Biblia na reference ya vitabu vya kipagani

Sasa kama lutu alilala nawawe na biblia imeandika ivyo,mbona kwa daudi haikuandika kuwa alilala na Jonathan I?
Sababu Biblia imesema story nzima ya Daudi A to Z imeandikwa kwenye kitabu cha Gadi na Nathan hivyo tukivisoma hivyo ndio vina details pana zaidi kuhusu maisha private ya Daudi.... Je wwe umevisoma?? Kama bado kwanini unabisha??

Pia Alichosema huyo mchangiaji ni kuwa Daudi hawezi kufanya hyo dhambi ndio sasa nahoji kama Lutu aliweza lala na wanawe au Daudi aliweza kumlala mke wa mtu na kumuua mme wake je kipi kinamfanya asifanye dhambi zingine kma hizo??
 
Wewe unacho kitabu cha yashari (original) au umewahi kukiona?

Unaelewa maana ya kanisa???
Maana unachosema Roman kwamba ni kanisa unakosea,,,vitabu vya Roman Catholic sio vitabu vya wakristo wote,,,Unapoongelea injili ya baraba,,injili ya Magdalene au injili ya batilomayo Tayari kwa wakristo wengi unakuwa umetoka nje ya mstari...

Hakuna injili ilio kinyume na Yesu kristo..Sijui Yesu alioa,,Yesu hakufa msalabani au Yesu ana baba wa kibinadamu,,,hizi injili zilifaa ziwe conspiracy theory kwenye you tube,,au ziwe vitabu vya kuwapa vichaa kwenye kambi zao maalum labda wangezielewa wakiwa bado hawajapona.

Kamwe Huwezi nielekeza chochote kwa vitabu vilivyoandikwa na wasomi feki wa theology au watu wahuni kama da Vinci hivyo vinawafaa watu wanye vimelea vya ucrazy.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
1. Ndio nimekisoma kitabu cha jasher na pseusepigrapha zingine....

2. Naposema kanisa simaanishi katoliki tu ila new testament canonization tokea council of Rome mpaka martin luther kwa madhehebu ya kiprotestant wote wanatambua hivyo vitabu kama ni pseudepigrapha lakini cha kushangaza manabii wa Biblia wamekinakiri....

3.Unaposema hakuna injili kinyume unamaanisha nini.... Sema waliochagua vitabu gani kukaa kwenye Biblia yaani council of Rome au wale wa contantinople na sinope ndio waliamua kuwa kati ya story A na B tuchukue za story A alafu zoooote zinazokinzana na story A tusiviweke pamoja ila unaposema INJILI it's usigeneralise maana injili zimeandikwa na wengi sana na zote zimekinzana ikiwemo zile injili 4 za kwenye agano jipya zinakinzana baadhi ya maeneo ila bado vimebakizwa kwenye Bible.... Je umewahi kujiuliza kwanini??

4. Wasomi feki ni kina nani?? Unaposema feki unaweza niambia muandishi wa kitabu cha wimbo ulio bora ni nani ilihali kimeandikwa miaka 200 baada ya Suleiman kufa?? Unaweza nisaidia nani kaandika kitabu cha waebrania?? Pia barua za paulo unaweza nisaidia ni nani aliziandika?? Je kama nazo hazikuandikwa na hao waliohusishwa na hicho kitabu mbona sijawahi kusikia mkisema ni WAANDISHI FEKI?? Hivi unafahamu kwanini kitabu cha yakobo kimeitwa James kwa kiingereza??

Naomba ujibu kwa mpangilio niliouliza... Na usije na mihemko tena bali hoja tu
 
1. Mkuu naposema standard bible namaanisha hii set kama ya Genesisi to Revelation but nachojua vilikuwepo vitabu mbalimbali mfano Torah na vitabu vya manabii wengine wa kiyahudi kwa mamia yake (sio 39 pekee) na wote tunajua kuna baadhi ya vitabu kama ufunuo wa yohana imeandikwa miaka mingi baada ya Yesu kufa hivyo unaposema standard bible ilikuwepo wakati wa Yesu hatuwezi kuwa realistic.

