiri kwamba baada ya kuona nini wale mahakimu walichokua wakikifanya,yaani kujitoa na kugomea kusikiliza case hiyo kwa muda mrefu Yeye kwa kufanya alicho fanya ange draw attention ya media kama ilivyo sasa!!!???

2.Kutokana na kitendo hicho,sasa wananchi pia wameingia kwenye mjadala,nasidhani yy hakujua matokeo ya hicho alichokua akikifanya.Lkn kutokana na Hakimu kua tayari corrupted alishindwa kuchukua hatua yoyote zaidi ya kudai alipigwa na butwaa kutishiwa kuambiwa hamjui yy nani!!!?

Tafadali jaribu kufikiri kwenye angle hii alafu tuendelee
 
Leo Waziri wa Utawala Bora Bw. Marmo amemtangaza Bi. Karume kuwa ni shujaa na ni mfano kuigwa katika kuumbua wala rushwa. Na akataka watu wengine wajitokeze kama kuiga mfano wake.
 
Leo Waziri wa Utawala Bora Bw. Marmo amemtangaza Bi. Karume kuwa ni shujaa na ni mfano kuigwa katika kuumbua wala rushwa. Na akataka watu wengine wajitokeze kama kuiga mfano wake.

Hapo ndipo ninaposema serikali hii imeoza kuliko zote tulizowahi kuwa nazo.
Waziri anasema ......"Karume kuwa ni shujaa na ni mfano kuigwa katika kuumbua wala rushwa". Na baada ya kufanya hivyo iweje tena?

Kwa hiyo dawa ya wala rushwa ni kwa wananchi kujitokeza kuwaumbua!

Naona sasa 'kuumbua' ndio imekuwa dawa, baada ya kufundishwa na ile 'list of shame' ya mafisadi waliyoitoa CHADEMA. Hata Rais kaingia huko huko kwa kutishia kuwataja viongozi waiba miembe!
 
Yawezekana kuwa ni kweli kabisa kuwa "Mahakama zetu zimekithiri kwa Rushwa",Lakini njia aliyoitumia Wakili Fatma Karume kuueleza Umma wa Watanzania kuwa kuna Rushwa Mahakamani sio SAHIHI,kama wakili kuna njia nyingi tu,za kuikosoa Mahakama na Watendaji wake!!!.Lakini sio kashfa na majigambo mahakamani.

Waziri Marmo(ambaye pia ni mwanasheria) sielewi amesukumwa na nini kutoa kauli hiyo ya kumpongeza Wakili Fatma.Hili Ongezeko la Migongano na misuguano ya Maamuzi linaifanya serikali pamoja na Idara Nyeti ya Mahakama kuonekana inaendeshwa na Wababaishaji.Viongozi wetu wanatakiwa kuwa makini kwenye utoaji wa Kauli na Misimamo yao!!.Viongozi wengi sasa hivi wamekuwa wanatoa kauli za kiushabiki na zenye Misimamo ya kisiasa.

Kauli hiyo ya Waziri Marmo ni wazi kwamba itapokewa kwa mitazamo Tofauti na jamii ya Watanzania.
 
Jamani, mi nilisema it's not an open shut case. Mimi nadhani tujiangalie sisi kama watanzania wote tuko kwenye boti moja. Whether you are rich or poor, influential or insignificant, tunabanana humuhumu. Sasa kama Fatma ambaye babake ni rais wa Zanzibar ameona kuna uozo katika jamii na kwamba kuna haja ya kuwaumbua wala rushwa, basi tujue ya kuwa na yeye ameona hili tatizo na kugundua niliyoyasema hapo juu.
This is our home! Leo unaweza kufikiri you have immunity lakini kumbe zero!
Mi nashukuru ya kuwa it was Fatma aliyefanyiwa visa and she took action! She was in a position to do that! Others are not! But the time has come kama mtu ametukingia kifua na sisi tuache woga. Sasa ndiyo wakati wa kujitokeza na kusema uozo uliopo katika mfumo mzima wa mahakama (justice system!). Na hata opposition inatakiwa ishikilie suala hili bango!
Look at Pakistan,mpaka Musharaf kaamua kumtimua jaji mkuu because he was INDEPENDENT! We need free thinkers!
 
"HONGERA SERIKALI B SASA TUNAANZA"
Ndugu wapendwa kum,nakumbuka katika ujumbe wangu tusiache kmhukumu dada yetu labda alikuwa na nia nzuri lakini ameshindwa jinsi ya kui represent,,huyu dada yetu kwangu mimi nampongeza pili namshukuru kwa kuwaonyesha MAMA NAGU NA MHESHIMIWA MWAPACHU kazi si kukaa tu maofisini waende wakajionee nini kinafanya=ika,,
NILITOA MFANO WA KAKA YANGU MMOJA ALIWAHI KUWA JAMBAZI WA KUTUPA TUKAJITAHIDI ATOKE BAADA YA HONGO SANA AKATOKA MATOKEO YAKE KAKIMBILIA MOSHI NA KWENDA KUUA PALE NBC,WASIO NA HATIA,,JE
1) NYIE MAHAKIMU MNAJUA MNACHOFANYA
2)KILA MTU AKIAMUA KUTOKA KWA HONGO JE MAJAMBAZI YATAISHA NDUGU ZANGUNI????
3)WALE WATUNZA MAFAILI MAMA NAGU NAOMBA UTUELEZE KUNA MATATIZO GANI MULE NDANI YANAYOTUHANGAISHA KIASI HICHO,,,???
4)JE NYIE MAHAKIMU MMESOMA ILI MNYANYASE WANANCHI AU MSAIDE WANANCHI,,MKIWA KAZINI TUNAOMBA MFANYE YALE YALIOWALETA HAPO MAHAKAMANI WATANZANIA HIVI SASA WAKO MACHO WANA=ZIJUA HAKI ZAO ANGALIENI MNACHOFANYA TUMECHOKA WANANCHI WAKAWAIDA SI LAZIMA MUUMBULIE NA WATOTO WA WAKUBWA JAMANI
NI HAYO TU NDUGUZANGU
 
