Biashara ya samaki

Mwenye kujua a to z ya hii biashara atupe madini
Mfano uumesema kilo 8,000/= wakati hapa arusha yenyewe kilo ni 8,000/= hiyo faida anaipataje
 
Mwenye kujua a to z ya hii biashara atupe madini
Mfano uumesema kilo 8,000/= wakati hapa arusha yenyewe kilo ni 8,000/= hiyo faida anaipataje
Naomba tu wakienda huko warudi kutupa feedback, biashara ya samaki wa ziwa victoria imeharibiwa ni takribani miezi 6 hukusikia majuzi ATCL walichelewesha mizigo ya abiria toka bukoba to mza to dsm ilikuwa inasachiwa kama wamebeba samaki wanasema wafanyakazi wao wanabeba,kuna vita eti sangara wadogo wanavuliwa
 
  • Thanks
Reactions: etb
naomba tu wakienda huko warudi kutupa feedback,biashara ya samaki wa ziwa victoria imeharibiwa ni takribani miezi 6 hukusikia majuzi ATCL walichelewesha mizigo ya abiria toka bukoba to mza to dsm ilikuwa inasachiwa kama wamebeba samaki wanasema wafanyakazi wao wanabeba,kuna vita eti sangara wadogo wanavuliwa
Aysee... Nlisikia ile ya Dom walipokuwa wanapima kwa rula walopikwa tayari! Kwa hyo ishakuwa ka bange
 
habari zenu wadau ,,,nataka nifanye biashara ya samaki aina ya sangara na sato toka mwanza naleta dar es salaam ,nmefuatiria mambo yote yanayohusiana na biashara hii ila nakwama sehemu mja tu ya kuhifadhia mzigo(freezer) kwani kiasi cha pesa nilichonacho hakitoshi kufanya yote .Naomba msaada wenu kama kuna mtu mwenye freezer na yuko tayar kufanya hii biashara anichek 0745703651 na pia kama kuna mtu anahitaji samaki anitafute kwenye namba yangu hapo juu


Naomba msaada wenu

Hupatikani
 
Kweli kabisa ni kuamua tu
Mkuu kila biashara ni ngumu na ni rahisi kwa upande mwingine! Ni maamuzi binafsi tu! Personally nawafahamu watu wanaofanya hii biashara na wanafanya vizuri sana!

Kitu kikubwa ni kuwa unahitaji kuwa na uelewa wa kutosha. Elimu ya hapa jf pekee haitoshi,you need some field experience. It matters the most.
 
UZOEFU KATIKA UVUAJI NA UUZAJI WA SAMAKI

Mimi Nimevua SANGARA ziwa Victoria, Sato tulikuwa tukiwakamata mara chache kwasababu tulikuwa tuna vua maji ya kina kirefu.

Mimi nimewahi kuvua ziwa Victoria kisiwa cha kome na visiwa jirani huko. Biashara ya uvuvi siyo rahisi na siyo ngumu. Urahisi wa biashara hii ikiwa wewe mwenye mtaji utaamua kuishi kambini na wavuvi wako, ukisimamia ukiwa site kabisa, yani anzisha kambi, wavuvi wengi tu, wanakuja wenyewe mnaanza kazi.

Malipo inategemea na wewe mwenyewe, unaweza kuwaliapa pesa, au ukawapa siku zao za uvuvi kama sehemu ya malipo yao. Yaani wanakuvulia Jumatatu mpaka Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wanavua lakini nizao au ndio malipo yao, wakipata sawa wakikosa pia wanelewa. Ila gharama za kuwalisha ni zako mwenye kambi, unanunua Unga tu, samaki wanapatikana ziwani kama kitoweo.

Unaweza ukawa unauza samaki wabichi, kwa wamiliki wa viwanda au kuna wachuuzi wa wenye viwanda wanazunguka na mzani wananunua na kupeleka kiwandani, ama unaweza wachana samaki ukawatia chumvi na kuwakausha juani kule wanaitwa Kayabo, soko lao ni Zaire, na Zambia kwa sana.

