Biashara ya samaki

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,519
1,825


Wakuu kwa mtu yeyote mwenye ujuzi kuhusu biashara hii hasa samaki wa maji baridi huko Dodoma.

Soko lake vipi lina upinzani mkubwa?

Mimi niko Mbeya. Nawasilisha kwa salamu na shukrani kwenu!


WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUJUA KUHUSU BIASHARA HII

MICHANGO YA WADAU KUHUSU BIASHARA YA SAMAKI

 
Inalipa sana inategemea unawatoa wapi? Kama ni mtera inakuwa poa sana hata bei yake inalipa kiasi.
 
Inalipa sana inategemea unawatoa wapi? Kama ni mtera inakuwa poa sana hata bei yake inalipa kiasi.

Nashukuru Sana Mkuu
Mimi Nimepanga Kuwatoa Ziwa Nyasa(mbeya)
Sababu Ndiko Niliko
Ila Kama Ulivyosema Mtera,itabidi Niangalie Inakuwaje!
 
Nashukuru Sana Mkuu
Mimi Nimepanga Kuwatoa Ziwa Nyasa(mbeya)
Sababu Ndiko Niliko
Ila Kama Ulivyosema Mtera,itabidi Niangalie Inakuwaje!

Mkuu watu wa Mbeya, Njombe na Ruvuma wako wengi tu DAR na wengine tumeoa huko na tungependa sana kupata samaki toka Ziwa Nyasa. Binafsi sijawahi kuona au sijuwi sehemu yeyote DAR panapouzwa samaki toka ziwa Nyasa kama vile Mbasa, mbelele n.k bila kuwasahau dagaa wake watamu. Nafikiri kwa DAR inaweza kulipa zaidi maana hata access yake ni rahisi kuliko DOM.
 

Mkuu Nimekupata Sana Sikulijua Hilo

Kiukweli Samaki Hawa Ni Wazuri Ila Changamoto Ni Uhifadhi Mpaka Ziweze Kufika DAR
shukran Sana Mkuu

Tafadhari Naomba Mawasiliano Yako

Vilevile Kama Kuna Mtu Anajua Soko La Samaki Hawa Kwa Hapo DAR kama Lipo,nahitaji Mchango Wenu!
 

Mkuu ushauri wangu ni kuwa unaweza kufika DAR ukajaribu kuzunguka kwenye mabucha/maduka ya kuuza samaki. Ongea nao wewe waweza kuwa supplier wao tu. Kama una mpango wa kufungua duka lako mwenyewe basi inabidi ujuwe sehemu ambayo idadi ya wakazi wa Songea/Mbeya ni kubwa ili uweze kupata wateja kwa haraka.

Wazoefu wa DAR wanaweza kutuambia hapa maana DAR imegawanyika japo si mgawanyo rasmi. Kwamfano ukitaka wachaga wengi utawapata Kimara, Wakurya utawapata Kipunguni na Kitunda, wasukuma utawapata Vingunguti na Kigamboni. Japo najua watu wa Songea unaweza kuwapa kwa wingi Mabibo huenda kuna sehemu nyingine waliko wengi zaidi.

Biashara ikishakuwa unaweza sasa kufungua matawi sehemu zingine. Soko ni kubwa tu na familia yangu tutakuwa wateja wako wa kudumu.
 

Shukrani sana mkuu kwa kunipa Mori Na Ushauri Makini,nitayafanyia Kazi!

Nafikiria Namna Ya Kuwahifadhi Samaki Mpaka Kufika Kwenye hzo Bucha Kubwa Bila Kupoteza Ubora Wake.

Sababu Barafu Sijazipa % kutokana Na Changamoto Za Usafiri!
 
Wakuu,
Kwa wale wataalam wa biashara ya samaki wabichi naomba mwongozo wenu wa namna ya kuendesha hiyo biashara.
  1. Ni kiasi gani cha mtaji kinahitajika?
  2. Ni wapi ambapo soko ni zuri kwa biashara hizi?
  3. Kuna tofauti yoyote ya biashara hizo za samaki wabichi kutegemeaa na maeneo ya bishara?
  4. Mambo gani ya muhimu nahitajika kuzingatia?
Naombeni maoni na ushauri pia.
Asanteni.
 
Mkuu unalitumia vizuri jamvi, kila la heri mkuu katika mipango yako ya kujitanua kibiashara!
 
Mkuu ungefunguka wanauwa nje ya Nchi wapi? Ulaya au Uganda, Kenya, ninavyo jua wana uzwa Ulaya ni waleSangara na huwa wamekwisha procesisia tiyali, jena wewe una process?
 
Greetings! Shikamoo! Habari zenu wanajamii!
Mimi nipo Bukoba najihusisha na biashara ya samaki. Kwa hivi sasa nahitaji business partner. Samaki wanauzwa nje ya nchi. Details zaidi ni kwa wale wako interested only. Mtaji ni Tshmil 4 kuendelea.

Samaki wa aina gani? Sato au Sangara.
 
Mkuu ungefunguka wanauwa nje ya Nchi wapi? Ulaya au Uganda, Kenya, ninavyo jua wana uzwa Ulaya ni waleSangara na huwa wamekwisha procesisia tiyali, jena wewe una process?

Samaki wa aina gani? Sato au Sangara.

May be kwa sababu amesema waliokuwa interested wamtafute,labda anataka tupige naye story za chemba ndio atafungukia huko.Si mnaona amepost tu kisha akatokomea kizani.Na hii inanitia hofu ikiwa kweli yuko serious kweli.
 
Hizi taarifa Mh!

scam@work!

siku hizi nasikia bukoba kuwa matapeli wengi sana sijui kwa nini? wadau kuwa makini!
 
Greetings! Shikamoo! Habari zenu wanajamii!
Mimi nipo Bukoba najihusisha na biashara ya samaki. Kwa hivi sasa nahitaji business partner. Samaki wanauzwa nje ya nchi. Details zaidi ni kwa wale wako interested only. Mtaji ni Tshmil 4 kuendelea.
Greetings!

Nauza set nzima ya star times decoder, aerial na cable yake ya 20m. Price 80,000. Haina matatizo yeyote. Nipo Dar es salaam. Asante.
wajingawatu upo arusha? Ni PM nina biashara
Tunakodisha machine ya hydraform ya kutengeneza matofali kwa kutumia udongo. Pia tunaye mtaalam wa kuyatengeneza kama utamhitaji.

Ona post za huyo mjasiriamali!
 
Kijana anatafuta mtaji, yawezekana anayo idea nzuri ya biashara ila mtaji ndo unagomba.
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…