Biblia na reference ya vitabu vya kipagani


1: stanard bible ya wqkati wake mkuu sio agano la kale na jibya. Naamini kabisa katika maandishi yote ya wakati wa Yesu yalikuwa hayapewi hadhi sawa. Yalikuwepo maandishi na '' Maandiko matakatifu''. Hata Yesu alitenganisha kati ya "maandiko matakatifu'' na ''Desturi za wazee''.
Ikiwa yalikuwepo, na huko nyuma nimesema kulikuwa na utaratibu wa kuyahifadhi. Naomba ushahidi kuwa hadi kitabu cha enoch kilikuwa sehemu ya hebrew holy inspired writings maana hata Apokrifa havikuwa sehemu ya Bibilia. Hata Jerome alipocompile vulgate alivitenganisha na vingine kuonyesha kuwa havina hadhi sawa.
Na ninachokisisitiza msingi wa utambuzi wa maandiko matakatifu ni resonance ya waandishi hao wasiopingana na hakuna anayefundisha kitu kipya.
Katika reference zote za Yesu na manabii anarefer wa vitabu vinavyofahamika na havipingani na mafundisho ya bibilia.

2:Nadhani kuna sababu nyingi zilizopekelea hivyo vitabu visiwe sehemu ya maandiko nanvingine viwe sehemu ya maandiko.
ambazo zinamashiko na hata mimi nakubaliana nazo ukijumuisha na za martino luther. najifunza zaidi hapo. Ila unapoleta hoja za 300AD unapaswa kuchanganya na hoja za Karne ya pili BC ambapo wasomi wa kiyahudi zaidi ya 70 walipokutanika alexandria nadhani kuandika agano la kale kuyoka kiebrania kwenda kigiriki na hivyo vitabu unavyovitetea mfano Enoch na Jubilee. kumbe utagundua pamoja na mavitabu mengi kuwepo enzi hizo za kale lakini sio yote yalipewa hadi za kuwa maandiko matakatifu. Kitu kingine historia ya wakristo ktk karne ya awali pia kuliibuka watu wengi kama alivyoahidi Paulo pale troa kuwa wataibuka mbwa mwitu wasiwahurumie, waliibuka watu wengi walifundisha mambo mengi yasiyofaa. na pia sidhani kama kila balua ilikuwa intended kuwa sehemu ya maandiko, hata wewe leo ukipata mafunuo kutoka kwa Mungu tutayapokea kwa kuyapima kama yanaumana na wenzakomwa kale waliovuviwa na kuyakubali ila haiayawi bibilia au sehemu ya bibilia bali maagizo tu ya Mungu kwetu yanayotufanya tumuamini zaidi yeye na mitume wake.
Nitajifunza zaidi na Inshallah mwenyezi Mungu akinipa neema nitapita kutia neno la ziada kwenye hoja mbalimbali.

3:kanisa unamaanisha nini mkuu? kuhusu Luther alikataa baadhi lkn baadae alivielewa akavijumuisha. Kuhusu apokrifa kwa katolīki licha ya kukataa vitabu vingine vingi, ni tamko la kidini la mtaguso wa Trent ndio lililohalalisha hizo apokrifa. Tena kutoa kemeo la kitisho '' anaethma'' kwavatayevipinga, wanaweza kukaa mitaguso mingine hata mtaguso wa '' hong kong'' wakavitoa japo wanasema yale makubaliano ya trent ni ''ex cathedra'' hayapingiki. hata jerome alipoandika vulgate ile kwa mujibu ya wananzuoni(kama nakosea utanirekebisha) alivitenga pembeni maana hata scholars wa kiyahudi hawakuvihesabu kama ni miongoni mwa vitabu vilivyovuviwa ila vinaelezea matukio halisi kihistoria. Hata KJV ilipoandikwa viliwekwa vikatengwa pembeni pia (apokrifa) wenda kwa manufaa hayohayo.
Wengine hasa catholic wanavikubali maana ndiko waliopatia mafundisho yao (Dogma) mengine ni kama nguzo ya kanisa, mfano ibada za wafu na wamakabayo. Hakuna tendo la ibada ya wafu nje ya wamakabayo kwenye vitabu vingine. Waandishi karibu wote wamekubaliana kuwa mtu akifa analala, na ibada za wafu zinaonekana kwa wapagani zaidi. Na sio salama kujenga fundisho kwenye kafungunkaboja ambako jakaungwi mkono na vyanzo vingine.
Binafsi na nawapendekezea wote wasome bibilia 66Books, inakila utetezi na Lengo la Mungu kutupa maneno yake liko uchi kabisa kama sio wazi kabisa.
Huko kwingine kusomwe kama kujiburudisha na kujua mambo ya pembeni ili kutanua ubongo na uelewa wa mambo ya nje ya bibilia ili uiamini zaidi na sio ili uwe muasi, mtukana Mungu, mtu aliyechanganyikiwa na kuishi bila matumaini ya Uzima wa milele kupitia Yesu.


