Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Tuwe tunafanya utafiti kabla hatujakosoa post za watu, kuna hadi taarifa kwamba kuna mtiki umewahi uzwa hadi $20,000!.kwa bei nyingi wana state $500 kwa cubic mita ambapo mti mmoja unaifikia na kupita, hapo bado hujauza maranda kama veneer, tatizo letu hatupendi kutafiti , bila shaka european union wasingewekeza $29million kama isingekuwa na hela nzuri, ukiachana na hayo nilisoma kwenye kijarida cha mazingira huko kilwa kuna kijiji walikuwa wanauza magogo kwa Tsh 1.2miliioni, biashara ya magogo ina hela mno ndio maana yule mtoto wa nguema ni tajiri sana.

Nashukuru kwa maelezo. Tunaomba source ya data. Bado hainiingii kichwani mtiki mmoja kuuzwa $20,000 (ambazo ni Tshs zaidi ya milioni 30!). By the way tunapanda mitiki Morogoro hivi tunavyoongea.
 
Nashukuru kwa maelezo. Tunaomba source ya data. Bado hainiingii kichwani mtiki mmoja kuuzwa $20,000 (ambazo ni Tshs zaidi ya milioni 30!). By the way tunapanda mitiki Morogoro hivi tunavyoongea.
Hongera kwa kupanda mitiki, vipi unapanda miche mingapi? Source just google price of teak tree utapata nyingi tu, uje unijulishe tafadhali.
 
Jamaa mimi namjua wanawahonga watu wa maliasili porini na wanakata sababu ya bishara ya mbao. Wana mashine zao kabisa and he makes serious money. Is this legal?
 
Hongera kwa kupanda mitiki, vipi unapanda miche mingapi? source just google price of teak tree utapata nyingi tu, uje unijulishe tafadhali.

Kuna sources nyingi sana kwenye internet ila nafikiri tunaongelea vitu viwili tofauti. Mimi naongelea bei ya mti shambani siongelei bei ya mbao ulaya iliyokuwa processed tayari. Data zipo wizara ya maliasili na utalii na ni juu sana ila ni kwa miti iliyopandwa miaka hamsini iliyopita na serikali.

Zinaonyesha bei za juu ila ni za kwenye makaratasi tu (za kisiasa for strategic planning). Nafikiri cha muhimu ni kuanzia na baseline data. Kama una mitiki kwenye uwanja wako Dar, halafu serikali ikakufidia kupanua barabara au kuendeleza hilo eneo, utalipwa kiasi gani? Hiyo ndio bei nzuri ya kutumia kwenye kufanya analysis kwa sababu hata wataalamu wengi ukiwauliza bei wanakwambia hakuna soko la ndani ni la nje tu. Kama utapata mtu ameuza mitiki hapa Tanzania shambani naomba utujulishe miti ilikuwa na umri gani na iliuzwa kiasi gani kwa ujazo au kwa mti.

Tumeanza na trial ya miti 600 kwenye ekari moja tuone kama itakwenda vizuri mwaka ujao tutaingia kwa gia kubwa. Mbegu tunanunua SUA, shs 1,000 kwa mche. Ila mvua zinatusumbua.

Nawasilisha.
 
Miaka isitukatishe tamaa unaanza kula toka kipindi unafanya thinning labda 7-10 years. hii miti pamoja na mipingo wanatumia kutengeneza vifaa vya muziki ndio maana vipo ghali sana kama piano.
 
FAQ about teak investments ni ngumu kupata data za bongo lakini hapa nimepata data kwamba mti wa 25 years in costa rica worth $1000 ni mti sio mbao.

Nakubaliana na wewe kuhusu hizo bei za nje. Bei za ndani zipo ila ni ya miti iliyokomaa sana, iliyopandwa na serikali miaka ya hamsini na sitini. Mimi nimetafuta bei na nina connections za very effective people huko serikalini wanaofanya kazi za misitu ila majibu hayapo consistent. Pia kumbuka miti ya miaka 25 sehemu moja ni tofauti na sehemu nyingine. Kwa mfano pines za miaka 15 za sehemu za baridi na mvua nyingi ni tofauti mno na sehemu isiyo na mvua ya kutosha sababu ya tofauti ya growth rate.

