Bilioni 11 za Rais Samia zamtetemesha RC Shinyanga, afanya maamuzi magumu

" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 

TZS Bilioni 11 za Rais Samia Suluhu zamtetemesha RC Shinyanga Bi Sophia Edward Mjema, afanya maamuzi magumu Kishapu,​

" Hakuna kama Samia "​


Mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga Bi Sophia Edward Mjema amefanya maamuzi magumu ya kumsimamisha kazi afisa manunuzi mzembe wa Wilaya ya Kishapu Ili kupisha Ujenzi wa madarasa kwa dharula kama ilivyoelekezwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
====
Mkuu huyo wa Mkoa amemshangaa afisa huyo mzembe kwa kuendeleza urasimu kwenye fedha za Rais Samia zinazotaka madarasa yajengwe kila sehemu yanapohitajika kwa dharula ili ifikapo trh 06|01|2022 wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza waanze mwaka wa masomo maramoja kwa pamoja.
===
Mtakumbuka Rais Samia alitoa Jumla ya madarasa elfu 15 kwa shule za Sekondari na madarasa elfu 3 kwa Shule shikizi za msingi huku akitoa Jumla ya madawati 462,795 sawa na Wastani wa madawati 120 na madarasa 4 katika Kila shule ya Sekondari ya Serikali nchi nzima yaani mjini na vijijini.
===
Mkoa wa Shinyanga ulitengewa na kupatiwa Jumla ya TZS 11BL ambazo leo kwa mujibu wa RC watu wazembe wanaziangalia tu kwenye akaunti kama mapambo badala ya kuchangamkia Ujenzi ili ifikapo trh 06|01|2022 ahadi ya Rais Samia kwamba kwenye mwaka wake watoto wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha Kwanza wataanza shule tarehe moja nchi nzima yaani trh 06|01|2022 saa moja kamili asubuhi.
===
Wakati huohuo Rais Samia Suluhu Hassan tayari ameshapeleka kwenye halmashauri zote 184 nchini Jumla ya TZS 62.4BL kwaajili ya elimu bure, Hivyo watoto hawa anaowapambania leo Bi Sophia Mjema tayari ada yao ilishalipwa,Wazazi|walezi wao watanunua uniform pamoja na madaftari tu,Huyu ndio Samia Suluhu Hassan Rais wa awamu ya Sita na hizi ndio kazi zake.

Kazi nzuri
 
Back
Top Bottom