KwA UFUPI
1: Hao wakkristo waliokitana miaka ya 300 AD sio watu wa kwanza kucompile maaandiko. Bali watu wa kwanza tukianza na agano la kale ni Ezra na Nehemia chini ya Uonhozi wa Mungu. Lkn pia Kwa Mujibu wa Muratori flagments za 1740 zilikutwa na almost vitabu vyote vya agano la jipya ambayo aliyevicompile ni mtu anayeitwa Pius askofu wa kanisa la kikristo huko rumi mwaka 150AD miongo karibu 15 kabla ya hao wa 300AD. Peshito Syriac nauo ikataja vitabu vingi tu vya agano jipya tunavyotumia sasa ikiwemo hadi ufunuo wa Yohana miaka mingi kabla ya hao wa 300AD , vimetajwa pia hadi na wakina polycap askofu wa efeso na anasaidikiwa alikuwa mwanafunzi wa yohana pia. ninachpfahamu limitation ya technology nayo ilichangia upatikanaji wa wakati mmoja wa maandishi ya watu zaidi ya 30 walioandika katika range ya miaka 1500, hivyo hata makusanyo lazima iwe process kureflect uhalisia. Na hii ni moja ya sababu ya mimi Kuamini bibilia. Haikushushwa ni maneno ya Mungu yaliyoandikwa na binadamu halisi kwa mazingira na ugumu wao halisi kwa lugha yetu rahisi binadamu kuelewa.


2:Bibilia ni ukuaji, sio dude lililodondoka kutoka mbinguni. Hata Baada ya Kutoka babeli Bibilia au maandiko ya wakati huo yalyokusanywa na Nehemia na Ezra hayakuwa bibilia tulionayo sasa, Vitabu vingine havikuwepo. Hata mwanahistoria Josephus anayaita hayo maandiko matakatifu ya enzi zake '' Against Apion'' na Yesu kayathibitisha pote katika kauli zake. Hakuwahi kuzunhumiza au kuquote cha Apokrifa wala pseudo.... wa'la enoch maana havikuwa sehemu ya maandiko matakatifu ya wayahudi ambayo Yesu alijifunza utotoni na ujanani.

3:Kingine kuhusu enoch na vingine kuwa quoted, nimejifunza uhalali na usahihi wa nani kamkopi nani ni debate kubwa.
Hata mtetezi mkuu wa hivyo vitabu humu jukwaani anaitwa Eiyar ukimbana anakwambia vimefichwa, mara viko sijui etjiopia, mara siwezi kukwambia kama ninacho au la, yaani vimekaa kinjamanjama ambapo vinaonyesha sio vya kuaminika. Hata wewe huwa unaibuka unasema kuna maneno ya Mungu yamefichwa sijui vatican na kuna wengine hudai yamefungiwa Medicci Library huko Florence Binafsi mkuu huwa siamini sana hizo sarakasi na usiti wa maandiko matakatifu. Haya Yaliyopo Yamekamilika,



mkuu nimetoa maoni ya jumlajumla unaweza ukaokota vipande vya dhahamu humo sina shaka.
 

chief imani ni hali fulani yenye nguvu, nzuri na inasaidia sana ila pia ni mbaya sana kama mtu ataibeba bila kushirikisha ufahamu na utashi wake.
 
Mkuu zito anatoa reference zinazoeleweka kwanini nyie mshindwe kuweka reference ya kuhusu kupasuka kwa mwezi au na nyie hamjui au hamna uhakika wa mahadithi mnayosimuliwa??!
Reference zitolewe mara ngapi ?
 
