Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,472
- 40,470
Biashara yoyote inahitaji uvumilivu; wengi wanaamua kufunga biashara zao na kulalamika kwa sababu wanakuwa wamekosa uvumilivu.
Na hasa ukiingia kwenye hii biashara ya kutengeneza na kuuza, muda mwingi wewe unakuwa unatoa pesa tu; mpaka uje uanze kuona faida inachukua muda mrefu.
Unapotaka kufanya biashara yenye mafanikio, ni lazima uwe na mtazamo wa mjasiriamali ''entrepreneur''; ambaye kwake kupata pesa, ni chaguo la pili na si la kwanza.
Biashara inaweza kuchukua miezi na miezi au miaka na miaka, mpaka kuja kukupa faida unayoitaka; muhimu uwe umeiwekea misingi mizuri ya kufika kule unakotaka kufika.
Mwanzoni ni lazima ukubali kupoteza pesa, ili baadaye ndio uje upate pesa.
Kwa mtu anayejiingiza kwenye biashara ya kutengeneza na kuuza; huyu anaingia gharama kubwa sana kuliko yule aliyeingia kwenye biashara ya kununua na kuuza (uchuuzi).
Ila huyu, anayetengeneza na kuuza (entrepreneur), huko mbeleni atakuwa na mafanikio makubwa sana, kwa sababu inampelekea kwenye kumiliki kiwanda kama sio viwanda.
Kama mjasiriamali, utajisikiaje pale unapotembelea duka la kwanza mpaka la 50 n.k, unakuta linauza bidhaa zako?
Kwa kifupi, hii biashara inalipa ingawa inachukua muda mrefu.
Karibu kwa maswali.