Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

Mie nafanya kwa huku kwenye Duka langu.
Nitakupa kwa ninavyojua mie.
Kwanza unaenda kwao wanakupa Bei ya Jumla.
Faida sio kubwa sana ila lazima duka lako liwe na vitu vya ziada na sio kutegemea Ice cream peke yake unless uwe na flow kubwa.

-Fridges:-
Kwanza hakikisha una Fridges zenye uweo mkubwa,chukua kopo la Azam na usome na kujua inatakiwa iwe kwenye Baridi ya degree ngapi.Jaribu kuwauliza wao kuna kipindi walikuwa wanayauza yale ya kwao.Kama upo Dar nasikia bado utaratibu huo upo.Yale yao ni makuubwa sana na ni Heavy duty na pia ni dhamana kwa kazi hii.Ila lazima ununue na bei yake sio ya kitoto.Milioni na kitu kama sikosei.
Angalizo,Ice cream zina contents ambazo zinafanya usichanganye na kitu chochote katika uhifadhi,kuwa makini sana na hili.Huwa hazipendi kabisa kuwekwa ndani na kitu kingine,la sivyo utaona kila kitu kina ganda ila zenyewe hazigandi,fundi atakula hela hapo mpaka basi.So,Fridge ukiweka Ice cream zile basi weka zenyewe tu au pamoja na chockstik.Na umeme ukikatika muda mfupi tu basi zinayeyuka kulingana na vitu vingine vilivyomo humo.
Kama utakosa kwao basi nakushauri nunu Fridge Jipya kwa ajili ya Ice cream.
-Umeme
Umeme ukikatika,hapa itabidi iwe tatizo sana,hasa kwenye baadhi ya bidhaa,sasa lazima uwe mjanja kwenye upangaji wake,ili usiwe unalifungua muda muda mrefu kutafuta size ya Ice cream anayoitaka mteja,maana hewa ya nje ni ya mvuke wa joto,sasa hufanya kuyeyuka haraka sana pindi umeme ukiwa hakuna.Lakini ukipanga vizuri itakusaidi kwamba kama umeme haupo basi unafungua tu na ku pick anachotaka mteja.Tatizo kubwa ni pale itakapofika masaa kuanzi 6 - 8 bila umeme ndio issue.Hasa kwenye chocksick.
-Bidhaa:
Mbali na Ice ceam jaribu pia kuuza chockstik kwa jina maarufu,huwa zinatoka vizuri kwenye biashara,mie kwangu ndio zinaoongoza kwenye mauzo,maana nipo karibu na shule International School

Nikikumbuka jingine nitakuja.Ila kwa ufupi ukipata sehem nzui ni biashara nzuri.
Mie nimeweka,Ice cream,chockstic,nauza Fruits,Juices,Coffee maana nina coffee maker,na pia Maji.Na Vitafunwa mbalimbali.
Na katika vitafunwaa mbalimbali imenifanya nipate mpaka order za maharusi mbali mbali na shughuli mbali mbali,yaani bila kutarajia nayo imekuwa biashara kubwa.Mfano upande wa orders nyingi ni Sambusa,Katless,chapati za maziwa,bagia,Cakes nk,na pia huwa baadhi ya siku navamia dayoutings za watu na kuwashauri niwafanyie picnic lunches,maana biashara nyingine lazima ujifanye hamnazo ili yako yaende.
Ni biashara nzui,zingatia sana usafi.
Mie mwakani natarajia kufungua kama hii huko Dar es Salaam.
Asante sana kwa ushauri mzuri mkuu, barikiwa sana sana.
Vipi faida yake ikoje mkuu? I mean Ice cream
 
Changamoto mpya... Marufuku ya serikali juu ya matumizi ya vifungashio vya plastic. Serikali inaruhusu vifungashio ambavyo vina nembo ya TBS tu. Kwa wajasiliamali wadogo hii ni changamoto mpya
 
Habari za mihangaiko wasakatonge wenzangu

Kwasasa nipo MBEYA naomba kujua kwa wale wazoefu wa uzalishaji wa ice lolly (lambalamba) mambo yafuatayo:
Vifaa hasa vya uzarishaji.
Gharama za uendeshaji
Changamoto zake
Soko lake pia(japo mimi nimetarget kwa wanafunzi wa sekondari Pekee).

Kutegemee mshahara pekee naona itanichikua mda mrefu kufikia malengo yangu...