Kama hawakubaliana Lazima had leo ingekuwepo nakala ya maandiko amnayo ingesema hichi kiliachwa au hichi kimeonvezwa haikikuwepo aababu watu waliokuwa a wamehifadh Quran ni wengi kama ambavyo ipo kwenye bible na kibaya ndugu yangu unasima sana history za mashia lakin hata wao hawana Quran mbadala...nikuuukize wwwe unaamini kwenye bibe ya bitabu 72,66 au 82 na nani yupi sahihi kati ya hao na kwanini vingine viwepo kwa wengine visiwepo.!
 
Mkuu mitale na midimu nimeona ntapandisha uzi kuhusu Canonicity ya Biblia na ntaeleza shida ilipoanzia maana naona imekuwa topic kubwa kidogo..... Labda kwa ufupi tu nkijibu hoja zako
1. Greek Septuagint iliinclude apocrypha/Deuterocanonical books na ndio iliyotumika kipindi cha Yesu na HAVIKUTENGANISHWA kabisa.... sema baada ya masoretic texts kuja ndio wakavitenga.... Na hapo unaposema manabii hawakunakiri nimeshasema mara 100 humu kuwa new testament imequote baadhi ya Apocrypha mfano hicho kitabu cha Enock na kama sio naomba unisaidie mistari hii imequotiwa kutoka kitabu gani cha agano la kale na kama hajatoa huko kivipi ufanane na kitabu cha Enock

Yuda
14 Na Henoko, mtu wa saba baada ya Adamu, alitoa maneno ya unabii juu ya hao, akisema, Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu,
15 ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu....

Yuda
6 Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.

Naomba kwa vyanzo vyako ukahoji kokote hizo reference za Yuda wanatheolojia wanakiri aliquote kwa Book of Enoch hasa sura ya 6.

2. Mkuu hapo nmeshaeleza Greek Septuagint ilikuwa na apocrypha zote bila kutenganishwa na ndio maana wakatoliki wameiadopt ikapelekea kuwa na vitabu 7 zaidi (nafkiri ntaliongelea zaidi kwenye huo uzi wa canonicity ya Biblia) ila nilichosema mimi kufikia AD 382 ndipo standard Bible hasa vitabu vya agano jipya ndipo vilikubalika labda wwe unaweza nipa source ya uwepo wa canon ya OT na NT katika mjumuisho wake kabla ya 380 AD.

3. Naposema kanisa namaanisha East orthodox church inayokubali baadhi ya apocrypha hivyo ina vitabu kama 68, Tawahedo Orthodox la Ethiopia lina vitabu 81, Protestants kama pentecost,lutherans,SDA wana vitabu 66, Roman Catholic vitabu 73!!! Ndio hapo nauliza huoni kuna shida?? Kwanini Mungu aruhusu kila kanisa kuwa na Biblia yake?? Je waliongozwa kweli na roho wakati wa kucompile (hili pia ntaliongelea zaidi kwenye ule uzi)

Kuhusu maswala ya nyongeza

1.Mkuu kuhusu NT Canon kabla ya council of Rome hyo AD 382 kulikuwa na wengi waliocompile lakini hawakufikia conclusion kuhusu canonicity ya baadhi vitabu mfano ufunuo,2 peter hivyo wengine waliviacha wengine waliviinclude lakini hao council of Rome ndio wakafanya cross reference na kufikia hitimisho RASMI kuwa NT iwe na Vitabu 27 ambavyo ni hivi tulivyonavyo.

2.Pia hakuna mahala niliposema Enoch ni kitabu kitakatifu ila nachosema manabii wa enzi hizo walivisoma pia na ndio maaana kuna makanisa kama ya Orthodox kama hilo la Ethiopia limekitumia mpaka leo tokea enzi za Yesu na walikuwa wanakisoma kanisani tokea AD 300... Na ndio maana nikaleta huu uzi kuhoji kwamba licha ya (Enoch,jasher,Acts of solomon) kutokuwa vya kitakatifu lakini mbona mitume wamevinakiri?? Na ndio maana hapo juu nimeuliza tu naomba unisaidie Yuda alitoa wapi reference kuhusu maneno ya Henoko kwenye mstari wa 4,6,13 n.k??

