Bima ya Afya kwa wote ni neema kwa Watanzania wote

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
108

BIMA YA AFYA KWA WOTE NI NEEMA KWA WATANZANIA WOTE

Na Amosi Richard

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliwahi kusema “Ni kupitia bima ya afya kwa wote ndipo tutaweza kutoa matibabu kwa kila Mtanzania anayeishi ndani ya nchi yetu. Mfuko huu utahakikisha mtu anapata matibabu yote anayopaswa kupata, huu ni kama upatu ambao Watanzania wote tunakwenda kucheza upatu huo na kati yetu anayepatwa na shida, upatu huo unamsaidia,”. Hii ni dhamira njema ya Mhe. Rais kuhakikisha wananchi wote wanakua salama kwa kupata tiba za uhakika bila gharama wanapopatwa na maradhi.

Ni miaka mingi imepita tangu Tanzania ilipopata uhuru wake mwaka 1961 na mara baada ya kukabidhiwa rasmi uhuru wake Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitangaza maadui watatu wa Taifa ambao ni Ujinga, Umaskini na Maradhi, katika ya maadau wote hawa kuhusu elimu tunazo sababu lukuki za kujikweza kuwa nchi yetu imepiga hatua kubwa kupambana naye vilevile upande wa umaskini jitahada za kumkomboa mtanzania kiuchumi zinaendelea na zinaendelea kuzaa matunda. kwa upande wa Maradhi serikali imejitahidi kuwekeza katika Miundombuni ya afya na rasilimali watu ili kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa urahisi Tanzania nzima mijini na vijijini.

Katika kila mafanikio na hatua za maendeleo changamoto hazikosekani, Rais Samia kajitahidi sana na kufanya makubwa katika ujenzi wa Zahanati, Vituo Afya, na Hospitali karibu maeneo yote nchini, pia serikali imeboresha miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini kwa kuweka vifaa na vifaa tiba kwenye hospitali zetu nchini ambapo kwa sasa kuna mashine za kisasa za CT Scna. lakini wananchi wanapopata maradhi suala la gharana za matibabu limekua likiziweka afya zao mashakani kwa kushindwa kuzimudu gharama hizo.

Katika kulitafutia suala hili ufumbuzi Mhe. Rais Samia kupitia Wizara ya Afya amekuja na mfumo wa Bima ya Afya kwa wote ambao ni njia rafiki ambayo itawaneemesha Watanzania wote bila kujali hali ya vipato vyao. Na ikumbukwe kwamba Bima ya afya ni utaratibu wa kuchangiana ambapo mtu/kaya iliyopata wagonjwa na kutumia zaidi ya michango iliyotoa inachangiwa na mtu/kaya ambayo haijapata wagonjwa, mfumo huu ni mkombozi kwa Wtanzania walio wengi ambao kipato chao ni cha chini au wastani ambao hawawezi kumudu gharama za matibabu makubwa kwa sasa mfano mgonjwa wa figo kuchuja damu kwa siku ni shilingi 180,000 na mtu anatakiwa kufanya hivyo mara tatu kwa wiki swali la kujiuliza ni je kwa mwezi ni kiasi gani mtu huyo atapaswa kulipa? Na akikosa mtu wa kumbadilishia figo atapaswa kufanya hivyo kwa miaka yote kitu ambacho ni gharama kubwa na ni vigumu kwa mtu wa kawaida kumudu gharama hizi lakini kupitia mfumo huu wa bima ya afya kwa wote wale wote watakaojiunga sheria itakapopitishwa na kuanza kufanya kazi watanufaika kupata matibabu kwenye ngazi zote Kuanzia Zahanati hadi Hospitali ya Taifa na ukizingatia kiwango pendekezwa cha kuchangia kwa mtu mmoja ni kidogo na kinaweza kumpatia matibabu yote yanayoinishwa kwenye kitita.

Mfumo huu bima ya afya kwa wote ni mfumo rafiki sana kwa watanzania wote kwani kupitia sheria inayopendekezwa, mfumo wa bima ya afya nchini utajumuisha bima ya afya ya Umma na Binafsi. Sheria inayopendekezwa pia itaitambua NHIF kama Mfuko wa Bima ya Afya wa Umma ambayo itahudumia Watumishi wa Umma na wananchi wengine watakaochagua kujiunga na Mfuko huo. Aidha, Sheria pia inaruhusu kuwepo kwa Skimu binafsi za Bima ya Afya ambazo zitatoa huduma za Bima ya Afya kwa wananchi katika sekta rasmi binafsi na isiyo rasmi.

