Vituko vya X zangu, Siku ya Harusi yangu

Keagan Paul

JF-Expert Member
Jul 19, 2018
500
3,058
Hata kabla sijatangaza kuwa naoa, nilikuwa na hofu kuhusu Ma X zangu wawili, nilijua kutokana na Ukaribu wa familia zetu lazima habari zingewafikia na lazima wangekuwepo siku ya Harusi yangu.

Kilichokuwa kikinipa mawazo ni kwamba hawa Ma X zangu hatukuachana vizuri. Halafu akili zao mbovu nazijua. Baadhi ya wana, familia na Marafiki walikuwa wakiwajua.

Mfano, mmoja Kati yao ilinibidi niachane nae kinguvu mwezi mmoja kabla ya Kutangaza Kikao cha Kwanza cha Harusi. Alivyosikia naoa alinipigia simu na kuniahidi lazima atakuja kufanya varangati, nakumbuka alinipigia simu na kuniambia “Wewe si kidume, Jiandae kudhalilika Baba”

Nikiri wazi kuwa huyu demu alikuwa akinipenda sana, hata kuachana kwetu nilifanya kazi sana, hakuridhika.

Kwa hiyo wakati wote wa Vikao, hili swala lilikuwa likinipa vimawazo vya hapa na pale. Nilijua lazima watakuwepo, Je nitawakabili kwa macho ya aina gani pale mbele? Hawa mademu wao walikuwa hawajuani.

Huyo mwengine sikuwa na hofu nae sana sababu nilijua siku ya harusi lazima wazazi wake watakuwepo, kwa hiyo niliamini hatoweza kufanya drama mbele ya wazazi wake, lakini pia kwa heshima ya kazi yake Serikalini niliamini asingeweza kufanya utoto wowote. Nilijipa moyo.

Ebhana siku hazigandi, mara siku ya harusi ikafika. Kuondoa mawazo na ile aibu, tulivyotoka tu Kanisani na Bibie, kwenye gari tuliyopanda kuna mhuni wangu mmoja nilimwambia aniwekee Serengeti Light za Kutosha kwenye gari.

Wakati tupo Beach watu wanapiga mapicha, Mimi akili yangu haikuwepo pale kabisa, nilikuwa natoka narudi, natoka narudi hadi kwenye gari, nakunywa pombe zangu kwa siri kisha narudi kupiga picha, nakumbuka mpaka Dereva wetu alinishangaa. Nakumbuka aliniambia “Vipi Mzee uko sawa, angalia usije Kuzima”

Kwa kifupi nilikuwa nawawaza sana wale mademu. Kila muda ulivyosogea hofu ilinizidi, Tukamaliza kupiga mapicha picha pale hao, safari hadi Ukumbini.

Ule muda tunasubiri watu wote waingie Ukumbini ndo Maharusi tushuke kwenye gari, Mimi nilikuwa busy kunywa pombe zangu. Mpaka wife alikuwa ananishangaa. Nilikuwa na mdanganya kuwa bila kunywa pombe sitaweza kucheza mziki vizuri mbele za watu. Aliniamini.

Mara ule muda wa maharusi kuingia ukumbini ukawadia. Hao tukaingia huku tunacheza. Watu wote walikuwa wamesimama kutushangilia maharusi. Baada ya kuzipita Meza kama mbili tatu, Macho yangu yakatua kwa X wa kwanza, yule Mfanyakazi wa Serikali, kutokana na pombe nilizokuwa nazo kichwani sikujali sana, nikajikaza.

Kufika mbele, bado nikiwa na Bibie tunacheza nashangaa X wangu wa Pili amekaa kwenye Meza Kuu ya Wazazi wangu. Dah

Inaendelea
 
Sawa tunasubiria kikombe cha pili.

kermit.gif

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
😂
 
Hata kama chai ila nimeikubali.
Na kuna ka experience kaukwel kabisa mfano, mara nyingi sama maharusi huwa hatu enjoy ile siku ya harusi (kwa wale ambao hatujaoana kwa show off). Mara zote vichwa vinakua concerned sana kufikiri hii shughul iende kama mipango ilivyokua imalizike ujue limeisha maana daah mambo ya harus huwa yana heka heka sanaaa.

Yan wengine wanafurahia mikuku minyama nyie akil zenu zinawaza ngoma hii iishe fasta tuendelee na maisha.
Hapo over overspendimg nje ya bajet unajua tu hapa sijui kamat itakua na figure gan huko! 😂😂.

Aman yetu mara nyingi ni baada ya harusi ndio angalau mnajitafutia ka moment kenu ka ku rewind shangwe ambalo hamkulifaid
 
Na hii siku ndio ma x hufanya juu chini watudishe upendo. Wanakatika hadi unahisi umekosea kuoa.
 
X akae kwenye viti vya wazazi wa bwana harusi? Y kwanini?
Mleta uzi unajipanga kuleta uongo mwingine.
Acha hizo asiee..
Unamaliza mwaka kwa uongo aisee))
 
Back
Top Bottom