Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Biashara ya mbao inalipa sana aisee ndungu. Namjua jamaa yangu mmoja anafanya na rafiki yake. Nimeongea nae jana tu aliniambia wanaenda kijijini.
 
Mkuu safi sana nimeipenda sana project yako pamoja na ng'ombe wazuri wa kienyeji. Karibu sana hapo juu kwenye jukwaa la ujasiriamali kuna nondo za kutosha, NB kuna thread yetu initwa "Kwenu kinaota/kinamea au kustawi kitu gani?" tulijadili pia miti ya mbao karibu kwenye mjadala.
 
Kilimo Kwanza in the move. Nimeipenda sana hii topic. Alijisemea Mwalimu Kilimo ni uti wa mgongo ni kweli kabisa. Shukrani mkuu kwa mada hii.
 
Mkubwa, umetisha sana kwa kweli. Haya ndiyo mambo tunapaswa kufanya ili kujinasua na pingu za ajira, na kwa wale tunaoanza kuchungulia anga hizo za ujasiriamali basi wewe ni mmoja wa WAALIMU wetu.

Ahsante sana kwa mchango wako na usiishie hapo, endelea kutoa darasa based on your experience.
 
Mi hii biashara nimeishtukia ila tatizo nikupata maeneo ya kupanda miti maeneo mengi yameshwa panda mi nacho kifanya sasa nanua maeneo kwa wenyeji wanauza pamoja na miti.
 
Kuna miti inaitwa mitiki,hii vipi kupanda mpaka kuvuna inachukua miaka mingapi? Je hizo pines na eucalyptus nikipanda kwenye heka 10 ninunue miche mingapi? Au unaweza kunisaidia kupanda miche ya hekari kumi?
Hii mitiki (teak) inachukua muda mrefu sana kuwa na bei nzuri ni ya miaka 15 na kuendelea, ila ukiwa unafanya thining ya shamba unaanza kuuza kuanzia miaka saba, na ina hela mti unaweza fika hadi milioni moja (wanatumia kwa nguzo za umeme, kujenga meli na fenicha za gharama), kuhusu mbegu sifahamu ila european union wanafadhili mradi huko kilombero nasikia tayari wana hekta 3000.
 
Aisee hizi taarifa ni za muhimu sana,tuna eneo moshi karibu heka kumi sijajua naweza kupata wapi taarifa za miti itakayochukua muda wa wastani chini ya miaka kumi ili nipande, miti baadhi iliyopo ni cyprus ila naona kama inachukua miaka mingi mno,kama naweza kunisaidia ushauri.
 
Cypresses kwa kawaida zinachukua muda mrefu kidogo. Pines watu wanaweza kuvuna zikiwa na miaka hata kumi lakini kwa kweli ni vizuri kuvumilia kidogo angalau ifikie miaka kama 15 hivi kwani hapo kipato chake kinaweza kuwa maradufu. Sina uhakika na hali ya hewa ya Moshi kama Pines zinastawi vizuri.
 
Ardhi ya kupanda miti kama pines bado ni nyingi sana hasa kwenye karibu ya mkoa wote wa Njombe has kwenye wilaya za Njombe, Ludewa na Makete. Nadhani kuna sehemu za mkoa wa Rukwa na mbeya miti hii hustawi vizuri pia.

Mimi nawatia moyo nyote ambao mnataka kupanda miti kufanya hivyo. siyo lazima uwe na kipato kikubwa sana. Huu ni mradi mzuri kwa wafanyakazi. Mimi nimepanda miti kutumia mshahara wangu tu. Tunaweza kupishana kipato lakini panda angalau eka 10 au 20 kwa mwaka. Ni gharama ndogo tu. Hata mimi mshahara wangu siyo mkubwa sana lakini kwa uvumilivu sana nimeweza kupanda miti ya kutosha.

Kazi ya kupanda inafanyika mwezi wa 12 kwa mikoa ya kusini. Ukishapanda huo mti unasubiri miaka ya kustaafu basi unaanza kuvuna. Ni kiunua mgongo kizuri kwa wafanyakazi. Lakini ukiwa kijana bado ni kipato tosha na cha uhakika kwa kila mwaka. Mbao za Tanzania zinauzwa Kenya, Uganda, South Sudan, Somalia na Uarabuni. Kwa sasa hivi mbao za Tanzania hazitoshi kwa hiyo wapasuaji wanakwenda mpaka Malawi kununua miti huko.

