Bilioni 11 za Rais Samia zamtetemesha RC Shinyanga, afanya maamuzi magumu

Eti raisi samia ameshapeleka fedha. Huu upuuzi ulianza awamu ya 5. Kwaninj usiseme wizara husika au serikali imepeleka
 
Halafu tukijenga majengo mabovu mnatukamata.

Hakuna jambo baya kama kutofuata sheria za manunuzi( PPA ).

Zimewekwa za nini? kama hamtaki tuzitumie?

Hasara za kutotumia sheria za manunuzi ni kubwa sana kuliko faida. Afisa manunuzi kaonewa bure tu, mchakato wa Tendering ni mkubwa sana mpaka kukamilika, Auditor akija ataangalia institutional arrangement pamoja na sheria zilizotumika, sasa kama akienda kinyume si kaa la moto tena.

Mnatukosea sana.
 
Hata kama ni dharura ni lazima watu wa procurements wafuate procurement procedures, hivi muende tuu kununua simenti, mabati, nondo etc kama unajenga nyumba yako si mtapigwa au hamuwajui vizuri maafisa manunuzi? Mfano kama hamjakubaliana kupata quotations ili muamue mtanunua kwa bei ipi si mtu ataenda kununua kwenye bei nafuu halafu makaratasi akaongeza cha juu?
Haraka haraka ya nini,kama ni kuchelewa,mtani umeshachelewa.Hizo fedha sio za mama Samia, ni kodi au mkopo kwa wananchi.Kuna mtu kasema acha kupotosha.Fedha ni za Watanzania.na sio zinagawanywa kwa hisani tu.Nadhani huyu mtani anadhani mama katoa kwenye pochi halafu akampa.

Shida sana, hawa wanasiasa ukimwambia atoe kwa maandishi kuamuru hizo fedha zitumike, utasubiri sana.Na ukimwambia mkuu, tunaomba idhini ya matumizi haya kwa maandishi tutumie kama supporting document,huwezi amini anakuwa mkali kuliko huyu mtani.Mara utasikia kwenye majukwaa huyu anakwamisha kazi,mara ananidharau,mara mimi ndiye rais wa mkoa huu nk.

Ok ikumbukwe,na ifahamike kuwa kuna kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za serikali kisheria zilizotungwa na bunge.Ni lazima maafisa ununuzi,wahasibu,wakurugenzi na wengine kuzifuata.Na zikifanyika kama anavyotaka huyu mtani wangu atawaruka hao wataalamu wakati Otto,Prof Asaad atakapohoji.(quere) hutaamini.Procurement prcedures zipo.Kwa nini anataka kupita short cut (Chunguzeni kuna kitu hapo).kuna mtu anatakiwa kupewa hiyo kazi bila kufuata utaratibu.PAC note down.

Hata zabuni hazijatangazwa ili kupata mkandarasi mtaalamu.Huyu mtani wangu anataka apewe billion 11 akanunue cement,mabati,matofali,
nondo nk.amesahau juzi tu mama mwenzake kwenye kamati ya PAC ilivyoibua matumizi mabaya ya fedha za serikali kwenye taasisi za serikali zikiwemo baadhi ya halimashauri.

Mimi nadhani nimshauri mtani wangu awaache wataalamu wafuate taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za serikali.Aache kuwatisha wataalamu.Wao ni wataalamu sio wanasiasa kama yeye, wamesoma na wameajiriwa kisheria,wala hawajateuliwa kwa hisani ya mtu kama yeye.

Ahsante wataalamu, simameni kwenye taaluma zenu.Akiwalazimisha aweke kwa maandishi.Jifunzeni kilichotokea kwa Yule Dc.Kwenye kutoa ushahidi alijitetea kuwa aliagizwa na ngazi za juu kwa mdomo bila document.Badala yake ona kichapo alichopata sasa.Be careful hawa wanasiasa sio watu hawa.Na yeye anataka ajulikane yupo.

Kwa nini asikae vikao vinavyojulika kiutendaji atangaze tenda,apatikane mzabuni halafu tuone kama wataalamu wangekataa kutoa fedha kwa maelekezo kutoka kwake.Wamemkatalia kwa sababu taratibu na kanuni za fedha hazijafuatwa.

Hoja za ukaguzi zikitokea wa kwanza kulaumu wataalamu hasa wahasibu na maafisa ugavi ni yeye.Na wa kujibu hoja hizo ni wahasibu na hao wataalamu wengine.Yeye anakaa mbali.Nina uzefu na hili.