Jambo linalofurahisha na kutia moyo kwenye dhamira hii ya serikali ya awamua ya sita kuhusu bima ya afya kwa wote ni kwamba hata wananchi ambao hawana uwezo kabisa wa kujiunga na mfumo huu wa bima ya afya kwa wote kupitia Sheria inayopendekezwa, watakuwa na haki ya kupata huduma za matibabu kupitia utaratibu uliowekwa na Serikali baada ya kuwatambua kupitia mfumo wa utambuzi wa watu wasio na uwezo wa Serikali. Lakini pia kila mwanachi atakayejiunga na Bima ya Afya atakuwa na fursa ya kupata huduma za matibabu katika vituo vya huduma vilivyosajiliwa na Mfuko katika Mkoa wowote.

Mfumo huu wa Bima ya Afya kwa wote ni mfumo huru na haumfungi mwananchi kuchagua aina ya mfuko anaupenda kujiunga nao kwani sheria ya bima ya afya kwa wote itaweka fursa kwa baadhi ya makundi ya wananchi kuchagua kujiunga na skimu za Bima ya Afya kulingana na matakwa yao kwa kuzingatia miongozo itakayowekwa na skimu za bima ya afya zitakazokuwepo kwa mujibu wa sheria.

Wananchi tusidanganyike wala kuyumbishwa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati ambao kazi yao ni kupinga tu liwe jema au lenye madhaifu wao huwekeza kwenye kukataa na sio kutoa ushauri kwa serikali au kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu Bima ya afya kwa wote wengi wao hawayapendi maendeleo kwani ni mwiba upande wao. Mambo yenye maslahi na ahueni kwa wananchi lazima wananchi tuyabebe wenyewe bila kuhitaji propaganda za kisiasa zinazofanywa na watu wanoishi kupitia propanda hizo.

Neema hii ya kupata matibabu ya uhakika katika ngazi zote inatakiwa kwa umoja wetu tusimame na kumuunga mkono Rais Samia kwa kutoa mapendekezo yenye tija ambayo yatajenga na kuifanya sheria hii ya Bima ya afya kwa wote iwe rafiki na kila mwananchi ayafurahie matunda yake.

Waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Afya Mhe. Ummy Mwalimu (MB) kwenye sheria hii ya Bima ya Afya kwa wote anastahili kupongezwa kwani amejitahidi sana kutoa nafasi kubwa kwa wananchi kutoa maoni yao na ushauri kabla ya kwenda kuipitisha Neema hii kwa Watanzania wote.

Serikali ya awamu ya sita ipo makini hivyo kwa namna yeyote naamini itaweka utaratibu mzuri na rafiki wa kumuwezesha mwananchi wa kipato cha chini kuweza kuchangia fedha kiwango kitakachopangwa kwa awamu hadi akamilishe ili apatiwe bima yake na kuanza kunufaika pale anapopata maradhi. Hii itasaidia kila mmoja kuwekeza kidogo kidogo kwa kadri anavyopata fedha.

Mwisho watanzania ni vyema kujitambua na kuelewa kuwa ugonjwa hauna hodi na matibabu kwa pesa taslimu ni ghali sana nawasihi watanzania wenzangu tuelewe dhamira nzima ya Rais wetu katika dhana nzima ya Bima ya Afya kwa wote na tuiunge mkono sheria hii kwa manufaa yetu sote.​
 
Unazijuwa dharama za kulipa bima ya afya kwa family?

Hakika ni mzigo mkubwa kwa mwanaichi wa hali ya chini.
Kama mlo ni tatizo ,,hyo pesa ya kulipa bima ya family nzima itatoka wp?

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Hivi mtanzania wa kijijini familia imelima mwaka mzima wanapata mahindi kunia 5 tu hivi uyo baba na mama watatowa wapi 340000 za bima ? Kwa uchumi wetu hatujafikia huko na serikali imeona vijana wanawatibu wazazi wao na Bima zao ikiwa bima kwa wote hakuna Tena ndugu au mzazi kutumia bima ya mwanaye
 
Kampuni inataka pesa, kampuni inataka faida. Wacha tukamuliwe. Kwani hatua gani zimechukuliwa na wenye a/c yetu ya china?
 
wanafamilia sita shilingi 340,000/= kwa mwaka???

Kama familia ina watu 8 .maana yake iwe ni shilingi 680,000/= kwa mwaka?

Kwa Tanzania ipi? Hii hii ya Samia??
 
Back
Top Bottom