At least ungetuambia kuwa huo utafiti umeufanya wapi, na kwa vipi. Habari za huyu binti zimeandikwa na kutangazwa kupiti Tanzania Daima.
1. Je, ulihojiana na waandishi wa Tanzania wa Tanzania Daima?
2. Huyu binti anasema kuwa alikuwa rafiki ya na alikuwa anasoma na mtoto wa aliyekuwa diwani sijui Sinza, na huyo ndiye aliyemtambulisha kwa Kapuya. Hadi sasa hatujasikia huyo aliyekuwa diwani akikanusha
3. Huyo binti anasema aliwahi kwenda polisi Oysterbay. Mbona utafiti wako haujahusisha maelezo toka kituo hicho.
Ndugu, naomba usicheze na watu wazima wenye akili zao... Kama kweli umeamua kufanya utafiti, basi fanya kitu kinachoeleweka ndipo ulete taarifa zako hapa... Mabinti aina za unaosema wamejaa mtaani maana hata mimi nilishakutana na binti kama huyo lakini yeye ni mweupe mfupi. Je, na mimi niseme tu kuwa huyo ndiye aliyebakwa na Kapuya?