Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

Hapana mkuu, sijawahi kuifanya hii biashara, wazo lako ni zuri la kufanya biashara na kujikwamua kimaisha, kama unavyojua vijana wengi hawana kazi wanasubiri kuajiriwa. Usisahau kadi ya machinga.

Kazi ya kutengeneza ice cream, mali ghafi (maziwa) ipo kwa wingi, nadhani utahitaji friza kwa ajili ya kugandishia.
 
Kwanza kabisa nenda Instagram kuna mtu mtu mmoja anawaletea Sana watu machine za kutengeneza ivo vitu anajiita biashara china kamuangalie hautokosa chochote kitu.
 
Asante Sana mkuu
Hapana mkuu, sijawahi kuifanya hii biashara, wazo lako ni zuri la kufanya biashara na kujikwamua kimaisha, kama unavyojua vijana wengi hawana kazi wanasubiri kuajiriwa. Usisahau kadi ya machinga.

Kazi ya kutengeneza ice cream, mali ghafi (maziwa) ipo kwa wingi, nadhani utahitaji friza kwa ajili ya kugandishia.
 
proskaeur,
Ingia instagram mtafute dada anaitwa queennenelwa au nelwas gelato. Huyu dada anajishughulisha na hayo mambo ya ice cream na amefika level za kimataifa. kupitia account yake huenda ukajifunza vitu au kumtafute yeye mwenyewe.
 
Waafrika bado sana kusaidiana kwenye biashara. Kule insta naona kuna pages za kufundisha huu ujasiliamali.
 
Ingia instagram mtafute dada anaitwa queennenelwa au nelwas gelato. Huyu dada anajishughulisha na hayo mambo ya ice cream na amefika level za kimataifa. kupitia account yake huenda ukajifunza vitu au kumtafute yeye mwenyewe
Nimemfuatilia sana youtube huyu"NELWA GELATO" yuko vizuri na ni kati ya watu walionivutia kufanya huu ujasiriamali
 
Je, wajua utengenezaji wa ice cream unaweza kubadili maisha yako? Utashangaa right? Ndio ice cream hizi hizi unazozijua za kutengeneza kwa mikono yako. Kutokana na wingi wa vijana wengi kua mtaani na kuwa tegemezi kwa madai kwamba hawana cha kufanya nimeona nifanye ku share hapa.

Ice cream ni biashara nyepesi na yenye pesa ukijua tu jinsi ya kuitengeneza kiutaalam can u imagine 20k a day? Just kwa kuanzia before hujajitanua zaidi? Mimi nimekua nikifanya hii biashara kwa miezi sita sasa kwakweli inanilipa. Kuna ice cream za aina nyingi na cha muhimu zaidi ni package yako, usinielewe vibaya; hapa naongelea "home made " ice cream ambayo nauza moja kwa 200/300, trust me it pays.

Vijana wenzangu tusio na ajira mimi na elimu yangu ya degree nimjasiliamali ambaye nafanya vitu tofauti tofauti vya kujiajiri. Nakushawishi pia uanze kufikiria kujiajiri si lazima uwe na pesa nyingi ndio uanze safari ya ujasiliamali. Ice cream zinahitaji raw material kidogo na nirahisi kupatikana. Let's think out of the box. If you are interested ask me how.
 
Hello friends ...

Naomba nijibu maswali yenu hapa. Kama nilivosema mwanzo kuna aina nyingi za icecream ila pendwa sana ni za maziwa. Mie hutengeneza za maziwa na za ubuyu, nianze na za maziwa.

MAHITAJI
1. Maziwa ya unga
2. Sukari
3. Maji
4. Ladha (vanila)
5. Rangi ya chakula ( mie hutumia yellow)
6. Kilainishi(optional)
7. Vifungashio

Sasa hapa unakua na vipimo vyako mwenyewe mfano kwa mahitaji ya icecream 70 za maziwa

1.Maji lita tano( yalochemshwa au weka water guard kurahisisha)
2. Maziwa ya unga robo kilo (tsh 3250)
3. Sukari robo kilo (tsh 650)
4. Ladha ya vanila (tsh1,000) hii utatumia vifuniko viwili tu au vitatu vya kichupa....
5. Kilainishi(tsh 500) kijiko kimoja cha chakula changanya material yako hayo namba moja hadi nne, kisha weka rangi yako (tsh 100 tu) kidogo tu. Baada ya hapo kilainishi unakiweka kwenye blenda unachanganya maji nusu kikombe ule uji wake weka kwenye mchanganyiko wako. Congratulations bidhaa yako ipo tayari funga ktk vifungashio (tsh 500) vyako kisha weka kwa fridge yako tayari kupokea pesa.

Mahitaji 3250+1000+650+500+500+100 =600

Mapato 70@200 =14,000
14,000-6,000= 8,000
net profit 6,000
Mahitaji kama ladha, rangi, vifungashio na kilainishi utatumia hadi mara 5 bila kununua tena imagn unaweza kuuza icecream 100 tu kwa siku.

100 x200=20,000 kwa siku mara siku 30 sawa na 600,000 kwa mwezi toa gharama za uendeshaji unacheza kwenye laki nne. Fikiria sasa kutanuà soko lako. Ni zaidi ya mshahara wa degree holder.

Ubuyu ndo cheaper zaidi. Oh I love this biz nakushawishi ufikirie. Mkihitaji ya ubuyu nitaelekeza pia.
 
Ice cream 200 wapii. Kwa huku uswahilin wateja n watot. So approximately bei n 100.

Half pia mdau jaribu kuweka maelezo ili lengo kuu la uzi wako litimie. Umetuacha njiapanda
 
Back
Top Bottom