Wanajamvi, nimefanya utafiti wakina kuhusu huyu binti. Kisa cha kufanya utafiti huu ni baada ya kuona maelezo yanayotolewa humu jamvini kuhusu huyu yanafanana kabisa na binti aliyemsumbua sana rafiki yangu mwaka jana. Nimefikia hata hatua ya kuuliza huyo binti umbo lake likoje.
Binti huyu aliwahi kuishi nyumba ya familia ya rafiki yangu mwaka 2011. Ni binti mwembamba na mweusi. Jina alilotumia ni Amina. Na alisema ni mtoto yatima na ansoma Sekondari huko Songea. Rafiki yangu alimpeleka hadi nyumbani kwa mama yake Kigamboni. Akidhani anamsaidia mtoto yatima. Binafsi nimewahi kumkuta pale nyumbani kwa mama wa rafiki yangu na katika maelezo yake alisema kuna mtu yupo jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kumbaka.
Wanajamvi, huyu binti alileta sokomoko pale Kigamboni kwa mama wa rafiki yangu, na details zake zipo polisi kigamboni, central na polisi Chang'ombe.
Ni binti hatari. Ana mtoto mmoja na anamume. Kama siyo mumewe kujakutoa ushahidi mahakamani, basi rafiki yangu angefungwa.
Kosa alilofanya rafiki yangu ni kulala na huyo binti. Hivyo basi kwakuwa Kapuya kalala naye basi kazi kwake.
Pale central police anafahamika kwani alishamtapeli hata mama Salma Kikwete. Yaani, Kapuya ajitahidi ampeleke tu pale Central Police basi kesi itaisha.
Kwakuwa binti mwenyewe ni huyu, basi hili jambo tulipe muda tu ukweli utajulikana muda mfupi. Mwisho naomba vyombo vya kutetea haki za binadamu, visaidie baada ya ukweli ukiwa wazi, basi wafuatilie yule aliyefungwa kwa kosa la kumbaka huyu binti atakuwa alionewa tu. Jamani binti huyu ni hatari, mengi sikutaka yaweka wazi ili nisimvue nguo rafiki yangu. Ila ushahidi ukihitajika nipo tayari kumleta huyu aliyesumbuliwa na binti huyu tapeli.