Kuhusu vitabu hivyo vilivyoachwa kuwa vitakatifu ni evident sababu tunaona Yuda na Petro wakifanya direct quotation ya maandiko ya Kitabu cha Henoko.... Hivyo kma sio matakatifu sidhani kama wangeweza kuyaquote na kujengea hoja kama ambavyo waliquote vitabu vya isaya,zaburi n.k

2. Kuhusu compilation
Kwa uelewa wangu kufikia AD 300 kulikuwa na vitabu na nyaraka mamia yanasambaa yakidai ni maneno ya mitume sasa ili kuzima hiyo sintofahamu ikabidi wafanya new testament canonization ili wapate standard bible ya kutumika ulimwengu kote.... Mfano Council of Rome kufikia AD 382 ndipo walipotoa complete list ya vitabu vya Biblia ambavyo ndio halali kabisa na kwa mara ya kwanza kanisa likatambua vitabu 27 ingawa kabla ya hapo vitabu vilikuwa vingi vinazagaa so baada ya mchakato wa kuvikagua ndio wakafikia conclusion kuwa Biblia halali ni hii kwa mara ya kwanzo ilikuwa 382 ikimaanisha kabla ya hapo hakukuwa na standard Biblia hivyo mnaposema kuwa vitabu vilivyoachwa vinakinzana na maneno ya mitume sidhani ni sahihi unless ungesema watu waliocompile Biblia waliamua kugawa vile vinavyokubaliana kutoka kwa vinavyopingana (Collect like terms) ila mnaposema vinakinzana na manabii it's as if Biblia (yaani vitabu 66/72 n.k) ilikuwepo ndipo vikaandikwa hivyo vingine kma cha Enock au Jasher ili viipinge Biblia hicho ndio nachoona sio sahihi.

3. Pia unasema vilivyopo ndio vinakidhi vigezo.... Sasa hivyo ambavyo unasema havikidhi vigezo ni kwanini Biblia inaviquote na kuvirefer tukasome??

Kama vinatosha sasa kivipi kanisa ulimwenguni liliruhusu kuwa na Biblia tofauti mfano catholic wawe na 72, protestant 66 hapo bado martin Luther naye alipunguza baadhi ya vitabu ambavyo protestants wengine wanavitumia (refer luther bible) hapo bado kuna orthodox la tokea enzi na enzi la huko Ethiopia lina vitabu 84!!! Sasa kwa staili hii who is right and who is wrong?? Na kama one is wrong kuongeza au kupunguza vitabu je ni kwanini Mungu ameliruhusu hilo kuwa kanisa lipotoshwe na watu wachache??

Embu tuwekane sawa mkuu maana kupitia maswali haya tunajifunza mengi, ubarikiwe
 
Tunaweza kutofautiana kitafsiri but kumtumikia Mungu na mwili kufa kwa dhambi (kwa maana ya kutubu dhambi) haviko sawa though vinafanana. Nitakupa mfano mmoja ambao na wewe pamoja na wachangiaji wengi humu tunaujua, kabla sijatoa mfano huo unao julikana niseme hivi; mtu anaweza kumtumikia Mungu tena vizuri tu lakini akawa hajafisha mwili kwa mambo ya dhambi na this is why kuna sehemu Yesu anasema hivi, "...Wengi watakuja kwangu siku ile wakisema, Bwana, tulitoa PEPO kwa jina lako na kufanya miujiza mingi na hata kutoa UNABII kwa jina lako, name nitasema, tokeni kwangu enyi watenda dhambi" Mathayo 7:7-kuendelea. Ukisoma hapo, Yesu hakatai kwamba watu hao walikua wakimtumikia au laa, concrn yake ni "enyi watenda dhambi". Sasa nitoe mfano, tumezoea kumuona mzee wa upako akihuburi kwenye television na sometimes hata kufanya miujiza iliondikwa kwenye Biblia but siku moja alionekana kalewa chakari na habari zilionesha (baada ya vipimo) alikua katupia mabapa kadhaa kwa mwili wake, now the question is, "Huyu nae kafisha mwili wake kwa dhambi"? Jibu lake kila mtu anaweza kusema lake! Na hatukuwahi kumsikia walau akijutia jambo lile but record iliopo ni kwamba alilaani watu wale walio andika habari zile kwamba baada ya muda Fulani watakufa, until now, zaidi ya mwaka sasa, hakuna aliyekufa. Mimi nilipata habari ile through my lovely dada Happiness Katabanzi kwenye FB wall yake so nadhani katika waandishi waliotakiwa KUFA kimwili ili tuwazike ni huyu dada Happy!
 