Kuna tetesi ya mpango wa kujenga kiwanda cha kuchonga na ku process mitiki sehemu za Morogoro (ni tetesi sina uhakika, kama sikosei karibu na Ifakara) na nilichoambiwa ni kuwa kukishakuwa na hicho kiwanda bei ya soko la ndani litafahamika vizuri. Hili swala la bei ya mitiki tumeliulizia hapa miaka kadhaa angalia hii thread ila majibu ya bei ya ndani ni tatizo Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe - JamiiForums

Nafikiri cha muhimu ni kupambana tu. Data za serikali zinakadiria kuwa ekari moja ya mitiki inaweza kutunzwa kwa milioni 40 kwa miaka ishirini. Mimi sio mtaalamu, ila wataalamu wanasema baada ya muda fulani unahitaji kufanya thinning ili kuongeza urefu na basal area. Hiyo inamaanisha kuwa by the time unavuna utakuwa na chini ya miti 300 kwa ekari. Kwa gharama hizo inamaanisha gharama za utunzaji wa mti mmoja ni zaidi ya laki moja kwa miaka 20. Hii ni estimate ya wizara.

Kuna blog inaitwa MITIKI -KILIMO KWANZA miaka kadhaa iliyopita iliweka information za jinsi ya kuitunza na huyo jamaa anaweza kukusaidia cha kufanya ukimpigia simu. Ila wakati najadili naye bei ilikuwa bado haieleweki vizuri.

Red Giant ninashukuru kwa muda wako. Tuendelee kufanya huu utafiti, ni eneo ambalo nataka kuwekeza ila tunaenda kwa tahadhari kwa sababu watu wengi ikiwepo wa serikalini wanakueleza mitiki ni gharama ila wanapanda pines kama sisi. Itasaidia sana tukipata stumpage price, i.e., the price paid for trees as they stand in the forest. Mimi sio mtaalamu kama nilivyoidhinisha hapo awali ila kuna miti mingi ambayo ni ghali kuliko hiyo mitiki ukitumia bei za nje ila bei za ndani zingetusaidia kujua tutegemee nini, especially kwa sababu tunaongelea kuwekeza sasa hivi na kufaidika robo karne toka sasa.

Nawasilisha.
 
hii mitiki(teak) inachukua muda mrefu sana kuwa na bei nzuri ni ya miaka 15 na kuendelea, ila ukiwa unafanya thining ya shamba unaanza kuuza kuanzia miaka saba, na ina hela mti unaweza fika hadi milioni moja(wanatumia kwa nguzo za umeme ,kujenga meli na fenicha za gharama) , kuhusu mbegu sifahamu ila european union wanafadhili mradi huko kilombero nasikia tayari wana hekta 3000

Safi sana mkuu kwa maelezo yako, napenda sana project ya hii miti, niliulizia huko dar mche m1 sh 3000, sasa sijui mkoa wanauza kiasi gani?
 
Ndugu tiro je wannakijiji wanauzajee eka mmoja ya shamba lilopandwa miti. Je, kwa eka kuna kuwa na miti kiasi gani na aina gani ya miti? Ndugu kmv je nikitaka kupata shamba angalau eka Mia moja nzuri ni maeneo gani naweza kupata?

Natanguliza shukrani.
 
Great topic, wadau naweza pata wapi miti aina ya Mitiki kwa bei nafuu nahitaji kama 300 hivi.
Nimeiona inakuwa vizuri kimbiji huko kigamboni.
 
Great topic , wadau naweza pata wapi miti aina ya Mitiki kwa bei nafuu nahitaji kama 300 hivi.
Nimeiona inakuwa vizuri kimbiji huko kigamboni.

