Bima ya afya NHIF, suala hili lina faida lakini angalieni pia changamoto zake

Ivan Stepanov

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
4,903
15,994
Habari ya jioni wananzengo, polen kwa msongo wa mawazo wale ambao ikifika jumapili jioninkama hivi raha yote inaisha kwa kufahamu kuwa kesho asubuhi "THE CYCLE REPEATS".

Twende kwenye mada na kama kutakua na makosa ya kiuandishi naomba usikwazike, nisamehe bure, jaribu tu kujiongeza.

Haya sasa naanza:

Binafsi sijawahi kabisaa kuajiliwa serikalini. Hivyo sijawahi kuwa member wa moja kwa moja wa mfuko wa bima ya afya wa taifa (NHIF) licha ya kwamba nanufaika na huduma hii kupitia kwa wife ambaye yeye ni mtumishi wa umma.

Nashukuru Mungu sijawa nikipata changamoto za mara kwa mara za kiafya zinazoni lazimu ku attend hospitali mara kwa mara, na pindi inapotokea hivyo, namshukuru Mungu huwa inakua ni ishu za kawaida tuu ambazo nazi sort by cash.

Sasa juzi nikiwa mkoani, nikakumbana na ishu fulani na kwakwel mfukoni sikua vizuri hivyo ikanilazimu kwenda hospital kwa dharura maana niliyakanyaga mwanaume nikajichanganya usiku na asubh kumekucha nikajihisi siko sawa hivyo kukimbia haraka kujali afya.

Ugonjwa ni privacy, kama mtu anaamua kuto disclose kwa hiyari yake. Hii ni haki ya mgonjwa. Napoamua kwenda kumuona daktari hilo linabaki kuwa suala binafsi kama sijaamua kumshirikisha mtu.

Sasa juzi ile niko masijala hospitali namaliza tu kufungua file, nashangaa simu inaita, kuangalia ni Wife anapiga anauliza " vipi nini shida maana naona uko hospitali muda huu, una tatizo gani?"

Basi nikamjibu uongo na ukwel pale kwa kadiri nilivyomudu.
Why? Sikua tayari kumueleza tatizo nini huo ndio ukweli.

Sasa nikajiuliza imekuaje akajua hii taarifa, ndio nikakumbuka kuwa NHIF wamemtumia notification ya kadi yangu imetumika mahali fulan muda fulani kwa kuzingatia yeye ndio mnufaika wa mfuko na ni mwanachama hivyo hii kadi yangu ni one of derivatives ya kadi yake.

Hii maana yake hata watoto wetu wakifikia hatua ya kuwa teenegers maana yake waki attend hospital mama yao atajua (hili kwa watoto sio baya japo haiondoi ukwel kwamba privacy ya mgonjwa ni private matter).

Nikajiuliza pia, kupitia kadi yake maana yake akiamua kufuatilia hospitali yeye kama mlipaji wa makato ya NHIF lli kujua ni kipi hasa nilitibiwa maana yake anaweza akajua.

HIi ni maana yake nini sasa? Na kwenye hili ni kwamba incase yeye aki attend hospital mimi sitaweza kujua. Anyway hili sio tatizo. Ila tatizo kubwa la msingi ambalo ni muhimu kulitatua ni nyie kujaribu kutuma message hiyo kwa mtumiaji wa kadi husika.

Maana pale napoandikishwa kama mnufaika kwa member wenu, si mnachukua namba ya simu? So kwenye algorithm za system yenu fanyeni kujua kama status ya aliyetumia kadi ni mume au mtoto au mke. Kama ni mume msitume message kwa mke hata kama ndio mwanachama wenu. Na kama mwanachama wenu ni mwanaume, mkewe akitumia huduma msitume message kwa mumewe .

Hii itasaidia kuondoa baadhi ya changamoto zinazoepukika.

Ahsanteni.
 
Nadhani nia iliyokusudiwa sio hiyo ambayo umeifikiria, mkuu. Lengo lao ni kuhakikisha bima inatumika kwa mlengwa, ndio maana anapewa taarifa muhusika mkuu. Pia, inasaidia kujua kwa mfano mtoto amezidiwa, yupo chuoni hajakupa taarifa, then inakuwa rahisi kujua.
 
Habari ya jioni wananzengo, polen kwa msongo wa mawazo wale ambao ikifika jumapili jioninkama hivi raha yote inaisha kwa kufahamu kuwa kesho asubuhi "THE CYCLE REPEATS".

inazoepukika.

Ahsanteni.
Dependant anapotumia kadi lazima mwanachama atapewa notification.


Lengo lao bima ni kuzuia fraud.


Nadhani hofu yako, ni matibabu yako.


Hawatumi matibabu.


======

Wanatuma message Kama hii👇👇


Card# 40246754 Togosho Wankaba imetumika JUMAA MSAMARIA HEALTH CENTER 03/07/2023 09:28 AM Ref# 870323355198. Piga namba 199 iwapo hutambui muamala huu.
======

Na nyingine siku hizi zinaandika gharama ya matibabu uliyotumia.
 
Back
Top Bottom