Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

Mwenye uzi uliuliza na umepata msaada wa wataalamu ila hujaonesha ka umechukua au unahitaji ya ziada.
 
Bahati mbaya wachina wamegundua Mashine zooote,kasoro ya kutengeza hizo ice cream kama unavyoziita.

Ice cream halisi ni zile zinauzwa mwenye cone,kibakuli ama wanazopaki mwenye kopo za plastic.

Hizo kama kwa picha hapo juu,siyo ice cream,maana hazina cream,hapo tumezoea kuziita ice cream, lakini kama unatumia sealer kuzifunga,labda tafuta na filler ili Mashine I we inajaza na kuseal outomatically kuongeza uzalishaji.
 
korino,

Hongera sana kaka, nisaidie nami ni vitu gani Unachanganya na kwa namna gani hadi kuleta kiwango cha ubora na kupendwa na walaji.
 
korino,

Mwenzenu mgeni bado napata changamoto ktk kutumia jukwaa hili kuuliza kwa kureply ujumbe wa mtu nafanyaje?
 
Hongera sana kaka, nisaidie nami ni vitu gani Unachanganya na kwa namna gani hadi kuleta kiwango cha ubora na kupendwa na walaji
Inategemea ni aiskirim gani unazozitaka...zipo za aina tofauti
 
Yaan askirim zangu zina ubora kila anaezila anasifia! Natengeneza za maziwa zenye ladha mbalimbali km vanilla, strawbery, banana na chocolate pia.. Ni tamu mno!
Mkuu naweza kukutembelea kwa ajili ya kujifunza? Mm niko Sumbawanga kwa sasa wewe uko wapi?
 
Wakuu hebu acheni utani yani mtuu uko na wazo unataka watu wakumwagie plans, akumwagie strategy, akupen na budget zote, hebu tuwe na mitizamo mirefu jamani hilo swala utakalo ni swala la utafiti tena kwenye tasnia husika na hakuhitaji majibu mwepesimepesi.
 
Kama una friji haifiki hata 40,000 labda kama utataka kununua cooler box al maarufu deli.
 
Nataka nianzishe biashara ya kuuza icecream kama za bakhresa na juice fresh wadau nani keshawahi kuifanya hii biashara?

Nahitaji nini na nini/vifaa?

Mtaji ni kama shilingi ngapi?

lol:israel:
Mkuu kma uko tayari naweza kukuunganisha na mtu moja kwa moja ambae anaweza kukushauri juu ya hio biashara na machine unayotka.

Anaweza akakuundia kabisa kwa bei nafuu.
 
Back
Top Bottom