Serikali imetoa wito kwa Watanzania, Viongozi wa kisiasa, kidini na kimila kuungana na Serikali katika kuhamasisha umma kujiunga na Bima ya Afya

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
Na WAF - Dodoma

Serikali imetoa wito kwa Watanzania, Viongozi wa kisiasa, kidini na kimila kuungana na Serikali katika kuhamasisha umma kujiunga na Bima ya Afya kwa wote pale mchakato utakapoanza rasmi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu swali namba 56 kwa niaba ya Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu swali la Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas Mbunge wa Jimbo la Kinondoni aliyeuliza Je, nini kauli ya Serikali juu ya Bima ya Afya kwa Watoto?

Dkt. Mollel amesema kuwa nchini kuna watoto Milioni 31, milioni 1.5 wako kwenye mfumo wa Bima ya afya ya sasa na milioni 30.7 wako kwenye mifumo ya bima za afya nyingine zilizopo nchini.

“Niwahakikishie wananchi kuwa ujio wa bima ya afya kwa wote utakuwa suluhisho la changamoto ya matibabu kwa wananchi wote bila kujali hali ya kiuchumi na kikwazo cha fedha, hivyo naomba mchakato utakapoanza wananchi mjitokeze kujiunga na skimu za zitakazobainishwa ambazo zitakua kwa rika zote”. Ameeleza Dkt. Mollel.
 
Back
Top Bottom