Uzuri mwingine wa kupanda mti ni kuwa unawatia hamasa wenyeji wa eneo utakalopanda miti. Wakati naanza kupanda miti pale kijijini nilikuwa karibu peke yangu tu. Baada ya kuwashauri wanakijiji nao kufanya kile nilichokuwa nafanya nao wakaanza kupanda miti. Leo hii kijiji kimezungukwa na mashamba mengi ya miti ya wanakijiji. Baada ya miaka mitano uchumi wa kile kijiji utapaa sana kwani nitakuwepo kuhakikisha hawalaliwi na walanguzi wa miti.
 
KVM naona hii kazi uliinza muda mrefu kidogo, mimi binafsi naipenda sana hii biashara maana nilishawahi onja utamu wa pesa yake baada ya kuuza miti kidogo niliyopanda nikiwa sekondari. Nimefanikiwa kunua ekari 200 huko njombe najipanga kuanza kupanda january 2013 na 2014 ili mwaka 2022 niwe milionea sio kuanza kulalamikia mafao!
 
Shime na hongera nyingi. Utafanikiwa tuuuuu!
 
Kwa mti unaoweza kutoa angalau mbao tatu ndefu za 2" x6" hiyo bei ni ndogo sana ukilinganisha na atakachopata mnunuzi. Ubao mrefu wa 2x6 na uliopakwa dawa DSM una siyo chini ya Shs 17,000. Bei ya mti moja pale Mafinga (Sao Hill) ni zaidi ya Shs. 50 000. Tatizo kule vijijini watu wananunua vimiti vichanga sana.
 
Kuna mwenye data za gharama za upasuaji na usafiri wa kuleta mbao Dar ili tuweze kulinganisha tofauti ya kuuza miti na kupasua mbao mwenyewe? Vilelive hiyo miti ya Sao Hill inayouzwa shs 50,000 ina umri gani tulinganishe na umri wa miti ya wakulima wadogo wanauuza shs 10,000 kwa mti. Je, umbali kutoka kwnye barabara kubwa au Dar, kwa mfano, Njombe vs Iringa unaleta tofauti kiasi gani kwenye bei ya miti?

Asante.
 
Kuna mwenye data za gharama za upasuaji na usafiri wa kuleta mbao Dar ili tuweze kulinganisha tofauti ya kuuza miti na kupasua mbao mwenyewe? Vilelive hiyo miti ya Sao Hill inayouzwa shs 50,000 ina umri gani tulinganishe na umri wa miti ya wakulima wadogo wanauuza shs 10,000 kwa mti. Je umbali kutoka kwnye barabara kubwa au Dar, kwa mfano, Njombe vs Iringa unaleta tofauti kiasi gani kwenye bei ya miti?

Asante.

Kwa sasa hivi sina gharama za upasuaji wa miti. Kwa kweli upasuaji karibu wote kwa sasa unafanywa pale Mafinga kwenye misitu ya serikali kwani huko vijijini ni kama miti imekwisha kabisa. Ni vigumu sana kwa mfano kupata miti kwenye plot moja ambayo unaweza kupasua na kujaza semi-trailer moja. Naweza kusema hali itakuwa hivyo kwa karibu miaka kumi ijayo kwani ni sasa tu watu wengi wameanza kupanda miti kwa wingi sana.

Miti wanayouza Sao Hill ina umri wa miaka 25 na kuendelea. Huko vijijini mti hata uwe mkubwa kiasi gani wanunuzi watanunua sana sana kwa Shs 20,000. Lakini kwa sasa hakuna miti huko vijijini, labda eucalyptus.

Wakati wa boom wa mbao kule Njombe na Makete watu wengi walikuwa wanasafirisha mbao kwa kutumia TAZARA. Hata hivyo miti mingine husakwa vijijini ambako kwingine hakuna usafiri mzuri sana. hata hivyo nimeshuhudia wanunuzi wa miti wakichimba barabara ili kutoa mbao zao.