Bei zinatofautiana sana kwa sababu zifuatazo. Ubora wa miche, location na muuzaji mwenyewe alivyoipata. Jana nimenunua Tabata Aroma pale, bei ni Tsh 1000/ kwa mche, nikaacha kununua Mbagala mwisho pale jamaa anauza 500/ kwa mche sababu ya ubora. Pia niliacha kununua Mkuranga mjini kwa sababu ya bei kuwa kubwa, ni Sh 3000/ kwa mche. Wastani wa bei ni Tsh 400/ mpaka 4000/ kwa mche.

Pia waweza tumia cuttings, kila cutting moja huuzwa Tsh 200/ na inasafirishwa toka Tanga. Hii njia ni nzuri kama una large scale na mvua zipo. Ila kwa mwaka huu mvua ni magumashi, usijaribu labda huko Tanga ambako mvua ziko.
 
Assante kwa majibu yako;

Natumaini unafahamu kuwa tuna umoja wetu wa misitu wengi wetu ni members was jamiiforums. Kama hufahamu ningependa tuwasiliane ili ufahamu tunafanya nini na jinsi ya kuweza kuwasiliana. Organizer wetu ni Malila na tumepanda mamia ya ekari msimu huu. Na baadhi wamekuwa wakinunua mashamba ya wanakijiji ya ekari chache.

Kama hufahamu kuhusu umoja wetu wa misitu na ungependa kujua tunachofanya wasiliana na Malila ili tuweze ku share information.

Asante.

Asante sana,
Nilikuwa porini huko na vijana. Ngoja nipitie huu uzi vizuri ili nichangie kiasi pale ninapoweza.
 
QUOTE=kakaamiye;3629943]Ninashukuru sana kwa hii topic,hata mimi nipo interested sana na kupanda miti na ni idea ya muda sasa, issue kwangu ni namna ya kuanza especially kupata shamba kwa ajili ya kupanda.Ningeomba kupata japo idea kama ninaweza kupata eneo huko njombe na kwinginekoukizingatia mimi ninaishi dar. Na price inakuwaje, pia gharama za miche kwasasa ni kiasi gani na kuotesha plus kutunza. Please please mwenye dataninaomba

Wasiliana na Malila, ni memba humu, mtafute
All the best mkuu.
[/QUOTE]

Asante, nipo nimejaa tele.
 
Asante KVM,

Nichangie kwa kuleta nyongeza za hapa na pale ili kujazia mjadala wetu. Maeneo ya kupanda miti yaliyosahaulika ni Kilolo, Mfindi,Mby vijijini, Makonde plateau.

Tumetaja sana pines, cyprus, teak,eucalyptus, tumesahau acrocarpus kwa ukanda wa baridi na Msederela kwa kanda za joto kiasi.

Hatujazungumzia mbegu, mbegu bora za Pines kwa sasa ni Tatizo sugu.Tangu mwaka jana kituo cha Iringa wameshindwa kuzalisha, kwa hiyo pines/cyprus zinaandaliwa kienyeji na vijana huko vijijini. Kwa sasa pines za uhakika zinapatikana Nairobi, ila bei imesimama.

Mwaka jana tulipata taabu sana ya tubes, ila mwaka huu walau zipo pale TFA Iringa, bei iko juu. Ukiwa na usafiri wako, ni bora kununua Dar ukasafirisha. Dar ni Tsh 5000/ kwa kilo na TFA Iringa ni 6500/ kwa kilo.

Ili kupunguza gharama za kitalu, watika miche mapema, miezi mitano kabla ya msimu wa kupanda haujafika.

Kama unataka ardhi kubwa,Makete usiende, ni kazi ngumu kupata eka 50 za pamoja zinazofikiwa na miundo mbinu. Utapanda milimani ambako utashindwa kuvuna. Na maeneo mazuri yaliyobaki bei iko juu. Ludewa/Wino/Lupembe/Mfindi kusini huko bei poa.Kilolo bei inaanza kupanda.

Kwa wale wanaonunua miti na ardhi, wawe waangalifu, vijijini unaweza kuta miti ni mtu mwingine na ardhi ni ya mtu mwingine.

Asante, tuendelee kukata issue.
 
Back
Top Bottom