Mkuu
mitale na midimu nimekuelewa hoja yako ila labda nigusie mambo machache
1. Unaposema kuwa hakatazwi mtu kuquote "nje ya Biblia"as long as unaangalia context..... Je ni wakati gani ambapo manabii walijua Biblia inasema A na wao wakaandika B ilihali mpaka Yesu anakuja hakukuwa na standard bible?? Nachojua ni kwamba baada ya wote kuandika ndio wakatokea watu miaka 300 baadae wakasema huyu anakinzana na huyu ndio maana vikatolewa na vingine vikaachwa Ndio kina Enock na Mwandishi wa Jasher na vitabu vingine vya kufanana wakawa victims wa hilo tokea mwanzo kabisa.
Kuhusu kuquote nachojiuliza sio tu kwa kuangalia muktadha ila Biblia mfano kwa story ya Daudi inasema historia ya Daudi MWANZO MWISHO na hata Rehoboam MWANZO MWISHO vimeandikwa kwenye kitabu cha Gadi n.k sasa je hapo nikienda kusoma na nikagundua inconsistency juu ya story ya daudi katika kitabu cha samweli/wafalme na kitabu cha gadi/Nathan je ntakuwa nina makosa kushikilia msimamo wa kitabu hicho???
2. Mkuu wanaosema vimepotea sio mimi ni hao hao waliocompile Biblia kuna apokrifa zilikuwa termed as LOST BOOKS yaani vilipotea katika uso wa dunia mfano kitabu cha shemaya kipo katika kundi hilo na ushahidi wote wa kiachiolojia unaonyesha manuscript zake zilishapotea kitambo unless una ushahidi mwingine kuwa Manuscript za book of shemaya,Gadi na Nathan bado vipo unaweza kutusaidia mkuu.
3. Mkuu kuhusu uandishi hilo jambo halipo kwenye Book of Enock pekee hata Wimbo ulio bora au barua kama 7 za paulo ni pseudepigrapha yaani havina ushahidi kuwa viliandikwa na paulo au paulo maana vimeandikwa vingi baada ya kifo cha paulo..... Mfano waebrania ni pseudepigrapha ila kwenye bible kipo hivyo sidhani kama hoja hii ya uandishi au backdating ya apokeifa ina mashiko tena hasa ukizingatia backdating/auhtorship crisis hata ndani ya Bible vipo according to theologians.
Ubarikiwe