Mkuu zitto junior simu yangu nahisi ilipigwa kipapai ,tags nyingi nilikuwa sipati ni kama vile simu ile (haipo tena)ilikuwa inaficha post....nimeipa talaka 7 na sasa niko huru ndio maana nimeweza kufika huku tangu Jana....nimeisoma mada kwa kutulia asante sana
 
Chiefs
Zito na Mshana Jr
naomba kuuliza
Katika kusoma,unakutana na uongo na ukweli katika maandishi na vitabu
Je!mnatumia njia gani hasa ya kujiridhisha,kuhusu vitabu hivyo mbali ya Bible,kuwa ni sahihi?!!

kwasababu,kuona mwandishi anamsema vibaya Nabii wa Mungu,si jambo dogo au la kuchezea hata kidogo

nataraji nitajibiwa vzr
nawatakia siku njema
 
Sijafahamu hivyo vitabu ni vipi mkuu ambavyo unaongelea lakini kama ni hivyo nilivyotaja basi unatakiwa uangalie mwandishi ni nani,vyanzo vyake,n.k ukiona vipo credible basi unaichukua hiyo taarifa maana lazima tukubali Biblia haikuandika kila kitu kama ambavyo Quran haikuandika kila kitu hivyo kurefer nje ya vitabu vya dini hakukwepeki as long as vyanzo ni credible....

Kwa case ya vitabu vya Bible ambayo inatumiwa na wakristu inatakiwa waombe kwa Roho Mtakatifu awafunulie na kuwatafsiria maandiko ambayo wao kwa akili zao za kawaida wanaona kama kuna makosa/sintofahamu au kutokueleweka.

Pia hakuna kitu kama uongo duniani as long as mtu ana ushahidi wa kubeba hoja yake mfano kuna wengine wanasema magufuli ni dikteta kwa kuleta hoja zao na wengine wanasema sio dikteta na wanahoja nzito pia hivyo inategemeana uzito wa ushahidi

Sasa kuhusu Nabii Daudi huwezi ita uongo kisa tu Biblia haijaeleza wazi ndio maana nikasema kama Daudi aliweza kumfanyia unyama uriah wa kumuibia mke wake kwanini dhambi zingine asiweze fanya pia?? Nachotaka tuelewane ni kwamba dhambi haina ukubwa wa jina ndio maana suleiman pamoja na hekima zote ila bado alikuwa na udhaifu wa uzinzi pia samson naye alikuwa na udhaifu huo wa ngono..... So hakuna exception maana hakuna mwanadamu kamili duniani muhimu kama alifanya kweli alishaomba msamaha kwa Mungu na atakuwa mbinguni.

Mtazamo wangu ndio huu
 
Nimekuelewa Mkuu

Ila sisi Waislam
Tumejengwa kwa misingi madhubuti,hususan kuhusu Manabii wa Mungu
Katika maandishi yetu,tumefunzwa kuwa
Manabii wamekingwa na makosa/madhambi makubwa,wanaweza kufanya dhambi ndogo kwa ubinaadam waliokuwa nao,kisha Mungu akawasahihisha,
Lkn kosa/dhambi kubwa,Hapana
Hakuna Nabii wala Mtume,aliewahi kufanya Dhambi kubwa ya aina yoyote
Dhambi ya Zinaa na Kunajisi kinyume na maumbile,ni dhambi za Laana,ni Dhambi kubwa,ambazo Mungu muumba mbingu na ardhi,anazichukia mno
Na tayari Mungu,ashachukua ahadi ya kuwakinga Manabii na Mitume yake na Madhambi/Makosa makubwa
Sisi,hatuna haki kabisa,juu ya kuwatuhumu wateule wa Mungu,na Madhambi mabaya kama hayo