Unahitaji kuwa na mitumbwi ya kuvulia kadhaa kutokana na mtaji wako na mahitaji yako, unahitaji kuwa na Injini za boti atleast Mbili. Kwasababu unahitaji pia kufanya doria ya nyavu zako, wavuvi ni wezi kama ilivyo kwa sehemu zingine, kama huna speed bot na hufanyi doria, hao hao wavuvi wako wanongea na wenzao wa maeneo mengine wanakuja kukuibia nyavu zote.Lakini wakijua una speed boti na unafanya doria pia umiliki bunduki wataogopa. Nimefanya kazi hizo za usimamizi miaka mingi kidogo imepita lakini huo ni uzoefu nilio upata huko.

Najua uzi huu labda ume expire lakini niliona ni shere labda uhitaji bado upo.

Naomba kuwasilisha.
 
mkuu nikwambie tuu biashara ya uvuvi hawezi mtu mwenye kipato kidogo ka wewe kipato chako ni kidogo hutoiweza maana ile boti yakununua ni kama milion 25 kulingana yakutengeneza nadhani itakuwa chini ila sidhani ka itakuwa chini ya milion 10 alafu unapaswa kununua vifaa vya kuvulia,niliwahi kufuatilia hii biashara mwaka 2014 baada yakuona gharama ni kubwa navile nilikuwa ni wakuziunga unga na vile niliogopa risk nikakimbia, but mwaka 2017 niliwahi kukaa na wavuvi wakaniambia inalipa wakanipa hesabu zao zinaridhisha kiuhalisia, wale wa hesabu pia niliwahi kukaa nao wenyewe wakivua wanakuja kuua then wanatoa gharama za mafuta wanatoa hela ya bosi then nyingine wanagawana ila wakasema sikuwakipata kikubwa boss anakula kikubwa kidogo nae anakula kidogo but hesabu inaweza kufika 700,000 mpaka 1000 000 but wanaweza kukaa kwenye maji mpaka wiki. but hizo faida ni kwa zile boti ndogo za kutengeneza hapa home

sijui sana kiundani ila kwahayo nidhani yanaweza kukupa kitu flani
 
usithubutu,utalizwa hiyo biashara mwanza ishakuwa kama biashaara ya cocaine,usumbufu kila kona
Ni kweli kwa sasa sifa zimeharibu, hii si biashara ya kufanya ukinunua mzigo utakuozea mikononi mwenye basi hata umpe laki 4 habebi samaki. Ni rahisi kusafirisha bange kuliko samaki na dagaa wa ziwa Victoria
 
mbona kila wiki samaki wanakuja dar es salaam kutokea mwanza ...samaki wanaokamatwa ni ambao wapo chini ya kiwango cha serikali ...kama samaki amekizi viwango hawezi kukamatwa
Ni kweli kwa sasa sifa zimeharibu, hii si biashara ya kufanya ukinunua mzigo utakuozea mikononi mwenye basi hata umpe laki 4 habebi samaki. Ni rahisi kusafirisha bange kuliko samaki na dagaa wa ziwa Victoria
 
Ni kweli kwa sasa sifa zimeharibu, hii si biashara ya kufanya ukinunua mzigo utakuozea mikononi mwenye basi hata umpe laki 4 habebi samaki. Ni rahisi kusafirisha bange kuliko samaki na dagaa wa ziwa Victoria
wanabisha wachangiaji hapo juu,tusubiri feedabck watu wanaenda kulizwa soon
 
Kwa anayehitaji fillet(Samaki ambao hawana mifupa) niwe nafanya nae biashara. Njoo PM tuzungumze
 
Habari zenu wan JF,

Kama kichwa cha habari kinavyoonekana, Naombeni mnisadie jinsi ya kusafirisha samaki kwenye ndege kutoka mwanza kuja Dar.

Ni vitu gani natakiwa niwenavyo ili nipate ruksa ya kusafirisha mzigo wangu ?
 
Back
Top Bottom