Biashara ya kutengeneza na kuuza "Askrimu" (Ice Lollies)

Mkuu

Hiyo Biashara Inaonekana Ya Kawaida Japo Ukweli Ina Pesa Sana Maana Wateja Wengi Sana. Jambo Muhimu Kwenye Uandaaji Wa Hizo Bidhaa Kwenye Ubora . Nunua Ubuyu Ambao Wengi Huutumia Huo Unauchemsha Jikoni Uive Vizuri Unachunywa . Nunua Ladha Ambayo Huchanganywa Kwenye Huo Mchanganyiko . Mengine Kama Members Walivyoshauri Hapo Juu Yaani Ni Huo Huo
 
Mahitaji
(kwa mahitaji haya utatoa zaidi ya pisi 200 za barafu ukitumia vifuko vya size 1¼ X 10)
Maji lita 7
Maziwa ya unga 1 cup (brand yoyote)
Unga wa wanga (corn starch) 2 cups uchanganye na maji lita 1.5 (unga wa wanga unauzwa supermarket) au sokoni unga wa ubuyu
Sukari kilo 1¾ (waweza punguza)
Chumvi ½tsp (ukipenda)
Utaweka ladha uipendayo (vanilla, mango, chocolate, pineapple, nk) Mifuko 300 ya kufungia ice candy (mifuko ya barafu)
HATUA:
1. Weka maji lita 7 kwenye sufuria kubwa na weka jikon yachemke, ongeza sukari na chumvi(ukipenda), kisha changanya vizuri hadi viyeyukie humo .
2. Ongeza ile corn starch na maziwa ya unga kwenye hayo maji yanayochemka, koroga vzr ili kusitokee mabujabuja, chemsha kwa dk 8, kisha zima jiko, acha ipoe kwa saa kadhaa kisha ongeza ladha uipendayo.
3. Funga kwenye vile vifuko na gandisha hadi ziwe barafu.

Kwa hisani ya Numbisa Jinsi ya kutengeneza barafu za kula, ice crem
Umenisaidia sana
 
Habari zenu! Nauza askirimu hizi za mitaani za watoto (wakubwa pia)

Nina viajana wawili wanatembeza mashuleni.

Nahitaji kukuza biashara yangu napendelea niuze jumla na rejareja pia. Ila changamoto niliyonayo ni machine kwaajili ya kutengenezea hizo askirimu. Kwa sasa natumia impulse sealer. Nahitaji nitengeneze kwa wingi na kwa muda mchache.
Ni mashine gani ambayo naweza kutumia?

Na kingine naombeni ushauri wenu wakitaalam namna ya kufanya biashara ikuwe. Nahitaji mawazo yenu na ushauri wenu!

Ahsanteni
 
Umenikumbusha biashara yangu ya mwanzoni kabisa ya aiskirimu na barafu,.mm sikuwa natumia mashine yoyote kwenye utengenezaji wa bidhaa zangu hizo,so kuhusu mashine sijafuatilia na wala sina ufahamu wa kutosha juu ya hilo,.kwenye kukuza biashara yako hiyo ongeza mtaji,tafuta soko jipya,boresha bidhaa yako ikiwezekana tafuta vifungashio vyako vya tofauti pia ongeza vionjo/weka vionjo vipya na vizuri kuwavutia wateja ilu kuongeza thamani ya bidhaa yako,.

Natamani kuifanya tena hii biashara.

tapatalk_1516219751888.jpeg
 
Habari zenu! Naombeni msaada tena. Msinichoke! Nina kijana ananiuzia askirimu mashuleni. Naishi nae mwenyewe nmempa rum mahitaji yote juu yangu! Kwa mwezi tunaingiza faida ya laki NNE je mshahara wake nimpe sh.ngapi?

Nisaidieni mawazo
 
Kwa mwezi tunaingiza faida ya laki NNE je mshahara wake nimpe sh.ngapi? Nisaidieni mawazo
Ni vyema ukamlipa vizuri, ili fedha ya mauzo iendelee kuonekana.

Waweza kumlipa 1/4 ya hicho kiasi, lengo assingiwe na tamaa ya kukuibia, na ili aipende zaidi kazi yake.

Uwe unakuwa naye karibu itamjenga zaidi na kuithamini biashara yako.

Kila lakheri
 
Ni vyema ukamlipa vizuri, ili fedha ya mauzo iendelee kuonekana.

Waweza kumlipa 1/4 ya hicho kiasi, lengo assingiwe na tamaa ya kukuibia, na ili aipende zaidi kazi yake.

Uwe unakuwa naye karibu itamjenga zaidi na kuithamini biashara yako.

Kila lakheri
Asante kwa ushauri. Najitahd kuishi nae vema! Namhudumia kila kitu na vya ziada pia.
 
Yaan askirim zangu zina ubora kila anaezila anasifia! Natengeneza za maziwa zenye ladha mbalimbali km vanilla, strawbery, banana na chocolate pia.. Ni tamu mno!
Naomba kujua kwa kuweka vionjo ivo, unakua unauza bei gani,!? Unatumia vifuko ivo vya kama kwenye iyo picha hapo juu!?
 
Yaan askirim zangu zina ubora kila anaezila anasifia! Natengeneza za maziwa zenye ladha mbalimbali km vanilla, strawbery, banana na chocolate pia.. Ni tamu mno!
Ukitia hizo chocolate, strawberry na banana unaziblend au unafanyage.
 
Mkuu nimeona uko na fursa adimu sana, mie naheshimu biashara ndogo sana maana najua ndizo zinanyanyua mtuu. mkuu kuna mashine inaitwa CHILA, inauwezo wa kugandisha kitu ndani ya DK45 so sijajua ka speed yake itakufaa pia haiweki barafu yenyewe inakuwa na maji na barafu au chochote kinaganda humo kwenye maji pasipo shida yoyote, mengine utakayohitaji nitakusaidia endapo utaona mashine hiyo inafaaa.
 
Back
Top Bottom