SoC01 Bima ya Afya bure kwa watoto Vijijini - Mapendekezo yangu

Stories of Change - 2021 Competition

Emmanuel Nelson

New Member
Jul 22, 2021
2
1
Kwa mujibu wa sheria zetu, mtoto ni mtu yoyote mwenye umri chini ya miaka 18. Bima ya afya ni mfumo unao muwezesha mtu kupata matibabu pasipo kuwa na fedha taslimu pindi apatapo ugonjwa fulani.

Mara kadhaa tumeshuhudia kwa kusikia, kuona ama kusoma kupitia vyombo mbalimbali vya habari/mitandao ya kijamii mzazi/wazazi wakiomba msaada toka kwa jamii ya wasamalia wema ili kuchangiwa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wao ambao hupatwa na maradhi/ magonjwa yatokanayo na sababu mbalimbali kama ajali au hata kuzaliwa nayo kutokana na kushidwa kumudu gharama husika.

Na pindi itokeapo kukosa msaada husika, hupelekea wengi wao kubaki kwenye lindi la umasikini kwani hujikuta wameuza mali(assets) kadha wa kadha katika kujaribu kumudu gharama za matibabu. Lakini pia wapo ambao hujikuta wapendwa wao wamebaki na ulemavu wa kudumu au hata kupoteza maisha na kuwaacha wazazi/ walezi wajibaki na huzuni na majonzi mioyoni mwao.

Hivyo basi kutokana na changamoto hiyo, ningeshauri serikali ianzishe utaratibu wa kutoa bima za afya bure kwa watoto vijijini ili kuwapunguzia jamii za vijijini umaskini na majonzi ya kuodokewa na wapendwa/watoto wao kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Hii inaweza ikafanyika kwa utaratibu maalum ambapo kila mzazi anayejifungulia kwenye zahanati/kituo cha afya awe anapewa kadi maalum pindi akabidhiwapo cheti cha kuzaliwa itakayomuwezesha mtoto husika kupatiwa matibabu bure mpaka afikishapo umri wa miaka 17.

Hii itasaidia sana kwanza wazazi wengi kujifungulia kwenye mifumo rasmi ya serikali na kuachana na ukunga wa jadi na hivyo serikali nao kuwa na takwimu rasmi za uzazi.

Pili, itasaidia kuongeza uzalishaji na kuwa na uhakika wa taifa lijalo lenye watu wenye afya kwa kuwa fedha na mali ambazo zingetumika kwenye matibabu zitatumika kwenye shughuli za uzalishaji maili kama kilimo na ufugaji.

Hili linaweza kutekelezeka kwa kuanzisha mfumo flani wa uchangiaji mfano kama inavyo fanyika sasa kwenye ununuzi wa umeme/luku ambapo huwa kuna makato flani hukatwa kwa ajili ya REA.

Lakini pia au hata kwa jamii yenyewe ya vijijini wanaweza kukawa na makato flani pindi wauzapo mazao yao kwa mfumo wa ghalani kwa ajili ya bima za afya kwa watoto wao kwani wao ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili ukilinganisha na jamii zilizoko mijini.

Nadhani kwa kufanya hayo tutajenga jamii za vijijini zenye afya bora na zenye kujisikia fahari ya taifa lao na kuwa "watanzania".
 
Back
Top Bottom