Huu ni uelewa wangu ndg
Shukran sana Bro
 
Mkuu nimekujibu kwa mujibu wa Biblia na apocrypha zake..... Na kwenye Biblia naona kuna baadhi ya manabii/waamuzi walifanya mambo ya mwilini kabisa kama uzinzi,mauaji kinyume na maagizo ya Mungu na Biblia inasema Mungu aliwaadhibu na baadae waliomba msamaha wote kabla ya vifo vyao kwa makosa yao waliotenda.

Ndio maana nikasema duniani hakuna ukweli au uongo ila ina depend ushahidi ulionao mfano Bible inasema Daudi alifanya uzinzi ila Quran haisemi hivyo kwa muktadha huo ndipo unazaa mjadala kuwa nani muongo nani mkweli...mjadala ambao haujawahi kuisha na hautoisha maana kila mtu ana maandiko ya imani yake yanayoprove anachosema.

Ila hoja yako nimekuelewa sana mkuu ubarikiwe
 
Kwahiyo Mkuu tuseme Mungu hana alichofanya katika kuweka sawa huo mvurugano kwenye biblia na imani yake kiujumla kwa kurekebisha ni lipi sawa na limepotoshwa?
 
Kwahiyo Mkuu tuseme Mungu hana alichofanya katika kuweka sawa huo mvurugano kwenye biblia na imani yake kiujumla kwa kurekebisha ni lipi sawa na limepotoshwa?
Haya mambo ya lipi ni sahihi na lipi si sahihi kwa mtazamo wangu watu wanamsingizia tu kuwa Mungu ndio kahusika ila nachokiona ni mawazo ya wanadamu wenyewe mfano

Wakatoliki wao wana vitabu 72

Protestants wana vitabu 66

Haya Martin luther baba wa protestants alifuta vitabu kama 6 kutoka biblia ya protestants (luther bible)

Orthodox la kale ambalo mpaka leo lipo Ethiopia (Tawahedo) wana vitabu 82

Sasa inatakiwa tujiulize kama ni Mungu ameamua tuwe na vitabu kadhaa kwanini basi kila kanisa lina Biblia yake?? Je Mungu anakinzana na maagizo yake mwenyewe?? Na kama sio ni kwanini basi watu wasistize kuwa vitabu gani viingie kwenye Biblia ilipangwa na Mungu mwenyewe ilihali madhehebu makuu yote yana Biblia tofauti??

Nachojua Mungu alituachia vitabu sawa ila zoezi la uhakiki na kuchagua lilifanywa na wanadamu kutumia akili zao tu ila kama ingekuwa wamesikia sauti ya Mungu kusingetokea huu mkinzano....

Siku nitaandaa uzi kuhusu Canonicity ya Biblia utaona humu wakatoliki,wasabato,walokole na walutheri watakavyokashifiana kuhusu namba halisi ya vitabu vya Biblia ni ngapi.... Cha kushangaza kila mmoja atakwambia utaratibu mzima wa kupatikana vitabu vya Biblia uliongozwa na Mungu!! Which is true lakini cha kujiuliza kwanini wawe na Biblia yenye vitabu tofauti??

Hapo kumbuka bado kuna mjadala kwa waprotestant kwamba kati ya King james na NIV ni ipi Biblia sahihi kutumika..... Conservatists wa kanisa wanakwambia NIV imechakachuliwa na reformists wa kanisa watakwambia NIV ndio halali ila king james ni batili.... Alafu muda huo huo watakwambia upatikanaji wa vitabu vya Biblia ulipatikana kwa uweza wa Roho mtakatifu....

Kazi kwelikweli
 
Huwa siangalii ukweli ama uongo binafsi naangalia uhalisia mantiki na uwiano...hivyo ni vipimo muhimu kwangu kwenye andishi lolote...
Dhana za uongo na ukweli zina mapungufu mengi kwakuwa ukweli wa imani A unaweza kuwa ni uongo wa imani B ....
 