Natanguliza shukurani
 
Hapo kwenye ladha huwezi weka ladha tofauti na vanilla?
Dah!! Mimi nilipo maziwa fresh lita bei rahisi sana so natengeneza za maziwa matupu bila maji ... zipo vizuri sana tatizo soko lipo chini sana...
 
Dah!! Mimi nilipo maziwa fresh lita bei rahisi sana so natengeneza za maziwa matupu bila maji ... zipo vizuri sana tatizo soko lipo chini sana...
Tafuta masoko hasa mashuleni na masokoni huko kuna hela!! Usisubir wakufate ulipo
 
Njoo nikuuzie na machine ya cone upige pesa.
Habari za mihangaiko wasakatonge wenzangu

Kwasasa nipo MBEYA naomba kujua kwa wale wazoefu wa uzalishaji wa ice lolly (lambalamba) mambo yafuatayo:
Vifaa hasa vya uzarishaji.
Gharama za uendeshaji
Changamoto zake
Soko lake pia(japo mimi nimetarget kwa wanafunzi wa sekondari Pekee).

Kutegemee mshahara pekee naona itanichikua mda mrefu kufikia malengo yangu...

Natanguliza shukurani
 
Hello friends ...

Naomba nijibu maswali yenu hapa. Kama nilivosema mwanzo kuna aina nyingi za icecream ila pendwa sana ni za maziwa. Mie hutengeneza za maziwa na za ubuyu, nianze na za maziwa.

MAHITAJI
1. Maziwa ya unga
2. Sukari
3. Maji
4. Ladha (vanila)
5. Rangi ya chakula ( mie hutumia yellow)
6. Kilainishi(optional)
7. Vifungashio

Sasa hapa unakua na vipimo vyako mwenyewe mfano kwa mahitaji ya icecream 70 za maziwa

1.Maji lita tano( yalochemshwa au weka water guard kurahisisha)
2. Maziwa ya unga robo kilo (tsh 3250)
3. Sukari robo kilo (tsh 650)
4. Ladha ya vanila (tsh1,000) hii utatumia vifuniko viwili tu au vitatu vya kichupa....
5. Kilainishi(tsh 500) kijiko kimoja cha chakula changanya material yako hayo namba moja hadi nne, kisha weka rangi yako (tsh 100 tu) kidogo tu. Baada ya hapo kilainishi unakiweka kwenye blenda unachanganya maji nusu kikombe ule uji wake weka kwenye mchanganyiko wako. Congratulations bidhaa yako ipo tayari funga ktk vifungashio (tsh 500) vyako kisha weka kwa fridge yako tayari kupokea pesa.

Mahitaji 3250+1000+650+500+500+100 =600

Mapato 70@200 =14,000
14,000-6,000= 8,000
net profit 6,000
Mahitaji kama ladha, rangi, vifungashio na kilainishi utatumia hadi mara 5 bila kununua tena imagn unaweza kuuza icecream 100 tu kwa siku.

100 x200=20,000 kwa siku mara siku 30 sawa na 600,000 kwa mwezi toa gharama za uendeshaji unacheza kwenye laki nne. Fikiria sasa kutanuà soko lako. Ni zaidi ya mshahara wa degree holder.

Ubuyu ndo cheaper zaidi. Oh I love this biz nakushawishi ufikirie. Mkihitaji ya ubuyu nitaelekeza pia.
Naomba unielekeze kiundan kuhus biashara
 
Habari zenu! Nauza askirimu hizi za mitaani za watoto (wakubwa pia)

Nina viajana wawili wanatembeza mashuleni.

Nahitaji kukuza biashara yangu napendelea niuze jumla na rejareja pia. Ila changamoto niliyonayo ni machine kwaajili ya kutengenezea hizo askirimu. Kwa sasa natumia impulse sealer. Nahitaji nitengeneze kwa wingi na kwa muda mchache.
Ni mashine gani ambayo naweza kutumia?

Na kingine naombeni ushauri wenu wakitaalam namna ya kufanya biashara ikuwe. Nahitaji mawazo yenu na ushauri wenu!

Ahsanteni

Bado unauza ice creamu? Nimeona umesena unauza jumla, naomba kama bado unauza kwa jumla tuwasiliane uniuzie. Nataka nianze mwaka kivingine!
 
Mbeya kungekua hakuna soko basi bakharesa asingeleta ice roll ya ukwaju na maziwa. Na anafanya kazi mwaka mzima.
Kama walivosema wana jamvi hapo juu kikubwa Ni ubunifu.
 
  • Thanks
Reactions: PYD
Back
Top Bottom