Mara zote kazi za zimamoto kama anavyotaka mtani wangu ndio hapo zinapopigwa fedha za kutosha kisawasawa halafu anayeitwa kufungua anakataa kufungua kwa sababu hazifanani na b.11.

Nchi hii wengi wanafanya hivyo na kuvunja sheria halafu adhabu anabambikiziwa mtaalamu.Tufuate taratibu zilizopo kisheria na tusifanane na yule jaji wa ile kesi ya PGO.
 
Huyu Dada yuko smart sana kichwani

hapa naona Rais Samia amelamba

penyewe Shinyanga itasogea sana
Yupo smart kwa kiwango gani kiongozi anayetaka kuvunja taratibu za manunuzi akitaka akanunue yeye.Kama yeye ni smart afuate taratibu zote za manunuzi.Safar baaaado kabisa.
 
Huu pia ni ujinga, yaani jengo kama linatakiwa lijengwe miezi miwili nyie mtalazimisha eti kwa sababu ya deadline ya shule? Kama issue ni deadline ya kufungua shule je hilo mlikuwa hamlijui?
Mwisho watoto wanangukiwa na jengo wakiwa ndani.
 
Ofa ofa!!!!Naunganisha GB 72 kwa mwaka mzima kwa mtandao wa tigo kila mwez utapata GB 6 Ambazo unatumia siku 14 kila mwez kwa mwaka mzima
Free call tigo kwenda mitandao yote kwa miaka 2 kuungwa
Wanaohitaji njoo Pm
nahitaji watu walio seriously TU pm usije pm kunijaribu Kama maelezo hayajitoshelez niulizie hapa hapa
Karibuniikikupendeza pm
 
Mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Edward Mjema amefanya maamuzi magumu ya kumsimamisha kazi afisa manunuzi mzembe wa Wilaya ya Kishapu Ili kupisha Ujenzi wa madarasa kwa dharula kama ilivyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Kweli nimeamini sasa kuwa moja ya sifa ya kuteuliwa kuwa DC au RC ni kujua "kusoma na kuandika" tu basi ( Na si habari ya kufika sijui darasa la ngapi, diploma au degree kama wengine wanavyofikiri).

Ubabe wa RC katika utekelezaji wa zoezi la kujenga madarasa kwa staili ya zimamoto linakiuka sheria ya utumishi wa umma (kwa kumuathiri (victimize) Afisa Manunuzi). Agizo hili pia linakiuka sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA). Vilevile agizo linauweka uongozi mzima wa Wilaya husika na Mkoa anaoungoza kupata lawama mbaya na hati chafu juu ( wasubirie ripoti ya GAC ) haitawaacha salama.

Haya mabilioni kwa maneno mengine ni kama aina fulani ya upigaji kwa jina la madarasa. Mwisho wa siku tutashuhudia matokea ya hovyo na shida ya madarasa ikiwa bado iko palepale na fedha zimeyeyuka.

Let us wait and see...Uh!
 
Hii nchi ni kama vile imepata Uhuru Jana, yaani miaka 60 ya Uhuru bado tunapambana kujenga madarasa?? Wakati wa awamu ya tano tuliambiwa Kwa sasa nchi haina shida ya madarasa. Kumbe zilikuwa siasa Tu.
 
Mkuu laid down procedures za uendeshaji nchi ni pamoja na kugawa kazi kwa haki, na kulipa kwa haki, n bado kusudi lililo tazamiwa litekelezwe.
Hapo ni project planning na execution.
Soyo kwenda tu kununua sementi kwa Mangi.
Haiwezekani kufuata sheria katika kuliendea jambo la dharura. Lakini ikumbukwe kuwa Mh. Rais alishasema utekelezaji usicheleweshwe kwasababu ya masharti ya PPRA.
 
Hata kama ni dharura ni lazima watu wa procurements wafuate procurement procedures, hivi muende tuu kununua simenti, mabati, nondo etc kama unajenga nyumba yako si mtapigwa au hamuwajui vizuri maafisa manunuzi? Mfano kama hamjakubaliana kupata quotations ili muamue mtanunua kwa bei ipi si mtu ataenda kununua kwenye bei nafuu halafu makaratasi akaongeza cha juu?
Wacha tuone mwisho wa hadithi!
 
Haiwezekani kufuata sheria katika kuliendea jambo la dharura. Lakini ikumbukwe kuwa Mh. Rais alishasema utekelezaji usicheleweshwe kwasababu ya masharti ya PPRA.
Tatizo si tamko la mama Samia, tatizo ni jinsi tamko hilo linavyoweza kuwa blank cheque kwa wapigaji.
 
Back
Top Bottom