Ufanisi wa Bima za NHIF Tanzania

Yusto Bitalio

New Member
Mar 18, 2024
2
4
Kwanza kabisa nianze kwa kuwapongeza watoa huduma za afya Tanzania, lakini kuna swala nimelishuhudia ambalo sidhani kama lipo sawa.

Binafsi nilipatwa tatizo la macho, nikaenda hospitali (ipo Dodoma) nikawa nimeonana na daktari kwa kutumia bima ya NHIF ambayo mimi ni mteja wao.

Nilionana na daktari lakini, akaniandikia dawa, cha kushangaza nilipewa dawa moja tu nyingine nikaambiwa ninunue kwa cash maana zile dawa kwa Bima hazitoki.

Baadaye nikaenda kuangalia list ya matibabu nikakuta nimeandikiwa nimetumia shilling 70,000 nikabaki nashangaa.

Naomba hili jambo lifanyiwe kazi maana tunaoumia ni sisi.
 
Back
Top Bottom