Unataka kunaimbia yesu alikuwa asnasoma injili ya luka,marko,matayo au yohana!?...hayo ni majina tu yakibidi yawekwe sababu hakuna alikuwa anajua nani alieyandika so njia rahisi ya kutambua sura ni kuweka majina hayo ya wanafunzi wa Yesu sababu wale wanafunzi wa yesu hawakuandika kitabu chochote yesu sabahu hata ukisoma kwenye bible inasema John na Peter walikuwa hawajasoma hawakujua kusoma wala kuandika
Acts 4:13 King James Version (KJV)
13 Now when they saw the boldness of Peter and John, and perceived that they were unlearned and ignorant men, they marvelled; and they took knowledge of them, that they had been with Jesus.
So bible ilipatikana na bahati mbaya kanisa katoliki ambali lilikuwepo hata kabla ya Yesu wakashukili mchakato na kuingiza mambo yao ya utatu.. Na mambo mengine mengine na kuweka vitu ambavyi hata yesu hakuwahi kuviagiza..!
Yesu haijui biblia vitu vingine vilibadilishwa na kuwekwa kwa mtindo wa kilatin sijui kama unajua hata jina JESUS sio jina halisi la muhisika, hilo ni jina la kilatin hata leo ushahid unao jina hili sio la kiyahud ni jina la kilatin utalikuta spain,mexic na sout america huwez kulikuta mshariki ya kati jina Jesus au Yesu au Jesu hajawahi kulisikia kwenye maisha yake.! Kama.ilivyo bible
Kuhusu Quran una haki ya kusema hivyo sababu hiifahamu kimpamgilio wake na Uthuman aliagiza zichomwe moto copy zote sababu alikuta kuna sehem wana copy zina mapungufu ya kisarafu na matamshi na sio kwamba wna Quran nyingine akawaita waandish walioteuliwa na mtume wakati wa kuandika Quran wakaandika upya na akaagiza watu wote waka copy ile lakin asingeweza kubadili sababu watu waliokuwa wamehifadh Quran walikuwa ni wengi akichukua hatua hiyo sababu alikuwa ndio kiongozi kuabadil copy sio kubadili kitu kilichopo vifuani kwa watu.!..sisi Quran ndio chakula au oxyegen yetu hautswali had ujue Quran mwez wa ramadhan inasomwa Quran kuliko kawaida had Uthuman anakuja kuchukua usukan miaka kumi imepita watu wanaish na Quran so kama angebadili chochote pangetokea utata lakin hakujawahi kuwa na shida hiyoo kwenye na yeye sio swahaba wa mwisho kwatiba maswaha wa mtume alikuwe Alii mkwe wa mtume na wajukuu zake mtume...unachokiziungumza ni katika watu wanao wapotosha ila havina ukweli..!
Hujanielewa labda kama unasoma kwa wasiwasi. Nitakuwa mwehu kusema Yesu alisoma Injili wakati hakukuwa na injili wakati wake. Hadi alipoondoka maisha yake na mambo aliyoagiza yakaandikwa. Nazungumzia Vitabu vya Musa, wafalme na wanabii.
Kuhusu hao vijana kuandika huku walikuwa "Sio Wasomi/ Learned" inaonyesha pia kuna haja ya kufahama Jewish education system. Inabidi uelewe Mungu alimaanisha nini alipowaambia wazazi wa kiyahudi maneno ya Torati 6:6-9
Yesu alijifunza kusoma na Kuandika Nyumbani kwa mama na baba yake. Ila uelewa wake ulikuwa mkubwa sana kwa wasomi wa kiyahudi pale hekaluni alipokuwa na miaka 12 alipojichanganya kwenye darasa la marabi katika shule iliyokuwepo pale hekaluni na uwezo wake na maswali yake yaliwashangaza maana yalikuwa ya kiwangu cha juu kuliko uelewa wa waalimu hao.
Timotheo alijifunza miguuni kwa Bibi yake Loisi na mama yake Yunisi. Aliishi mji wa kipagani Listra ambao haukiwa hata na sinagogi. Ndio ujue wamama wa kiyahudi sio wamchezo.
Kwa ufupi kusoma na kuandika watoto wa kiyahudi walijifunzia nyumbani hasa wale masikini kama wakina Yesu. Huyu bado alikiwa anatambuliwa kama mtu mjinga tu maana walikuwepo kwenye shule za marrabi, na mafarisayo chini wa waalimu nguli kama gamalieli. Wazazi wake paulo walimpeleka jeruslaem kutoka huko tarso akabobee kwa huyu mwalimu.
Pia kutokujua kusoma na kuandika sio mipaka kwa Mungu, Yeremia nabii hakuwahi kuandika kitu, ila Yote aliandikiwa na msaidizi wake Baraki.
Kuhusu Quran rudi ujifunze, ujue na watu 700 waliokuwa wamekariri maneno ya mtume na walifia vitani, hofu hiyo ikapelekea kaandikwe kwenye kitabu maana wale waliokariri wakifa na chenyewe kitakufa. Kumbuka pia ali na uthman walikiwa sio kitu kimoja kama unavyofikiri. Na kuna scholars wanasema hata hiyo aliyoandika haikukubalika na kila mtu sema ilibidi ikubalike kwa sababu ya nguvu ya dola. Rudi usome fitna za wakati huo kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika vya kiimani wenda ukajifunza upya. Ila kwa sababu sio mada naishia hapa, tujifunze zaidi. Maana mimi nilifuatilia history ya Islam series Karibu 22 na hiyo source ilikuwa ya hukohuko. Na sioni kama walichokuwa wanasimulia kinapingwa sana ukiacha moja juu ya imani kuw kitabu kile kiko perfect na ni direct maneno ya Allah japo hatufafanuliwi kwa kina hapo kwa uthman na uhakika wa nini kilichukuliwa na nini kiliachwa.