3. Hakuna debate yeyote mbona wanatheolojia wameshaconclude tu... Unajua shida ya sisi tunakuwa biased mfano Yohan akicopy maneno ya Isaya au stefano akicopy maneno ya Yakobo watu wanasema amecopy OT ila mtu akinakiri book of jasher au Enoch au acts of solomon utaulizwa "una uhakika gani kama hicho kitabu alichonakiri ndio kile original"!!! Sasa kwanini kwa mathayo hamkuhoji kama ni kitabu cha "mwanzo" halisi ila kwa Yuda na Joshua mtahoji hivyo?? Hii bias ndio inaleta debate lakimi tukiamua kuwa objective tutagundua kuwa ukweli ni mmoja TU

Kuhusu mkuu Eiyer naweza muunga mkono sababu mfano hicho kitabu cha Gad the seer kimekuwa termed as LOST BOOK!! hata kitabu kinachodaiwa kuandikwa na Mfalme Ogu nacho kimekuwa termed as LOST BOOK ingawa kuna script moja ya wanatheolojia wanadai sio kma vimepotea bali vimefichwa!! Otherwise labda nikuulize wwe vitabu vya watakatifu kama Nabii Gadi au Nabii Samuel inakuaje vipotee?? Ina maana maneno ya Mungu yanaweza potea tu kama toilet paper??

Ubarikiwe mkuu
 
● "Narrated Hisham's father: Khadija died three years before the Prophet departed to Medina. He stayed there for two years or so, and then he married `Aisha when she was a girl of six years of age, and he consumed that marriage when she was nine years old." (Sahih Bukhari 3896)

● "Narrated `Aisha: That the Prophet (Muhammad) married her when she was six years old, and he consummated his marriage when she was nine years old, and then she remained with him for nine years (i.e., till his death). (Sahih Bukhari 5133)

● "Narrated 'Urwa: The Prophet (Muhammad) wrote the (marriage contract) with `Aisha while she was six years old, and consummated his marriage with her while she was nine years old, and she remained with him for nine years (i.e. till his death)." (Sahih Bukhari 5158)

● "Narrated `Aisha: The Prophet (Muhammad) used to lean on my lap and recite Qur'an while I was in menses." (Sahih Bukhari 297)

● "Narrated Um Salama: While I (Aisha) was laying with the Prophet (Muhammad) under a single woolen sheet, I got the menses. I slipped away and put on the clothes for menses. He said: "Have you got "Nifas" (menses)?" I replied: "Yes." He then called me and made me lie with him under the same sheet." (Sahih Bukhari 298)

● "Narrated `Aisha: The Prophet (Muhammad) and I used to take a bath from a single pot while we were Junub. During the menses, he used to order me to put on an Izar (dress worn below the waist) and used to fondle me. While in I`tikaf, he used to bring his head near me and I would wash it while I used to be in my periods (menses)." (Sahih Bukhari 299, 300, 301)

● "Narrated `Abdur-Rahman bin Al-Aswad: (on the authority of his father) `Aisha said: "Whenever Allah's Messenger (Muhammad) wanted to fondle anyone of us during her periods (menses), he used to order her to put on an Izar and start fondling her." `Aisha added, "None of you could control his sexual desires as the Prophet (Muhammad) could." (Sahih Bukhari 302)

● "I (Aisha) said (to the Prophet): "I feel that your Lord hastens in fulfilling your wishes and desires." (Sahih Bukhari Volume 6, Book 60, Number 311)

● "Narrated 'Aisha: I used to wash the traces of Janaba (semen) from the clothes of the Prophet (Muhammad) and he used to go for prayers while traces of water were still on it (water spots were still visible)." (Sahih Bukhari Volume 1, Book 4, Number 229)

● "Narrated 'Aisha: I used to wash the semen off the clothes of the Prophet (Muhammad) and even then I used to notice one or more spots on them." (Sahih Bukhari Volume 1, Book 4, Number 233)
 
Kule nyuma umesema uislam unaenea kwa kasi sana ulaya na marekan.Na makundi kwa makundi ya wazungu wanaingia katika uislam.hiyo inamaanisha kuwa uislam umeanza kukubalika kwa kasi sana huko ulaya na marekani.
Sasa hapa unasema;UKIANDIKA KTABU CHOCHOTE KILCHO AGAINST NA UISLAM, UTAPATA SAPOT KUBWA KTOKA ULAYA NA MALEKAN.
SWALI: huko uraya na marekani wanaishi jamii gani?.
Iweje wazungu waupokee uislam kwa kasi..
Alafu hao hao wanao upokea uislam kwa kasi..akitoke mtu kama gwajima akaandika kitabu kinachoupinga uislam wanamsapot.