Ndiyo hivyo tena mkuu tatizo limeshatokea na hakuna namna kwa watu wenyewe kupata ufumbuzi,ndiyo maana najiuliza kama Mungu ameacha tu mvurugano huu uwe tu kama ulivyo?
 
Ila mkuu dhambi ile ya daudi ambayo hata kwenye biblia iliandikwa tumeona pia adhabu aliyopewa Daudi na alikemewa juu ya hiyo dhambi ila hiyo dhambi nyingine sijaona Nabii gani alienda kumkemea na adhabu yake ilikua ipi?
 
Ndiyo hivyo tena mkuu tatizo limeshatokea na hakuna namna kwa watu wenyewe kupata ufumbuzi,ndiyo maana najiuliza kama Mungu ameacha tu mvurugano huu uwe tu kama ulivyo?
Mungu alijua hili litatokea ndio maana alitoa hukumu kupitia kitabu cha ufunuo ambacho alisema adhabu ipo kwa atakayeongeza au kupunguza neno lolote la Mungu.... Hivyo naamini mchakato mzima watu walitumia akili zao kuamua kitabu kipi kikae kipi kitolewe ila leo hii ukihoji wanasema WALIONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.... Sasa unabaki kujiuliza je kivp Roho MTAKATIFU aongoze Biblia kukinzana kila dhehebu.

Ila naamini ukweli utapatikana cku moja
 
Ila mkuu dhambi ile ya daudi ambayo hata kwenye biblia iliandikwa tumeona pia adhabu aliyopewa Daudi na alikemewa juu ya hiyo dhambi ila hiyo dhambi nyingine sijaona Nabii gani alienda kumkemea na adhabu yake ilikua ipi?
Mkuu hoja yangu sio kama Daudi alikuwa shoga au lah na haijawahi kuwa hoja yangu nachopinga ni mtu mmoja kusema DAUDI HAWEZI.... Yaani hana capacity ya kufanya dhambi ndio nikatolea mfano kwamba kama aliweza kufanya uzinzi kwa kutamani mke wa mtu je hawezi fanya dhambi zingine za uzinzi??

Nachodebate hapa ni UWEZEKANO wa daudi kufanya type B ya uzinzi kama alishafanya uzinzi type A..... Je unaonaje?? Alikuwa na uwezo huo (bila kujali kama aliwahi kumlala jonathan ama lah).
 
mkuu unapotaja watumishi wa Mungu unatakiwa uwe very specific au tutakuuliza mtumishi wa Mungu yupi? Mzee wa upako si mtumishi wa Mungu ninaye mjua. si kila Mhubiri wa Injili ni mtumishi wa Mungu. Yeye huyo anayejiita mzee wa miupako ni muubiri wa Injili tu kama Masanja Mkandamizaji wala si mtumishi wa Mungu. Na ukikubali kuwa jamaa uliyemtaja ni mhubiri wa injili na unafahamu wapo wanaohubiri kwa hila jibu unalo.
 
Dhambi Kama binadamu anaweza akawa ameifanya labda ya hasira au Aina nyingine ya Dhambi Ila sio dhambi ya Uzinzi au ya ulawiti kwani baada ya Daudi kufanya kosa Mungu akamtuma Nabii Nathani aende kumwambia Daudi dhambi alilolifanya kuwa lilikua chukizo mbele za BWANA na tunaona mshahara wa ile dhambi ulivyokua Soma 2Samweli 12:1-18 .

Swali iwezekaneje Daudi amlale Nabii Wa BWANA Nathan?? Yani unaona kabisa dots haziunganishiki! Maana Mungu ile dhambi aliijibu kwa mapigo makubwa kwa Daudi Soma izo haya nilizoweka utaona.

Ila pia Kama nikikubali alitenda iyo dhambi Basi tukubaliane pia Daudi ufalme wake ulifutwa na pia yupo jehanamu anaangamia kwenye Moto wa milele.
 
Haya maandiko unapoyasoma
changanya na akili yako
Ikiwa muumini kweli,Basi ogopa kumnyoosha aliechaguliwa/kuteuliwa na Mola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…