Yawezekana kuwa ni kweli kabisa kuwa "Mahakama zetu zimekithiri kwa Rushwa",Lakini njia aliyoitumia Wakili Fatma Karume kuueleza Umma wa Watanzania kuwa kuna Rushwa Mahakamani sio SAHIHI,kama wakili kuna njia nyingi tu,za kuikosoa Mahakama na Watendaji wake!!!.Lakini sio kashfa na majigambo mahakamani.

Waziri Marmo(ambaye pia ni mwanasheria) sielewi amesukumwa na nini kutoa kauli hiyo ya kumpongeza Wakili Fatma.Hili Ongezeko la Migongano na misuguano ya Maamuzi linaifanya serikali pamoja na Idara Nyeti ya Mahakama kuonekana inaendeshwa na Wababaishaji.Viongozi wetu wanatakiwa kuwa makini kwenye utoaji wa Kauli na Misimamo yao!!.Viongozi wengi sasa hivi wamekuwa wanatoa kauli za kiushabiki na zenye Misimamo ya kisiasa.

Kauli hiyo ya Waziri Marmo ni wazi kwamba itapokewa kwa mitazamo Tofauti na jamii ya Watanzania.

Naomba nikujibu ndugu yangu, wakili Fatma hana kosa nionavyo mimi, yeye alifuata taratibu zote zinazotakiwa ikiwa ni kumfundisha mteja wake am- record huyu hakimu aliyekuwa anakula rushwa, baada ya hapo akawakilisha shutuma yake pamoja na vithibitisho vyake huko PCCB.... LAKINI HAKUNA KILICHOFANYIKA.

Yeye kama binadamu wa kawaida akakereka, na zaidi alipoona MAHAKIMU wote wanakuwa na matatizo ktk kusikiliza hiyo kesi.

mimi ninavyoona PCCB ipo pale kama ushahidi tu lakini RUSHWA Tanzania itaendelea kuwepo milele na milele, kizazi kwa kizazi.
 
This is a typical collision, of a class!, Majaji waliopita na kunena mtawakumbuka! Mwalimu and his class per se,ndio yaliyowapata- kwani walitaka kusema lakini hawakuwa na uwezo bali ;Woga,haswa!(woga wote)... au ilikuwa ni nia ya kulinda matakwa na kanuni za Uzalendo-(na ujiulize Uzalaendo wako umebobea wapi!).

Naamini sababu nyingi za binti kusurutishwa na ukiritimba kwenye mahakama hiyo sio ngeni. Lakini uzalendo wake unapatiwa kuwekwa katika kipauembele kwenye duara la kisiasa Tanzania; na hususani 'Siasa ya Nchi na Jamii'

Hata kama ni mtoto wa Karume- wajibu wake Kikatiba na desturi zingine zinazowakilisha, ina-maana,uwajibu huo unaandamana na hoja yake ambayo ni kukataa rushwa kwa namna yeyote sehemu yeyote,na mimi kwa maafikirio yango,-ni alishindwa kutoa rushwa!Sababu... Sababu ni kushindwa kuitoa rushwa hiyo au aliafikika na ukweli wa ukiritimba ambao kwa namna moja au nyingine umeji-changanya kwa kiasi, na 'Siasa za Ukiritimba(kujuana) Serikalini'.

Huyu binti amejikuta huko kwa nia zote , na nafikiri hoja yake ni nzito!
 
Leo Waziri wa Utawala Bora Bw. Marmo amemtangaza Bi. Karume kuwa ni shujaa na ni mfano kuigwa katika kuumbua wala rushwa. Na akataka watu wengine wajitokeze kama kuiga mfano wake.

Hii Serikali yetu hi jamani..sasa huyo Marmo kinamuwasha nini kuingilia taratibu za kimahakama???!!! Kwa maneno yake hayo ina maana anakubali kuwa mahakimu ni wala rushwa (sababu Fatmu Karume kasema), lakini hawachukuliwi hatua yoyote.
 
Waziri Mkuu mstaafu Warioba alisema mahakama zimejaa rushwa. Jaji Mkuu mstaafu Samatta alisema tatizo la rushwa mahakamani limemkosesha usingizi! Leo Wakili Msomi Karume amesema, anaonekana shujaa! Tunamwona mkombozi wetu sisi wanyonge, maana sasa wala rushwa wote wa mahakamani watashika adabu! Angekuwa mtetezi wa hao wanyonge, kesi ngapi anazifanya pro bono? Tatizo ni vitendo alivyovifanya mahakama ambavyo haviendani na heshima ya mahali pale! Kwa hili ndio anatakiwa kutetewa na/au kuhukumiwa na si kwa hii smoke screen! Kama ilivyowahi kuulizwa, sasa amewaumbua, itakuwaje? Au mwenzetu alitazamia kwa vile kapeleka "ushahidi" PCB, basi mahakimu wote Kisutu wangekamatwa na kufungwa? Mbona tunaambiwa kila siku kuwa ni lazima uchunguzi ufanyike kabla ya mtu kufunguliwa mashtaka. Asituzuge wenzake!
 
Back
Top Bottom