Maelezo yako yanakanganya sana na hii n kwasababu mnaamin na kuabudu vitu visivyo kuwepo.
 
Tukutane uwanja wa hukumu...kila mtu ujumbe umemfikia ni akili yako...

Allaha amesema " tutawaonesha ishara zetu had watakaposema hii ni kweli na hatutamuhumu yoyote ila tu yule tuliyemfikishia ujumbe..!"

Am out on this
 
Nilipokuwa nikisoma canonicity nilifundishwa vigezo vilivyotumika kuweka vitabu kwenye Biblia na moja ya vigezo ni kunukuliwa na Bwana Yesu. Kwa mfano Yesu katika huduma yake alinukuu vitabu vingi vya agano la kale lakini hakuna ushahidi wa kutosha kuwa Bwana Yesu alinukuu yale mavitabu ya apokrifa.
Sisi wakristo kiongozi wetu ni Bwana Yesu na zaidi katupa roho mtakatifu anayeshuhudia ndani yetu. Only common people with common mind cannot comprehend
 
Sasa mbona Joshua na Yuda wamenukuu Apokrifa ila bado vitabu vyao vipo kwenye Biblia?? Unaweza kutusaidia kwanini?? Pia utueleze kivp Mwandishi wa samuel na wafalme alinukuu vitabu vya apokrifa pia lakini mbona vipo kwenye Biblia bado??

Tuanzie hapo kwanza
 
Kama Yesu akivinukuu sio case. Jambo lingine je, unaamini ujazo wa Roho mtakatifu? Je, umezajwa Roho mtakatifu?
 
Kama Yesu akivinukuu sio case. Jambo lingine je, unaamini ujazo wa Roho mtakatifu? Je, umezajwa Roho mtakatifu?
Nimeandika nimefuta nimeandika nimefuta.... Hata sijui nijibuje!!

hivi tumefikia huku kwamba mtu akihoji basi hana Roho mtakatifu!! Kwahiyo wakristo wote wasihoji kitu!!
 
Nimeandika nimefuta nimeandika nimefuta.... Hata sijui nijibuje!!

hivi tumefikia huku kwamba mtu akihoji basi hana Roho mtakatifu!! Kwahiyo wakristo wote wasihoji kitu!!
Pasipo Roho mtakatifu Ukristo hauna maana. Ukiwa na Roho mtakatifu atakufunulia siri zote zilizositirika. Atakufundisha na kukusaidia kuomba, atakufundisha nini ufanye na nini usifanye. Atakupa uwezo wa kuishida dunia. Wakristo hatukuachwa yatima na wale wakristo wa kweli huwa hatubishani mambo ambayo ni controversial kwa common mind kwa sababu tuna Roho mtakatifu anayeishuhudia kweli ya Kristo ndani yetu katika hili hatuteteleki kwa sababu katika dunia hii mafundisho na dini za uongo zipo tangu zamani na wote wanatumia Biblia lakini hutawasikia wakimzungumzia Roho mtakatifu kwa vitendo.
Ukiwa mkiristo bila Roho mtakatifu, ukristo wako ni bure
 
Daah!!

Mkuu nimesoma baadhi tu ya page za uzi huu na mwishoni,nikipata wasaa kunako majaaliwa nitaupitia...

Hakuna namna yoyote mtu anaweza kubisha na kuondoa umuhimu wa vitabu vingine kuelezea mambo yaliyoko kwenye biblia kwa kina na hii inavifanya kuwa vitabu vya muhimu kwa muktadha huo...

LAKINI,vitabu vilivyoko kwenye biblia ni vitabu vilivyoandikwa kwa namna yake na inahitaji utulivu kweli kweli kuelewa mambo mengi kama si yote....

Ndio maana watu wanaishia tu kutoelewa na kuita hadithi....
 