Kuhusu kuuza mti au kuupasua mimi ningependelea kuupasua mimi mwenyewe na kuuza mbao. Lakini inategemea una miti kiasi gani. Kama unayo michache ni afadhali kuuza miti.
 
hii mitiki(teak) inachukua muda mrefu sana kuwa na bei nzuri ni ya miaka 15 na kuendelea, ila ukiwa unafanya thining ya shamba unaanza kuuza kuanzia miaka saba, na ina hela mti unaweza fika hadi milioni moja(wanatumia kwa nguzo za umeme ,kujenga meli na fenicha za gharama) , kuhusu mbegu sifahamu ila european union wanafadhili mradi huko kilombero nasikia tayari wana hekta 3000

Tuwe waangalifu na utoaji wa data zenye matata ili kutunza hadhi ya jukwaa. Tunajua mitiki ni gharama ila hiyo bei (in red font) kwa mti haileti mantiki.
 
Kwa sasa hivi sina gharama za upasuaji wa miti. Kwa kweli upasuaji karibu wote kwa sasa unafanywa pale Mafinga kwenye misitu ya serikali kwani huko vijijini ni kama miti imekwisha kabisa. Ni vigumu sana kwa mfano kupata miti kwenye plot moja ambayo unaweza kupasua na kujaza semi-trailer moja. Naweza kusema hali itakuwa hivyo kwa karibu miaka kumi ijayo kwani ni sasa tu watu wengi wameanza kupanda miti kwa wingi sana.

Miti wanayouza Sao Hill ina umri wa miaka 25 na kuendelea. Huko vijijini mti hata uwe mkubwa kiasi gani wanunuzi watanunua sana sana kwa Shs 20,000. Lakini kwa sasa hakuna miti huko vijijini, labda eucalyptus.

Wakati wa boom wa mbao kule Njombe na Makete watu wengi walikuwa wanasafirisha mbao kwa kutumia TAZARA. Hata hivyo miti mingine husakwa vijijini ambako kwingine hakuna usafiri mzuri sana. hata hivyo nimeshuhudia wanunuzi wa miti wakichimba barabara ili kutoa mbao zao.

Kuhusu kuuza mti au kuupasua mimi ningependelea kuupasua mimi mwenyewe na kuuza mbao. Lakini inategemea una miti kiasi gani. Kama unayo michache ni afadhali kuuza miti.

Assante kwa majibu yako;

Natumaini unafahamu kuwa tuna umoja wetu wa misitu wengi wetu ni members was jamiiforums. Kama hufahamu ningependa tuwasiliane ili ufahamu tunafanya nini na jinsi ya kuweza kuwasiliana. Organizer wetu ni Malila na tumepanda mamia ya ekari msimu huu. Na baadhi wamekuwa wakinunua mashamba ya wanakijiji ya ekari chache.

Kama hufahamu kuhusu umoja wetu wa misitu na ungependa kujua tunachofanya wasiliana na Malila ili tuweze ku share information.

Asante.
 
Tuwe waangalifu na utoaji wa data zenye matata ili kutunza hadhi ya jukwaa. Tunajua mitiki ni gharama ila hiyo bei (in red font) kwa mti haileti mantiki.
Tuwe tunafanya utafiti kabla hatujakosoa post za watu, kuna hadi taarifa kwamba kuna mtiki umewahi uzwa hadi $20,000!.kwa bei nyingi wana state $500 kwa cubic mita ambapo mti mmoja unaifikia na kupita, hapo bado hujauza maranda kama veneer, tatizo letu hatupendi kutafiti , bila shaka european union wasingewekeza $29million kama isingekuwa na hela nzuri, ukiachana na hayo nilisoma kwenye kijarida cha mazingira huko kilwa kuna kijiji walikuwa wanauza magogo kwa Tsh 1.2miliioni, biashara ya magogo ina hela mno ndio maana yule mtoto wa nguema ni tajiri sana.
 
Assante kwa majobu yako;

Natumaini unafahamu kuwa tuna umoja wetu wa misitu wengi wetu ni members was JamiiForums. Kama hufahamu ningependa tuwasiliane ili ufahamu tunafanya nini na jinsi ya kuweza kuwasiliana. Organizer wetu ni Malila na tumepanda mamia ya ekari msimu huu. Na baadhi wamekuwa wakinunua mashamba ya wanakijiji ya ekari chache.

Kama hufahamu kuhusu kuhusu umoja wetu wa misitu na ungependa kujua tunachofanya wasiliana na Malila ili tuweze ku share information.

Asante.

Asante. nitawasiliana naye.
 
Back
Top Bottom