Na huu ndio unafiki wa wana JF ulikuja na hoja ya kimwili kwamba apokrifa haikuwa quoted na BIBLE mie nikaleta ushahidi wa kimwili pia kuwa zilikuwa quoted.... Ndio sahivi unamuingiza roho mtakatifu kwenye hii mada kwanini na wwe usingeenda kwanza kuomba mungu kabla hujaja kujibu mada kwa kutumia "akili zako".

Kama hamtaki tuhoji mada za kiimani basi kusingekuwa na haja ya vyuo vya biblia, kusingekuwa ha haja ya bible study au kwenda kanisani bali tungejifunza tu maandiko wenyewe chumbani bila haja ya kusubiri ichambuliwe na mchungaji wako.

Kama ni hivi basi shule tusiende,kazi tusifanye tukae nyumbani tusubiri roho atufanyie kila kitu!!

Hizi defence mechanism za wafia dini, zinaua hili jukwaa.
 
Na hiyo Biblia kuisoma bila divine illumination na revelation inayotokana na Roho mtakatifu ni kazi bure.
 
Ahsante sana naomba majina ya hao watu 12(maswahaba As) waliokuwa wakiiandika Quran wakati wa mtume(saw)
1.Uthman
2.zeyd
3.
4.
12.
Na majina ya maswahaba(as)6 waliobakia na kuiandika tena upya baada ya Uthman kurudi Makkah
Nitashukuru
Nalog off
 
66
 
asante mkuu kwa mrejesho mzuri.
Kuna mambo kadhaa kama hutaona tabu uyajumuishe kwenye Uzi wako utakaouleta.

1: Kuna ushahidi wowote kuwa vitabu vivyo hasa apokrifa vilikuwa ni sehemu ya cannon ya wayahudi?
2:Wakati Septugiant (LXX) inaandikwa Nusu ya kwanza ya karne ya tatu, Vitabu ambavyo vilikuwa na uhakika kuwa vimeandikwa au kuwa sehemu ya canon ya wayahudi ni Pentateuch au Torah. weka uthibitisho wa wanatholojia kuwa 100% wanauhakika kuwa kwenye pentateuch kulikuwa na Apokrifa kama jewish canon.
3: Je, Kuna ushahidi kuwa Apokrifa vilikuwa sehemu ya Jewish canon japo najua vilikuwepo kama vitabu vingine vingi ambayo list yake haifahamiki lakin nahoji canonicity yake?
4: Unamzungumziaje Jerome aliyetafsiri Septugiant na list ya vitabu vilivyokuwemo kwa wakati wake, Mwaka 345- 420, Na kwa akili yake timamu akaweka wazi kabisa hivyo sio sehemu ya Canon na Visitumike kuundia doctrine '' kama wenzetu wanavyovitumia kutengeneza doctrine ya kutolea sadaka za wafu na mambo mengine''. Na kwa sababu hilo zoezi alilifanyia hukohuko uyahudi katikati ya wayahudi huoni kama alijua nini kiliaminiwa na nini hakikuaminiwa kama cannon kwa wayahudi?
Japo aliviona vyafaa kusomwa, maana hata mimi naona hoja kwa sababu vinacover intertestimental period karibu miaka minne kati ya malaki na mathayo na angalau vinatujulisha nini kilitokea katika wakati huo wa ukimya.

5:Augustine ndiye aliyetoa pendekezo la kuandika iandikwe bibilia ya kilatini ili kuunganisha wale wa magharibi na wale wa mashariki walio kuwa wanatumia kigiriki. Na inaonekana yeye ndiye aliyependekeza hizo apocrifa kuwa na hadi ya inspired japo kwa wenzetu Catholic church zilipigiliwa msumari kwenye mtaguso wa Trent baada ya kuibuka upinzani wa waprotestant.
Hii unaizungumziaje, unaweza kukosoa au kuipinga uhalali wake kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya kitaalimungu katika uzi huo ili tupate vina vya mada.

6:Unawazaungumziaje Luther na Jerome wote kwa pamoja kutambua uwepo wa vitabu hivyo lkn sio katika level za canon au inspired na kuonya visitumike kudefine christian doctrine.


Kwa sababu Pseudepigraphical books sio apocrifa ie book of enoch na wezake, na quote za Yuda hapo ninahojankadhaa.

1: Kama unasema inakubalika kwa wanatheolojia wote katika utofauti wao, maana na wenyewe wanapingana (liberal, historical criticals, conservatieves etc) naomba hapo nisibishe ila niseme kuwa kiwepo au kisiwepo miongoni mwa sababu ya kukiacha ni kuwa mujibu wa wanatheolojia pia hata wayahudi hawakukipa hadhi ya kuwa cannon. Hivyo kuwa quoted ikiwa ndivyo ilivyo haikihalalishi uvuviwaji wake. Ndio maana huko nyuma nilikuambia Paulo alipoquote mtunga mashahiri wa athene haikuhalalisha kila kilichomo humo. Hivyo sioni hoja kwenye kuquote, au kuzungumziwa wa vitabu vilivyo hivyo.

2:Naunga mkono sio maandiko matakatifu kwa sababu pia kinapingana na maandiko mengine ambayo yanakubaliana kwenye some issues.

mfano
Yesu anasema wazi kuwa Mbinguni hakuna Ngono. Hivyo malaika sio Sexual beings. Sasa huyo wa Enoch anazungumzia habari za ngono na malaika. Japo najua hapo kuna mgogoro wa mwana wa Mungu vs wana wa wanadamu. Ila mimi namuamini Yesu ambaye aliyoka huko mbinguni kuwa No sex in heaven, hivyo angels are not sexual beings. Mathew 22:30
Kuna story nyingi za kufurahisha ambazo zinaleta migogoro mikubwa na waandishi wake.
Pia kinakadiliwa na baadhi ya wananzuoni kuandikwa karne ya kwanza BC hivyo kwa uzingativu wa nono-canonoicity wake hata story zake sio za kutumainiwa. Nawaunga mkono wote wanaovipinga hivi pamoja na apokrifa.




kuhusu Quote, au kuandikwa kwa vitu vingine kwenyw vitabu vilivyovuviwa nimesema na naendelea kusema sio tatizo na haivifanyi vitabu hivyo kiwa Vimevuviwa.
Pia Kristo Yesu kwa sisi wakristo hakuanzia Pale Bethrehemu alipozaliwa, alikuwepo Hata kabla ya waandishi wa Vitqbu Vyote, na vilivyovuviwa alishiriki hivyo kauli zake kwangu ni Zaidi ya Authority. Hakuwahi popote kuindorse mavitu yanayopingana na 66Books katika kauli yake.

Pia mimi kama SDA, kama kanisa na wanatheolojia wa kitengo cha utafiti wa Bibilia kwa kitafiti kwa kina na kwa msaada wa Roho mtakatifu hayo yanayoitwa maandishi ya siri, vilivyopotea, Apocrifa, pseudo... tumehitihisha 66 inspired books are our authority.
Na Vingine vyote nje ya hapo ni vitabu vizuri vunavyofaa ambavyo havijavuviwa na havifai kufanywa kama rejea kitabu kilichovuviwa. Ila naweza kurejea kitabu chochoote hata sio tu cha wayahudi, bali hata cha wahindu, freemasonry, wapagani afrika kumagnify kile bibilia ya 66 inachosisitiza, kama alivyofanya paulo au Yuda ikiwa kweli hicho kitabu cha enoch.

Mfano umenifundisha Kuhusu Cathage empire na Yule mbabe aliyekaribia kuangusha dola ya Rumi. Nikisimama popote kuzungumzia Unabii wa Daniel 2, 7, Ufuno 13 kuthibitisha kauli ya Mungu kuwa Roman empire haitaanguka, bali itqgawanyika na ushawishi wake utakuwepo hadinmwisho wq dunia nitawaonyesha watu jinsi ilivyoshindikana kuangushwa na watunisia/cathage.
Hii yote haiyafanyi maandishi ya kikathage au hizo historia nilipoquote hilo tukio nimevipa hadhi sawa na bibilia.

Mwisho
Point yangu kuu kwenye uzi huu ni ile niliyoiandika front page ya kwanza kabisa. Bibilia ni Kitabu cha Mahusiano kati ya Mwanadamu mdhambi na Mungu wake, Tukikosa big picture hii katika kujadili haya tutakuwa umeamua Kunywa maji ya kunawa kisha tukaondoka tukiwa tumeacha misosi mitamu na maji ya kunywa na kufa kwa njaa kwa upofu huo.


ubarikiwe mkuu zittoJr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…